Je, ni wazo zuri kubadili gari kutoka Toyota Vanguard 2011 kwenda Nissan Extrail Third Generation ya 2016?

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Wakuu naomba kufahamu wataalamu wa magari, je ni wazo jema mtu kutaka kuuza Vanguard ya mwaka 2011 na kutaka kununua Nissan Extrail ya mwaka 2016.

Naomba uzoefu na ujuzi wenu wakuu.

Gari zote hizi hapa chini.

1685803799751.png

1685803859320.png
 
Hoja sio kampuni ya Nissan Ila ni aina ya hiyo Nissan
 
Mkuu usitoke kwenye Toyota kaa humo. Kibongobongo Toyota Ina mafundi wengi wanaojua madhaifu yake. Nissan wengi wataanza kujifunza kutengeneza hiyo ya kwako.
ikiwa mfuko unaruhusu na ukawa tayari kulipia gharama kubwa kwa service ya kawaida unaweza kukaa kwenye Nissan.
Binafsi nimepitia changamoto kadhaa za spea na ufundi nilipomiliki gari tofauti na Toyota . Kwa sasa
Nitatoka kwenye Toyota siku Tanzania ikiwa dona kantri.
 
Ingejenga hoja kwamba spea za Toyota zinapatika kirahisi ungeeleweka...

Toyota ya mwaka 2011 zinawapasua kichwa mafundi kanjanja...

Teknolojia ya hiyo toyota ya 2011 na hiyo Nissan ya 2016 hazijaachana kivile...

Hizo ni gari za kutumia diagnosis kabla ya kupiga nyundo...
 
Back
Top Bottom