Je, ni ustaarabu ukiwa kwenye Daladala na una simu ya Tsh Milioni 1 na Laki 7 kisha kudai kwa kelele chenji ya Tsh 100 kwa kondakta?

Je, ni ustaarabu ukiwa kwenye Daladala na una simu ya Tsh Milioni 1 na Laki 7 kisha kudai kwa kelele chenji ya Tsh 100 kwa kondakta?

Naomba unielekeze na mimi jinsi ya kuingia jamii forum kwa kutumia simu ya kitochi
 
Wenye akili wanasema
'Take care of the cents and the dollars will take care of themselves'
 
Sasa kama Wewe Abiria Mwenzangu umeshika Simu ya Gharama (ya Kitajiri) ya Tsh 1,700,000/= na Unaidai Chenji yako ya Tsh 100/= kwa Kondakta tena kwa Kelele nyingi Daladalani Mimi GENTAMYCINE Choka Mbaya mwenye Simu yangu hii ya Phillips Kitochi nifanyeje?

Najua kuwa Hela yoyote ni Halali ya Mhusika ila sometimes unaweza Ukadharaulika na Hadhi yako Kushuka kwa Ushamba na Ujuha kama huu.

Na huyu Mwamba niliyekutana nae leo Kimwonekano wake si kwamba ana Dhiki ya Kimaisha kama Mimi GENTAMYCINE bali anaonekana ni Mtu mwenye Maisha yake mazuri ila alikuwa anakomaa kudai Chenji yake ya Tsh 100/= kwa Kondakta ndani ya DalaDala kama vile Beki wa Yanga SC Bakari Nondo Mwamnyeto anavyowakomalia Washambuliaji Hatari ili Wasifunge Magoli.
Nidhamu ya fedha inaanza na financial management katika level ya chini (sana), hata Bil Get haachagi change ya kiasi chochote kile!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom