Je, ni sahihi Steven Mbazi kusimamia mali za Bilionea? Tumpe ushauri DC Jerry Muro katika utatuzi wa sakata hili la mali

hili tatizo linahitaji busara ya Mungu nalifananisha na tukio la Mfalme Sulemani na wanawake wawili wakigombania mtoto, mfalme akaamua mtoto akatwe wagawane vipande lakini mama halisi akagoma mtoto asikatwe bora yeye akose mtoto apewe mama mwingine...
 
Jerry Muro anajibebesha tu gunia la misumari. Huyo dogo inaonekana mjomba/ndugu wa mama yake wameshamharibu ubongo japo ana umri wa miaka 23 lakini utadhani ndio kwanza ana miaka 12 kama mtoto anayesumbuliwa na balehe. Huyo dogo akili zikija kukaa sawa atajikuta kabaki na boda boda tu. Ni wakati muafaka sasa kwa wazazi na ndugu wa Erasto Msuya kufungua kesi kwa hati ya dharura ili huyo mjomba aondolewe kwenye usimamizi iwapo kweli wana uhakika kuwa huyo mjomba anasimamia mali za marehemu isivyo halali na anazitapanya. Ijulikane wazi hata msimamizi halali wa mirathi iwapo anatapanya mali mahakama ina uwezo wa kumsimamisha kusimamia mali husika.

Kwa aliye karibu na ndugu wa Erasto Msuya awaambie kuwa kulumbana kwenye vyombo vya habari hakuwasaidii bali wachukue hatua za kisheria haraka ili mali zisizidi kupotea au kubadilishwa umiliki. Ni kweli wanaweza kuwa na uchungu wa kuwapoteza wapendwa wao lakini wajue kuwa kukaa kwao kimya au kusubiri mkuu wa wilaya awasuluhishe itakuwa ni suluhu ya muda tu. Lakini uamuzi wa mahakama ndio itakuwa suluhusho la kudumu na hata hao watoto wa Erasto Msuya watakuja kuwashukuru sana baadae watakapokuwa watu wazima na kukuta baadhi ya mali alizoacha baba yao zipo salama na zinawasaidia maishani.
 
Hyo familia hata kesi ikiisha na wakigawanya mali bado visasi vitaendelea. Mtoto wa marehemu Anety alieshuhudia damu zikitiririka toka chumbani kwa mama ake asubui na akija kujua aliefanya auliwe ni aunt yake lazima chuki iwepo na itaendelea kuwepo. Cha msingi ni kumuomba Mungu awasaidie
 
alieanza kuharibu ni mama wa uyo dogo kuua kwa mambo ya ajabu ajabu matusi tu, mjomba yeye hana shida na izo mali ila anatake profit mapemaaa,dogo alijichanganya ktk maneno yake yani dogo amekosea kuonyesha rangi yake kusaliti upande wa ukoo wako ni kosa kubwa sana babu na bibi ake,uyo dogo aachane na wotee amsikilize babu yake nini anasema,
 
Nimewahi shuhudia mjomba anauza mali za wajomba zake na walikuja shtuka ni vingi vimeuzwa.

Kelvin huenda anapotoshwa na mjomba ili mjomba akamue mali za babake.
Huyu mjomba aondolewe kwenye hiyo nafasi ya Msimamizi wa mirathi, mtoto mkubwa wa marehemu achukue nafasi hiyo.Pia, mjomba abanwe ili arudishe mali zote alizouza kinyemela, ikiwezekana afilisiwe mali zake ili kufidia.Kazi ya msimamizi wa mirathi cyo kuuza mali za marehemu bila ridhaa ya warithi wote
 
Hao watoto inaonekana hawajiwezi no wonder hata mama yao kamuamini kaka ake.
Huyo wa huko nje naona kaona ajikatae huko asahau mabalaa ya nyumbani.
 
Ukiwa napesa nyingi suluhisho nikumuandia mtu mmoja Mali zote kuepusha huu upuuzi. Atakma utakua nawatoto 6 dawa nikumpa mtu mmoja
 
tatizo kubwa naloliona hapo shangazi mtu ambaye Doctor kiongozi wa familia ukoo wa msuya anataka huyo mtoto aongeze elimu kiwango cha diploma ndipo anaweza kusimamia hizo mali zote ndio hapo mambo yalipoazia kutimbwirika
 

Kwa biashara za migodi kuwa billionaire ni kitu cha kawaida tu..na wapo mabillionaire wengi tu arusha..inshu ni kwamba hakuanza from the scratch kama wanavyoanza wengine..maelezo yanasema alipewa migodi na mzee wake,mali pamoja na foundation ya hoteli...kwa mtu mwenye akili ni vyepesi sana kufika on top..btw ukishakua na biashara kubwa..ukafala huja automatically kulinda/kujilinda..
 
Ayajakukutaa wewee ya kukuta ndioo utajuaa NDUGU WAKO ama ZAKO.n baba mama YAKO waliokuzaaa
 

Kikubwa ni kwamba anajiskia vbaya mama ake anavyosota jela wakati wana mimali..kwa yeye na kwa sbb yule ni mama yake anaweza fanya vyovyote akavyoambiwa either na yeye mama au na wajomba endapo tu ataona kinafaa ili mama yake atoke alipo..sio akili yake btw..
 
tatizo kubwa naloliona hapo shangazi mtu ambaye Doctor kiongozi wa familia ukoo wa msuya anataka huyo mtoto aongeze elimu kiwango cha diploma ndipo anaweza kusimamia hizo mali zote ndio hapo mambo yalipoazia kutimbwirika
Sikiliza clip. Vizurimjombaa anasema ada zimelipwa kama zilivyoandikwa MTOTO ana mwaka WA.... MDA wakugraduate umepita BASI TUMA matokeo raha ya SHULE usome umalize sio kujulikana UKO NJE

Hapoo ndipoo Shida ilipokuja
Na inabyoonekanaaa kuna NDUGU walitaka kumtumia HUYU MTOTO kama mitajii YAO kupitia adaa..wajomba wamesoma ujinga awataki na kama ujamaliza ama umefeli NJOO bongo upelekwe Uganda ama Nairobi ukapate vyeto

Ukiyakuta kwakoo. NDIO utaelewa mkuuu MTOTO WA mfanyabiashara pale KMR buchaa ALIKUWA Uganda mzee anamtumia tu pesa KILA mwaka miaka mitatu ikapita akatwngeneza docs mzee akaingiaa chakaa MTOTO alifeli amehamia chuo kinginw wee KUJA kushtuka inaumaa kijana adaa zote alizimeza na mademu WA kigandaa.....

So ogopaaa MTU anaekutumia docs degree miaka mitatu UNAJUA MWANAO anagraduate

ALAFU wanne ANATAKA ada watano ANATAKA helaa wasita HELA we unasomea udk ama...kha
 
MZIGOOOO UNAOUMIZA KICHWA HUKO HAPA

WWALE WANAAMINI KIJANA AKIKABIDHIWA MALI AKIUZA MAMAKE ATATOKA HIKO NDICHO KINAWAUMIZA KICHWA PANDE WA PILI

NA NDIO MAANA WALIPATA SHOCK WALIPOELEZWA HATA MKIRUDI MSIMAMIZI ANABAKI KUWA MAMA (MLE)NA MALI ZA MAREHEMU N ZA MKE NA WATOTO PALE WALITOKA NA GOLI MOJA MKONONI AKA HANDCUP
 
Ndugu upande wa dingi ni mbanga chali angu, am talking with experience, nimeshashuhudia mama na wanae wakinyan'ganywa mali hivihivi, nimeshuhudia watoto wakiachwa yatima bila malezi ya shangazi, baba mdogo wala mkubwa wazee walikimbilia maduka ya spear na magari ya abiria vitoto vya watu vikaachwa hapo angali wa kwanza akiwa na 12yrs,walikua wanne,wajomba wakagawana watoto na kuwalea hakuna ndugu wa baba aliewahi ulizia wanaendeleaje, watoto wanakua wakubwa wanapewa tuu hadithi wazazi wao walikua well of, it is over 25yrs now.Ndugu wa dingi hawana hata mia mali zilimfuata wenye mali.Imeisha hiyo
 
dah mkuu hiki kitabu chenye hii picha kilinifanya niijue bible nje ndani enzi hizo niko primary
 
Mkuu wa wilaya na yeye aliza alambe kitu kidogo, hawezi toka mtupu.
 
Daah, mkuu wosia wa aina hiyo ukipelekwa mahakamani unatenguliwa.
Ukiwa napesa nyingi suluhisho nikumuandia mtu mmoja Mali zote kuepusha huu upuuzi. Atakma utakua nawatoto 6 dawa nikumpa mtu mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…