PostGE2025 Je, ni Wasanii wana jukumu la kuikosoa serikali pale inapokosea? Twende kazi

PostGE2025 Je, ni Wasanii wana jukumu la kuikosoa serikali pale inapokosea? Twende kazi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo wote!

1. Kumekuwa na vuguvugu mitandaoni la kuwapiga Pin Wasanii kwa sababu mbalimbali.

2. Nitaeleza sababu halisi bila kuficha kama ifuatavyo;
a) Wasanii kutokemea maovu yanayohusishwa na Dola.
Hii ndio sababu kuu. Ambayo wananchi wanaona Wasanii hawapo upande wao isipokuwa upande wa Dola.

b) Dharau
Hii ni sababu ndogo Sana. Kwani Maneno ya Diamond Platinum ya dharau na kejeli hayawezi kutumika kuhukumu Wasanii wote.
Haki ingekuwa wasanii walioonyesha dharau ndio wapewe adhabu. Ni kweli sio wasanii wote wameonyesha dharau.

3. Baadhi ya Wasanii wamekuwa wakipotosha kuwa Wananchi wanawachagulia Itikadi ya vyama vya siasa. Hapana huo ni uongo. Hakuna mwananchi yeyote anayempangia msanii awe na chama gani au asiwe na chama gani.

4. Wananchi madai yao ni Msanii bila kujali upo chama gani. Au hauna chama kabisa. Wanachotaka ni kuwa upande wa wananchi, kukemea Maovu ndani ya jamii ikiwemo uonevu, dhulma, unyanyasaji unaofanywa na watawala. Hii ndio hoja kuu.

5. Lakini Pamoja na kuwa hoja hiyo ni nzuri na inamashiko. Swali linakuja;

6. Je Wasanii wanajukumu la kuikosoa serikali pale inapokosea?

7. Swali hilo linamajibu kulingana na mambo makuu mawili; HAKI na MAADILI

a) HAKI
Jibu ni Hapana. Msanii Hana jukumu wala wajibu wa kuikosoa serikali pale inapokosea au kutenda uhalifu.
I) Msanii anahaki ya kuchagua aimbe nini, aimbe lini, Aimbe muziki gani, na aimbie hadhira gani.

ii) Msanii anahaki ya kuamua kunyamaza bila kuikosoa serikali. Hayo ni maamuzi take.

iii) Msanii anahaki pia ya kuikosoa kama atataka kwa maamuzi na hiyari yake Bola shinikizo kutoka popote iwe kwa watawala au Kwa wananchi.

iv) Hivyo kwa Upande wa HAKI sio jukumu la msanii kuikosoa serikali pale inapokosea. Ni hiyari na maamuzi yake.
Kuingilia hiyari ya mtu ni kumnyika haki yake.

b) MAADILI.
Kwenye upande wa Maadili, jibu ni Ndio. Msanii anajukumu la kuikosoa serikali pale inapokosea.
i) Msanii nguvu yake kuu ni kipaji na wafuasi wengi.

ii) Kipaji bila Wafuasi hakina maana.
iii) Msanii ni sauti ya Wafuasi wake. Jamii yake. Hivyo kimaadili anajukumu la kusema matatizo yanayowakumba wafuasi wake ambayo ni jamii.

iv) Hii ni kusema wasanii wasioisemea jamii Yao hawana maadili. Hiyo ni Kweli.

v) Lakini Sio Kila Maadili ni HAKI.
Maadili ni subjective wakati mwingine. Kwamba Jambo Fulani linaweza kuwa maadili kwa mtu au jamii Fulani lakini kwa mtu mwingine laweza lisiwe maadili.

8. Swali linakuja, Je Wasanii kwa kukaa kimya waliwasaliti wananchi au wafuasi wao? Jibu hapa ni inategemeana;

a) Msanii anaweza kukaa kimya sio kwa sababu amewasaliti wananchi hapana, kuna sababu nyingi zinazoweza mfanya msanii au mtu yeyote kukaa kimya pindi uovu ukitamalaki ndani ya Jamii au nchi. Sababi hizo;
I) Woga na kuhofia kuhatarisha Usalamaa wake na familia.
Msanii ni mtu kama wewe. Woga unaweza mfanya akae kimya sio kwa sababu amewasaliti watu wake.

ii) Mikataba na makampuni.
Makampuni mengi sio rahisi kuingia ubia na kushirikiana na Wasanii wanaoikosoa serikali.
Kama TaikonMaster nimeshawahi kukutana na wafanyabiashara wa kimataifa wengi wao walisisitiza hawataki kukimbizana na State(Dola) kwa namna yoyote.
Kibiashara ukishaanza kusuguana na vyombo vya Dola tayari biashara ishaingia ruba.
Hivyo wasanii wanaweza kukaa kimya kwa sababu wao wapo kibiashara, kwao muziki ni biashara. Kama wewe na Mimi tunavyofanya shughuli zetu zingine.

3. Shinikizo la Familia.
Msanii anaweza kukaa kimya kwa sababu watu wake wakaribu. Baba, mama, make/mume au watoto wanamshinikiza akae kimya na aachane na kuichokoa serikali.
Fikiria mimi TaikonMaster ambaye sio mashuhuri na siandikii makala radical yaani sina ukosoaji ule mkali kwa serikali lakini mara kadhaa nakumbushwa na watu wangu wa karibu niachane na kuandika mambo ya serikali.
Vipi kuhusu msanii mwenye followers wengi? Akikosoa serikali lazima apate hofu kwani yeye anawafuasi na serikali itapata damage kutoka kwa watu.

Sababu zinazopelekea humu JF watu watumie Fake ID(wajifiche) na wanaharakati wakimbie nje ya nchi ndio hizohizo zinazowafanya wasanii wa muziki wa ndani wakae kimya.

9. Je tuwalaumu? Hapana.

10. Isipokuwa serikali na vyombo vya usalama wanajukumu la kuangalia mambo haya katika hatua za kuongeza utawala bora wa Sheria.

11. Wananchi hakuna sababu ya kuwa na chuki na wasanii ingawaje mnayo HAKI ya Kuamua Wasanii wakuwa follow au kutokuwa follow.
Mnayo Haki ya kuamua kusikiliza au kutokusikiliza kazi ya wasabi.
Mnayo Haki ya kuwaungisha kwenye biashara zao au kutowaungisha. Hizo ni haki zenu pekezenu (in habil khabil voice)😆

Acha nipumzike sass

Ijumaa kareem. Nawatakia maandalizi mema ya Sabato

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom