Je ni sawa Kuweka nyimbo au mambo ya dini kwenye usafiri wa jamii

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Kuna baadhi magari ya abiria unakuta wanaweka mambo ya dini kwenye redio zao tena kwa sauti kubwa je hii ni sawa maana mule mpo watu dini tofauti pia wengine awana dini pia wengine awaamini kinachoongelewa kwa wakati huo hii naona kama haiko sawa
 
Hasa mwendokasi wanaweka sana hawa matapeli akina Mwamposa na Rashiiiid Gwajima na wenzake. Dini ni uzezeta hasa pambana kumuomba mungu wako na saidia wasiojiweza na wagonjwa.
 
Ukisema kuhusu kuweka nyimbo za dini kwenye usafiri wa umma kuwa sio sawa nahisi hata nyimbo za kidunia nazo sio sawa,,, ukifata kila takwa la mtu binafsi kwenye mambo ya umma basi utakuta kila kitu hakipo sawa.
Hivyo basi kwenye usafiri wa umma piga miziki yoyote yenye maadili haina shida.
 
Kikubwa dereva asiweke mahubiri au mawaidha ya kuuudhi Imani fulani..nyimbo, mahubiri ya kikristo au mawaidha ya kiislam Ni mazuri....Kuna dereva mmoja wa Bus BM Kutoka Arusha dar Tena luxury aliweka mawaidha ya kumponda yesu haikuwa sawa..angetafuta mawaidha mazuri general watu wangebarikiwa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hapo akajiona kapigana jihadi😝😝😝
 
Kuna baadhi magari ya abiria unakuta wanaweka mambo ya dini kwenye redio zao tena kwa sauti kubwa je hii ni sawa maana mule mpo watu dini tofauti pia wengine awana dini pia wengine awaamini kinachoongelewa kwa wakati huo hii naona kama haiko sawa
Huwa waanaamini halitapinduka wala kupata ajari ni muendelezo wa unafiki wa Mwafrika.
 
Hawa ndiyo binadamu,huwezi mlidhisha kila mmoja!, Kama ni muziki wa dini naona ipo vizuri, maana kuna nyimbo nyingine za kidunia ukiwa na mtu mweshimiwa utatamani ushuke hilo dini, hata wasio na dini wakisikiliza ni nzuri zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
^yenye maadili^ 100%
 
BAKI NA IMANI YAKO.
au tafuta earphone uwe unavaa
Hata Mimi mwanzo nilikuwa nachukia kusikia mahubiri na kwaya .lakini nikaja kuwaza dunia bila Mungu itakuwaje hata imani zetu tofauti.
 
Hasa mwendokasi wanaweka sana hawa matapeli akina Mwamposa na Rashiiiid Gwajima na wenzake. Dini ni uzezeta hasa pambana kumuomba mungu wako na saidia wasiojiweza na wagonjwa.
Hauwezi kumjua Mungu bila dini.vinginevyo utaenda abudu mizimu na mawe
 
"mwisho wa uhuru wako, ni mwanzo wa ustarabu wa mwengine"
-Samia suluhu Hassan

Kuna watu hawajui mipaka ya uhuru wao ,Wala hawajui kuzingatia ustarabu wa wengine.
 
Sasa gari bovu alafu unaweka nyimbo za dini kulinusulu si ukichaa huo.
Afadhali ingekuwa hivyo kwamba ajali zote hutokana na magari kuwa mabovu--tungekuwa na relatively few accidents. Achana na takwimu za akili yako mbovu.
 
Mlimfanyaje dereva? Au mlibaki mnagugumia tu? [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…