Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Ninauliza hili swali ili ndugu zangu kama Watanzania tupate kufahamu hawa jamaa wamarekani ambao huiona nchi yao kama paradiso wametuwekea zuio la kutusua kuingia nchini kwao.
Hapa Tanzania kuna ukiukwaji wa haki za binadamu? Na kama upo ni zipi? Kwa mujibu wa Serikali ya US ni kwamba pamekuwa na uminywaji mkubwa wa demokrasia, uhuru wa kuongea au kutoa maoni, na wamezidi kusema kuwa hata haki ya kuishi nayo inakandamizwa sana (maana yake kuna mauji yanafanyika).
Tanzania sio nchi pekee iliyowekewa zuio la kucheza Green Card Lottery, Nigeria imo pamoja na baadhi ya nchi za Africa na Asia.Ila hapa Tz wamekwenda mbali hadi mmoja wa kiongozi ametajwa kuwa anahusika (labda wana ushahidi)
Jana BBC wameonyesha documentary fupi kama ya dakika 15 ikionyesha jinsi vyombo vya dola nchini Nigeria vinavyowatesa watuhumiwa hadi wakati mwingine kusababisha vifo na ulemavu kwa watuhumiwa.
Hayo yanayofanyika Nigeria hata hapa Tanzania yanafanyika watu na hata baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola huyafanya (wakati mwingine kwa kukosa maadili) huenda ikawa sababu ya hawa jamaa kutuweka katika kundi la nchi zilizopigwa ban (zuio). Vitendo hivi vinachafua taswira ya nchi yetu. Nasema hivyo sababu Tanzania ni nchi inayoendeshwa kwa kufuata misingi ya sheria.
Mtu anaiba kuku anapewa kesi ya unyag'anyi wa kutumia siraha.Akitoka humo ndani ana kirema (tortured) na haya mambo yanafanana kabisa na kule Nigeria.
Mimi maoni yangu tunapaswa tujitafakari kama Taifa; justice system yetu iko vipi? Ipo sawa watuhumiwa wanapata haki zao? Watuhumiwa wanateswa mpaka kufa? (Maana kuna minog'ono vijiweni kuwa watu wanapotezwa bila kuwa na hatia)
Tusijikite zaidi katika kuweka hisia zetu kuwa kesi za akina Eric ndio sababu (hizi ni kesi ambazo zipo mahakamani) Ila hatujui kuna wananchi wangapi ambao ndugu zao walipata matatizo wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola (nazungumzia watu wasio na uwezo).
Tanzania sasa hivi ni nchi iliyopiga hatua. Kama waliweza kuipa kampuni tenda (jina kapuni) ifunge mitambo ya kutambua alama za vidole kandarasi ambayo mpaka leo ni kitendawili, kwa nini wasinunue lie detectors! Kama nchi za wenzetu.
Mambo ya kutesa na kupiga watuhumiwa yamepitwa na wakati.