King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Tapeli yupo kwao Lubumbashi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na wewe umekosea kujiita “SET-FREE”, ni Yesu tu ndie mwenye uwezo wa kuwaweka huru wanadamuHalafu wewe, unakosea sana kujiita Father of All
Mungu pekee ndiye Father of All.
Soma Ephesians 4:6, NIV.
"One God and Father of all, who is over all and through all and in all."
Kiboko ya mchawi ni mchawi mwenzakeKimaandiko, kujiita "Kiboko ya Wachawi" sio sahihi kwa sababu inahamasisha kiburi na kujitwalia mamlaka ambayo ni ya Mungu pekee.
Sababu za Kimaandiko:
Yesu ndiye anayeangamiza kazi za shetani
1 Yohana 3:8 – "Kwa sababu hii Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Shetani."
Yesu ndiye mwenye mamlaka ya kuharibu kazi za shetani.
Hata wanafunzi walipopewa mamlaka ya kutoa pepo, waliambiwa watafanya hivyo kwa Jina la Yesu, sio kwa nguvu zao.
Marko 16:17 (SUV)
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya."
Luka 10:17
"Na wale sabini na wawili wakarudi kwa furaha wakisema, Bwana, hata pepo wametutii kwa jina lako."
Kwa Maandiko hayo tunaona kuwa ushindi dhidi ya wachawi na nguvu za giza unatokana na uwezo wa Jina la Yesu, sio nguvu za mtu binafsi. Hivyo ni bora tukawa wanyenyekevu kuliko kujitukuza na kujipa majina makubwa.
Yakobo 4:6-7 – "Mungu huwapinga wenye kiburi, bali huwapa wanyenyekevu neema..."
Badala ya mtu kujiita "Kiboko ya Wachawi," afadhali aseme:
"Mimi ni mtumwa wa Yesu Kristo au mimi ni mtumishi wa Mungu aliye hai."
Bulldozer ni jina la kiingereza ambalo generally lina-imply strength, forcefulness, and the ability to remove obstacles. Mtumishi wa Mungu akijiita hivyo yamkini atakuwa anajilinganisha na Nabii Yeremia. Katika kitabu cha Yeremia 1:10 tunasoma kwamba Mungu alimwambia Yeremia: “nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza...” Kwa kazi hiyo, tungeweza kumwita Nabii Yeremia Bulldozer. Lakini kazi aliyopewa Yeremia haikuwa hiyo tu ya kung'oa, kubomoa, kuharibu na kuangamiza. Aliagizwa pia kujenga na kupanda. Kwahiyo jina Bulldozer halimfai Yeremia, kwa sababu Bulldozer haina uwezo wa kujenga na kupanda.Bulldozer
Wewe umenukuu jibu langu kuhusu Mzee wa Upako, jibu ambalo halihusiani na swali lako. Nimeishaeleza kwa undani kuwa sio sahihi mtu kujiita kiboko ya wachawi. Kwahiyo hata wafuasi wake hawapaswi kumwita hivyo. Wachawi tunawashinda kwa Jina la Yesu, sio kwa nguvu zetuKwahiyo kàma wafuasi wake bdo walimwita kiboko ya wachawi ni sawa?
Brand name yako ni Mzee wa kuwapaka au sioKama mtu ameona kuna wajinga wengi huko asitafute brand name? Hilo ni jina la kibiashara , hata mimi maisha yakinipiga sana nafungua kanisa nakuja na mafuta ya nazi yanabadilisha jina alafu najiita mzee wa kuwapaka napiga hela alafu napotea
Sioni tatizo huyo akijiita hivyo.Kuna mwingine anajiita Muwakilishi wa Yesu
YeahBulldozer ni jina la kiingereza ambalo generally lina-imply strength, forcefulness, and the ability to remove obstacles. Mtumishi wa Mungu akijiita hivyo yamkini atakuwa anajilinganisha na Nabii Yeremia. Katika kitabu cha Yeremia 1:10 tunasoma kwamba Mungu alimwambia Yeremia: “nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza...” Kwa kazi hiyo, tungeweza kumwita Nabii Yeremia Bulldozer. Lakini kazi aliyopewa Yeremia haikuwa hiyo tu ya kung'oa, kubomoa, kuharibu na kuangamiza. Aliagizwa pia kujenga na kupanda. Kwahiyo jina Bulldozer halimfai Yeremia, kwa sababu Bulldozer haina uwezo wa kujenga na kupanda.
