Je, ni wazo zuri kubadili gari kutoka Toyota Vanguard 2011 kwenda Nissan Extrail Third Generation ya 2016?

Je, ni wazo zuri kubadili gari kutoka Toyota Vanguard 2011 kwenda Nissan Extrail Third Generation ya 2016?

Mkuu usitoke kwenye Toyota kaa humo. Kibongobongo Toyota Ina mafundi wengi wanaojua madhaifu yake. Nissan wengi wataanza kujifunza kutengeneza hiyo ya kwako.
ikiwa mfuko unaruhusu na ukawa tayari kulipia gharama kubwa kwa service ya kawaida unaweza kukaa kwenye Nissan.
Binafsi nimepitia changamoto kadhaa za spea na ufundi nilipomiliki gari tofauti na Toyota . Kwa sasa
Nitatoka kwenye Toyota siku Tanzania ikiwa dona kantri.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Vuta chombo ambacho kitaikosha roho yako.
Kimsingi unatakiwa uwe na gari ambayo ukiipaki sehemu lazima ugeuze shingo kuicheki tena huku ukitabasamu.

Kama ni tofauti na hivyo ujue hiyo gari haijaukosha moyo wako na upo nayo si kwa sababu unaipenda bali kwa sababu ya kufuata mkumbo au ndipo mfuko wako ulipoishia.
 
mkuu tatizo ni mfuko, we unadhani watu wanapenda vits,starlet na funcargo??
 
CIF USD 10,000-12,000, Kodi 14M (unless hujui kucheki tra calculator) Total around 40m,

Vanguard inazunguka mitaa hiyo hiyo

Yes, ina bei nzuri sana ukilinganisha na bei za Toyota kwa za miaka hiyo
 
Back
Top Bottom