mabutu1835
JF-Expert Member
- Nov 25, 2018
- 909
- 1,425
Naendelea kushuhudia kuongezeka kwa matukio ya baadhi ya familia watoto hasa wengine wakiwa na miaka 17 wakishirikishwa katika kusuluhisha migogoro ya wazazi wao.
Inawezekana hali hii inatokana na kukosekana kwa watu wazima katika familia au viongozi wa dini wakikosa kuaminiwa na baadhi ya familia.
Kwa mtazamo wangu sioni kama ni sahihi watoto kushirikishwa katika kutafuta suluhu ya wazazi wao. Usuluhishi wa migogoro ya wanandoa inahitaji umri, ukomavu wa akili kuhusu maisha, uzoefu wa masuala ya ndoa, nk.
Kila mmoja atoe mtazamo wake na ushauri ikibidi ili tusaidie vijana wasiogope ndoa kutokana na majeraha ya nafsi walizoshuhudia katika vikao vya kutatua migogoro ya ndoa za wazazi wao.