Katika Agano Jipya, agizo kuu tulilopewa na Yesu sio kung'oa, kubomoa, kuharibu wala kuangamiza. Katika Mathayo 28:19-20 Yesu anatuambia: “basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi...”
Yesu hajatuambia tufanye kazi aliyoambiwa Yeremia ya kung'oa, kubomoa, kuharibu na kuangamiza mataifa.
Labda mtu anaweza kusema anajiita Bulldozer kwa sababu kazi yake ni kumng’oa, kumbomoa, kumharibu na kumuangamiza shetani. Hiyo kazi pia hatujaagizwa. Shetani amewekewa moto wa milele(Mathayo 25:41), lakini saa yake ya kuangamizwa bado haijawadia. Kwa sasa tumeagizwa tu kumpinga shetani(Yakobo 4:7). Hata wachawi sio kazi yetu sisi kuwaangamiza, tunatakiwa kuwahubiri Injili na wao waokoke. Wasipotubu, wataangamizwa siku ya mwisho. Tunachopaswa kufanya ni kuvunja tu nguvu za kichawi.
Katika Matendo 13:8 kuna habari ya Elima, mchawi aliyeshindana na Paulo na kutaka kumzuia Sergio asisikie Injili. Mtume Paulo hakumuangamiza, alimkemea tu akawa kipofu kwa muda.
Katika kitabu cha Mathayo 23:5-12 Yesu aliwakataza wanafunzi wake kujiita titles kubwa kubwa kama Mafarisayo walivyokuwa wakifanya. Mafarisayo matendo yao yote waliyatenda ili kutazamwa na watu; walipenda kukaa viti vya mbele katika karamu; kuketi mbele katika masinagogi, kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, 'Rabi'. Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “...aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa...”
Tazama jinsi Yesu anavyoonyesha unyenyekevu katika Yohana 13:14 (SRUV)
“Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha miguu, imewapasa ninyi pia kuoshana miguu ninyi kwa ninyi.”
Katika Wafilipi 2:6-7 tunasoma tena juu ya unyenyekevu wa Yesu. Kwamba Yeye, kwa asili alikuwa daima Mungu; lakini hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kung'ang'ania kwa nguvu, akajifanya kuwa hana utukufu, akatwaa hali ya mtumishi, akaonekana kama wanadamu.
Mungu akituwezesha kufanya mambo makubwa, tujifunze kuwa wanyenyekevu kama Yesu. Tusijiite majina yanayotukweza; badala yake tumpe Mungu utukufu wote. Maana pasipo Yeye sisi hatuwezi kufanya lolote(Yn 15:5).
Al-mukheef , I’ve provided a detailed response—does this fully answer your question?
1 Petro 3:10-12Hakuna kosa. Anaweza kujiita hata kinyesi akitaka
Ungemwuliza yeye mwenyewe kwanini ajiite hivyo. Halafu tafuta kazi za kufanya.Kimaandiko, kujiita "Kiboko ya Wachawi" sio sahihi kwa sababu inahamasisha kiburi na kujitwalia mamlaka ambayo ni ya Mungu pekee.
Sababu za Kimaandiko:
Yesu ndiye anayeangamiza kazi za shetani
1 Yohana 3:8 – "Kwa sababu hii Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Shetani."
Yesu ndiye mwenye mamlaka ya kuharibu kazi za shetani.
Hata wanafunzi walipopewa mamlaka ya kutoa pepo, waliambiwa watafanya hivyo kwa Jina la Yesu, sio kwa nguvu zao.
Marko 16:17 (SUV)
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya."
Luka 10:17
"Na wale sabini na wawili wakarudi kwa furaha wakisema, Bwana, hata pepo wametutii kwa jina lako."
Kwa Maandiko hayo tunaona kuwa ushindi dhidi ya wachawi na nguvu za giza unatokana na uwezo wa Jina la Yesu, sio nguvu za mtu binafsi. Hivyo ni bora tukawa wanyenyekevu kuliko kujitukuza na kujipa majina makubwa.
Yakobo 4:6-7 – "Mungu huwapinga wenye kiburi, bali huwapa wanyenyekevu neema..."
Badala ya mtu kujiita "Kiboko ya Wachawi," afadhali aseme:
"Mimi ni mtumwa wa Yesu Kristo au mimi ni mtumishi wa Mungu aliye hai."