Je, ni sahihi wananchi kuchangia mafuta ambulance au magari ya polisi wanapohitaji huduma?

Je, ni sahihi wananchi kuchangia mafuta ambulance au magari ya polisi wanapohitaji huduma?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Imekuwa kama kasumba sasa. Mwananchi akipata tatizo kwenye mahospital ya wilaya ambazo ziko na hospital za rufaa na kisha kuandikiwa rufaa huwa anaambiwa kuchangia mafuta ili mgonjwa apelekwe.

Polisi nao ukienda kuripoti tukio la uhalifu ili waende eneo la tukio huwa wanahitaji mafuta ya usafiri.

Je, serikali huwa haitengi fungu la mafuta?
 
Mimi Nilifikiri watu wanatakiwa kununua mafuta ya Mwamposa tu, kumbe hata hayo?!
 
Sio sahihi maana unatozwa kodi ili zifanye kazi hizo,but Serikali yako haipelekei fedha za kutosha kwa huko kwa ajili ya kuendeshea Ofisi-wahusika hawana cha kufanya zaidi ya kuwachangisha.
 
Kwann zisitengewe bajeti ya mafuta mbona v8 zina bajeti yake si chini ya lita 2000 kwa mwezi.

Hao police na ambulance wakitengewa lita 2000 hawamalizi
 
Ni sahihi mbona wanachangia mambo mengi? Kwa mfano ujenzi vyoo vya shule madarasa madawati kuchimba mitaro ya maji kujenga vituo vya polisi na afya
 
Ni sahihi kabisaaaaa.
Kama tunachangia kuanzisha ujenzi wa kituo husika sisi wenyewe kisha ndio tunaiita serekali ije kuweka jiwe la msingi, tutashindwaje kuchangia mafuta ya chombo ambacho tulipewa kama zawadi kwa shida zetu wala hatukuomba gari ktk uwekaji wajiwe la msingi.
Polisi wao inategemea na taarifa waliopelekewa. Kawaambie kuna Jambazi au mtu anataka kuuliwa uone kama watakudai mchango wa mafuta, lakini unaenda Polisi taarifa yako ni fumanizi au mifugo shambani, LAZIMA UCHANGIE WESE TU.
Wao wakutafutie bwana shamba, bwana mifugo mtendaji wa kata na kijiji, kisa tu umetiliwa mifugo shambani, Khaaa!!!!!! Acheni basi.
 
Back
Top Bottom