SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Nafikiri kuna haja ya Mahakama kuweka taratibu fulani za kuhakikisha mavazi wanayovaa watuhumiwa na washitakiwa wakiwa mahakamani hayana maandiko, picha au nembo yoyote.
Nimeona kuna mtuhumiwa wa ubakaji kafikishwa mahakamani akiwa ametupia jezi ya Ajax. Hii inaweza kutafsiriwa kama ni kuchafua brand ya Ajax. Itakuwaje kesho mwingine akifikishwa mahakamani amevaa jezi ya Yanga au Simba, itakuwa sahihi? Vipi akifika amevaa t-shirt ya Vodacom? Tuliangalie hili kabla halijaleta shida huko mbele ya safari.
Na hili nalo mkalitazame.