Je, ni sawa kuendelea na uhusiano na mtu ambaye hana muelekeo wa maisha ilhali unampenda?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Wapendwa habari zenu, kuna suala nimelifikiria hapa naomba nipate ku-share na ninyi.

Kuna hii hali unakuta unakuwa kwenye uhusiano na mtu unayempenda kwa dhati, mnaelewana na mnafurahia kuwa pamoja vizuri tu. Lakini kadiri muda unavyokwenda, unaanza kujiuliza kuhusu maisha yenu ya baadaye kwa sababu mwenzako anakua labda haonekani kuwa na mipango inayoeleweka au juhudi za kufikia malengo fulani.

Hapa ndipo changamoto inapoanza. Unampenda na hutaki kumpoteza, lakini pia una ndoto zako, malengo yako na maisha unayotamani kujenga.

Kwa upande mwingine, inawezekana mtu akawa hana mafanikio makubwa kwa sasa lakini ana juhudi, anajitambua na anapambana kubadilisha hali yake.

Sasa je, ni sawa kuendelea na uhusiano kwa sababu ya upendo pekee, hata kama huoni mwelekeo wa maisha yenu ya baadaye? Au ni muhimu kuangalia zaidi ya hisia na kutathmini kama mnaweza kujenga maisha pamoja.

Which is which yani? Nisaidieni mimi jamani nimekwama kiukweli kwenye hili.
 
IMG-20261017-WA0278.jpg
 
Sasa unasema mtu Hana muelekeo wa maisha je wewe pia umemsaidiaje hata kiushauri na kimipango maana Kama unampenda uyo mtu na mnataka kufanikiwa pamoja ni vizuri kushauriana au unamaanisha hata kushaurika hashauriki uyo mtu.
 
hashauriki ndio
 
Wapendwa habari zenu, kuna suala nimelifikiria hapa naomba nipate ku-share na ninyi.

Kuna hii hali unakuta unakuwa kwenye uhusiano na mtu unayempenda kwa dhati, mnaelewana na mnafurahia kuwa pamoja vizuri tu. Lakini kadiri muda unavyokwenda, unaanza kujiuliza kuhusu maisha yenu ya baadaye kwa sababu mwenzako anakua labda haonekani kuwa na mipango inayoeleweka au juhudi za kufikia malengo fulani.

Hapa ndipo changamoto inapoanza. Unampenda na hutaki kumpoteza, lakini pia una ndoto zako, malengo yako na maisha unayotamani kujenga.

Kwa upande mwingine, inawezekana mtu akawa hana mafanikio makubwa kwa sasa lakini ana juhudi, anajitambua na anapambana kubadilisha hali yake.

Sasa je, ni sawa kuendelea na uhusiano kwa sababu ya upendo pekee, hata kama huoni mwelekeo wa maisha yenu ya baadaye? Au ni muhimu kuangalia zaidi ya hisia na kutathmini kama mnaweza kujenga maisha pamoja.

Which is which yani? Nisaidieni mimi jamani nimekwama kiukweli kwenye hili.
Kama huyo ni mwanaume ni tatizo kubwa sana .

Kukosa version ni kuukaribisha umaskini.

Ata kama ni mtu una mpenda
Take a walk.
 
Kama yeye hana malengo, we weka hayo malengo..... mtatumia malengo yako, vivyo hivyo kama hana akili mtatumia zako.

Si umesema unampenda?
 
Back
Top Bottom