Sayansi imeshindwa jambo moja la msingi sana ambalo ni
1. KUHAISHA.
Sayansi imeshindwa kutengeneza Uhai, iwe wa mnyama au mmea.
Hii inaonesha Mwanadamu sio zao la Sayansi.
Hii inaonesha Sayansi sio msingi wa maisha ya viumbe, na maisha kwa ujumla wake.
Hii inaonesha Sayansi sio taaluma ya kuitegemea sana katika maisha.
2. Sayansi imeshindwa kuhudumia viumbe kwa asilimia mia moja.
Yaani Sayansi imeshindwa kutibu baadhi ya magonjwa yanayomkabili binadamu na viumbe vingine.
Yaani Sayansi imeshindwa kufufua viumbe vilivyokufa ili kuvirejesha katika hali ya uzima ya mwanzo.
Yaani Sayansi imeshindwa kuzuia baadhi ya majanga yanayosababishwa na nguvu za asili kama Matetemeko ya Ardhi, Vimbunga vya El-Niño, mvua za Gharika nk.
Sayansi imeshindwa kutoa majibu kuhusu masuala ya mahusiano ya Sayari kubwa, mfano.
Haisemi Jua likiharibika litarekebishwaje.
Haisemi msingi wa Sayari kuelea bila kushikiliwa na mihimili au nguzo zenye nguvu. Inasingizia kuwa nguvu za Gravity ndizo zinazoshikilia Sayari lakini haisemi hiyo Gravity imeegemea kwenye kitu gani kinachoipa nguvu ya kushikiria hizo Sayari zote.
Sayansi imeshindwa kueleza kwa ufasaha nini Chanzo na Hatima ya Uhai.
Sayansi ilichofanikiwa ni kubuni nyenzo za kufanyia kazi, kwa kiwango cha kawaida maana kazi bado inaendelea ya kubuni nyenzo za kumuwezesha binadamu kufanya kazi zake kwa urahisi zaidi bila kuvitegemea sana viungo vyake.
Sayansi ilichofanikiwa kiasi ni kurekebisha hizo nyenzo za kifanyia kazi na kutibu baadhi ya maradhi yanayomsumbua Binadamu na viumbe vingine.
Sayansi imeshindwa kujibu maswali ya msingi sana katika maisha.
Nani aliyeasisi Uhai ?
Nani alimtengeneza Binadamu ?
Binadamu yupo kwa ajiri gani ?
Ulimwengu anaoishi Binadamu umetengenezwa na nani ?
Unaisha lini ? (expire date yake)
Nini hatima ya maisha ?
Hapa bila shaka kuna hoja ya msingi sana ya kudadisi maisha zaidi ya majibu ya Wanasansi.
Sent using
Jamii Forums mobile app