Je, ni vizuri kumpiga shemeji yako?

Je, ni vizuri kumpiga shemeji yako?

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Nina dada yangu ambaye ameolewa.

Huyu dada yangu na Mme wake kila siku ni matatizo tu.

Maisha Yao yamekuwa kama movie tu.

Mara ana mpiga na kumfukuza nyumbani kwake baada ya miezi kazaa ana Rudi kumchukuwa mke wake
Wazazi ni watu wa Dini unajua kwenye ukristo na sheria Zatu ukimuacha mke Wako Bila talaka uyo bado Mke wako tu.

Licha ya Ivo dada yangu naye ana mpenda huyu Mme wake saana pamoja Na vituko vyote ambavyo anamfanyia lakini akirudi Kuja kumuomba msamaha cha ajabu ana msamehe Na wanarudiana Tena wakienda kukorofishana Tena anajileta nyumbani hata ukimkatalia Mama ana mtetea binti yake.

Jana alikuja nyumbani amelewa alikuja kuongeya na Mke wake dada yangu alikaribishwa nyumbani vizuri Na mke wake wakaanza kuongeya kwa upumbavu wao wakaanza kubebana hapa hapa nyumbani kwetu kwa kukosa adabu huyo Mme wake akaanza kutukana mke wake mbele ya familia na kibaya zaidi akaanza kutukana mpaka familia yangu sisi tulivyotaka kuingilia ili tumfunze adabu uyu bwege, dada yangu akaanza kumtetea Mme wake pamoja na kuona anavyo kosea familia yetu adabu bado akawa mpande wa uyo Mme wake tu.

Je, ni vizuri kumpiga shemeji Yako
Maana Kuna kitu nafikiria hapa
 
No wala usimpige shemeji yako wewe waache warudi makwao kabla ya sherehe za 8 8 lazima dada yenu arudi katobolewa macho.

Kwani sh ngapi? Kateni mawasiliano na dada yenu abaki na mama yake anae mtia ujinga.

Shemeji yenu anatoa wapi kiburi cha kuja kwenu kalewa na kuongea ovyo? Kuna vipesa anawasaidi kama familiya?
 
Ana saidia wapi ndugu kumtunza huyo mke wake tu ni shida
Tatizo Mother
Unajua father hayupo Tena duniani kwa hiyo ukianza kujibizana naye anaona kama vile una mdharau Na kumkosea adabu
Na yeye ndo amemlea dada yetu Ivo hata ukikataa anaanza kujiliza yeye pamoja Na binti yake kwanini tuna wadharau Na kuwatesa ndo maana tumeacha hatuna la kuongeya dada yetu Yuko peke yake mwanamke katika familia
 
Sijui huwa kuna nini katikati ya ndoa za aina hiyo kwani huwa hawaachani kirahisi.

Yaani ndugu mtaongea hadi mtachoka mwenyewe anajionea sawa tu.
 
Umeniwahi na hili swali, kama sio shemeji ndio mtoa huduma basi dada itakuwa ndie mismamia show kupitia kwa mumewe.

Huyo mbwiga sio kupigwa tu, alipaswa kuvunjwa vunjwa kabisa.
Tena mlevi ningemtia vitasa ujinga wake akafanyie kwake huo.
 
Bro sijajua age yako ila ningekushauri waache wenyewe wamalizane.
Yaani mimi ni muumini wa "leave and observe from watchtower"

Tena ingependeza ukawa na life lako mwenyewe na sio kukaa home.
 
Nakaa na Mama ndugu yangu Sasa hivi ni mtu mzima pia ni mjane Baba Alisha tangulia mbele za haki
Pia nina wadogo zangu ambao Wako nyuma yangu ni wanaume wote Na huyo dada yetu ndo mwanamke pekee katika familia Na yeye ndo wakwanza kwenye familia
 
basi fanya busara ujitenge na mzozo wao. Wanawake wakiwa upande mmoja huwezi kuwashinda hoja wala akili.

Mwanamke akitaka lake ni mithili ya teja aliyekuwa na alosto. Wewe baki kuwa mtazamaji tu. Ikiwa nyumba ni ya familia ukiona huyo jamaa kaja wewe ondoka tu ili usione wanayofanya. Na chukua hili kama motisha ya kuhama hapo nyumbani ukae kwako mwenyewe.
 
Nakaa na Mama ndugu yangu Sasa hivi ni mtu mzima pia ni mjane Baba Alisha tangulia mbele za haki
Pia nina wadogo zangu ambao Wako nyuma yangu ni wanaume wote Na huyo dada yetu ndo mwanamke pekee katika familia Na yeye ndo wakwanza kwenye familia
Kwa maelezo haya wewe ndo kiongozi wa familia, bro mkanye huyo shem wako tena mbele ya mama na dadaako tena uoneshe hasira za wazi.
hata kama watalia machozi ya damu ni bora kuliko dharau kwa familia nzima. Yaani usikubali machozi au maneno yao yaondoe heshima hata kidogo mliyonayo.

Kwani usipoonesha reaction yoyote basi jamaa ipo siku atataka kuvaa taulo hapo kwenu na kukutuma dukani ukamletee sigara. Mazoea hujenga tabia.
 
Sijui huwa kuna nini katikati ya ndoa za aina hiyo kwani huwa hawaachani kirahisi.

Yaani ndugu mtaongea hadi mtachoka mwenyewe anajionea sawa tu.
Huyo dada siku akitobolewa macho ndo akili itamkaa sawa. Aachwe kama alivyo
 
Back
Top Bottom