realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Hii ni kwa baadhi ya Shule za Msingi zinazofanya hivyo.
Hii inatisha sana kwa sababu watoto hutia huruma wakati wengine wakiwa nje na mawazo Mengi sana.
Niliwahi kufanya utafiti kidogo wa kuwauliza watoto kuwa wanafikiri ni kwa nini wazazi hawawalipii Chakula? Majibu yao yalikuwa tofauti tofauti.
Wengi wao walieleza kuwa wazazi Hawana kipato cha kutosha.
Wengine walisema wazazi wao wenyewe wakiwa nyumbani wanakula milo yote mitatu lakini wanashindwa kuwalipia pesa kidogo ya Chakula.
Wengine walisema baba zao wanajua ratiba zote za Mechi za mipira lakini hawajui kama watoto hawapati chakula cha mchana Shuleni.
Walieleza kuwa wanajisikia vibaya sana kwa sababu wanashindwa kuelewa hata masomo darasani kwa kuwa na njaa.
Kama Inawezekana basi ule mfumo wa zamani wa kulima mahindi shuleni urudi ili watoto wote wapate chakula Shuleni.
Hii inaumiza sana Serikali tunaomba mlifanyie kazi.
Kama tunaweza kutoa msaada wa mahindi nchi za Jirani basi Tusaidie na watoto wetu.
Wanafunzi wana njaa sana.
PIA SOMA
- Mtoto wako (aliye shule ya kutwa) anapata chakula shuleni? Kwa kiwango gani mzazi/mlezi unahusika katika kufanikisha hilo?