Je, ni sahihi mkristo kufunga ndoa mwezi huu wa ramadhani?

Je, ni sahihi mkristo kufunga ndoa mwezi huu wa ramadhani?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Je ni sahihi mkristo kufunga ndoa mwezi huu wa ramadhani?

Maana miongoni mwa watu waliomchangia pesa ya harusi ni waislamu na waislamu muda huu wapo kipindi cha mfungo na hata baadhi ya wakristo nao wanawasindikiza waislamu katika ibada hii ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Hivyo kufunga harusi mwezi huu kunawanyima fursa wengi kuhudhuria kwenye hiyo harusi.


..............
Kutoa hoja kwamba harusi inafanyika usiku napo ni batili,shamra shamra zote zinaanzia tangu asubuhi.

Usiku ni kuhitimisha tu
 
Wanahudhuria mbona. Sherehe ukumbini ni usiku.
 
Wiki ijayo pia mfungo kwa wakristo unaanza yaani kwaresma. Wakati wa mfungo huo arusi Huwa hazifungwi pia.

Ila kwa kipindi hiki Cha Ramadan kama Kuna arusi ya mkristo, muislam anaweza kuhudhuria maana sherehe hufanyika usiku.
 
Yani watu waheshimu jambo laki la harusi ila wewe usiheshimu funga zao?

Majority ya watu wanafurahia harusi ambazo bia zipo kama bia hamna usitegemee michango ya kueleweka.
 
Kwahiyo wewe pombe unakunywa kwa sababu mchango ulioutoa ni mkubwa sana? Kwahiyo mwezi ukiisha ruksa kurudi kwenye ulevi sio?
Kwani kuna dini inayoruhusu pombe?.

Unachangisha michango mikubwa kwa lengo lipi?
 
Kwenye harusi ukichangia ni kufanikisha lengo la shughuli; hakuna ulazima wa kuhudhuri wala kula .
 
Kwani kuna dini inayoruhusu pombe?.

Unachangisha michango mikubwa kwa lengo lipi?
Unapofunga mwezi mtukufu unatakiwa ubadilike uache kila kitu ambacho hakimpendezi Mungu na sio uache kwa huo mwezi tu, bali hata baada ya huo mwezi.
Sasa ukienda kwenye harusi ukila chakula na juice na maji au vinywaji vingine unakuwa haujasherehekea?
 
Unapofunga mwezi mtukufu unatakiwa ubadilike uache kila kitu ambacho hakimpendezi Mungu na sio uache kwa huo mwezi tu, bali hata baada ya huo mwezi.
Sasa ukienda kwenye harusi ukila chakula na juice na maji au vinywaji vingine unakuwa haujasherehekea?
Yani ni sawa kwenye harusi uwachangishe watu pesa kisha ukawalisha ubwabwa maharage au ugali.
 
Ni busara yako tu lakini ni ruksa kufunga ndoa kipindi hiki!
 
Huu ndio ukenge. Kila kitu udini dini tu. Kama ulishindwa kugharamia gharama za harusi wewe na familia yako hadi ukachangisha watu subirie wafungulie ndio ufunge vinginevyo uwaandalie vyombo vya kubebea msosi ili wakale huko makwao wakati wa ifutar.
 
Haina kikwazo, sherehe/karamu hufanyika usiku mnene, watakula misosi muda huo
 
Maisha ya mtu mweusi ndani ya bara la Afrika ni ya kipekee sana 🐼
 
Back
Top Bottom