Wazazi sasa hivi wamekwa 'mateja' wa karatasi za nailoni zenye spongi kwa ndani maarufu kwa jina la pampasi kuwavalisha watoto wao badala ya kutumia vile vitaulo vyembamba vinavyojulikana kama nepi. Pampars ndiyo brand ya kwanza kuingiza bidhaa hizi zilizochukua nafasi ya matumizi ya nepi tulizozizoea, ingawa sasa hivi ziko kampuni nyingine zenye bidhaa kama hizi lakini watu huwa wanaziita zote pampasi hata kama brand yao sio Pampars, sawa na ilivyo kwa bidhaa za Shell, Kiwi, PANADOL, Mobil.
Madhumuni ya wazazi na walezi kuzipenda bidhaa hizi ni ule uwezo wake wa kuzuia mikojo na kinyesi toka kwa mtoto kisisambae nje na kuchafua sehemu nyingine za mazingira yanayomzunguuka mtoto. Hivyo mtoto ana uwezo wa kukaa na mkojo na kinyezi chake kwenye "pampasi" kwa muda mrefu sana usiku, safarini, au wakati walezi wanafanya kazi nyingine.
Pamoja na uzuri wa bidhaa hizi kwa walezi lakini zinasababisha kasoro kubwa na mbaya za kiafya kwa watoto. Ndani ya kinyesi wako bacteria na fungus wengi ambao wanasababisha ugongwa wa UTI and fangasi kwenye mfumo wa mkojo unayojumuisha kibofu cha mkojo na mafigo. Mtoto mwenye UTI anakuwa anahangaika ama kulia sana wakati wa kukojoa, anakojoa mkojo "mchafu" wenye vitu kama usaha na utando fulani (turbid), harufu na kupata homa kali isiyotibika kwa dawa za malaria. UTI isipotibiwa vizuri na haraka inasababisha uharibifu mkubwa wa figo za mtoto na mtoto kuonyesha dalili za kuvimba miguu na hatimaye mwili mzima kisha kifo.
KInachofanyika pale ni kwamba kinyesi na mikojo inapokuwepo pamoja kwenye pampasi kwa muda mrefu vinatawanyika hadi kugusa njia ya mkojo na kuwafanya bacteria walioko kwenye kinyesi (enterobacteria) wapate muda wa kutosha kuweza kupandisha juu kwenye kibofu na mafigo kupitia tundu la kukojolea na mirija inayosafirisha mkojo. Tofauti na nepi za kawaida ambazo kwa vyovyote vile mtoto huwa hakai na kinyesi chake kwa muda mrefu hivyo kupunguza muda wa bacteria kuweza kujisogeza hadi kwenye kibofu bila kufagiliwa (flushed) na mkojo mwingine wa mtoto.
Tatizo la UTI ni kubwa sana kwa watoto wenye jinsia ya kike kuliko jinsia ya kiume kutokana na maumbile ya jinsia ya kike kuweza kuruhu kinyezi kingi kibaki ukeni na kwa muda mrefu pamoja na umbali ufupi sana wa njia ya kufika kwenye kibofu ukilinganisha na mwanaume. Lile "bomba" la mwanaume huwa linairefusha safari ya bacteria kukifikia kibofu cha mtoto wa kiume. Mtoto wa kiume aliyetahiriwa mapema ana uwezekano mkubwa pia wa kujikinga na maambukizi ya UTI kuliko wenzao ambao hawajatahiriwa.
Wazazi pampasi ni janga sio ufahari, mkojo na kinyesi HUWA vina tindikali (acid) ambayo ikigusana na ngozi ya mtoto inasababisha kuunguza ngozi ya matako, mapaja na sehemu za siri za mtoto na kuonekana zimechubuka na kuwa nyekundu, hivyo kusababisha watoto wengi wapate mapele, majipu na fangasi kwenye ngozi mara kwa mara NA KUWAFANYA WAZAZI WANAPOZE HELA Na muda wao mwingi kununua pampasi, kununua matibabu ya watoto wao na kutumia muda mwingi wa kufanya vitu vingine kupeleka watoto dawani. Kama huwezi kuachana kabisa na matumizi ya pampasi basi Hakikisha kuwa unaibadilisha kila mara, yaani mara 3 kwa usiku kucha na mara 5 kwa mchana kutwa.