Je, NIDA ni haki yako? Je, kwanini huruhusiwi kupata taarifa za NIDA yako ukienda kuomba?

Je, NIDA ni haki yako? Je, kwanini huruhusiwi kupata taarifa za NIDA yako ukienda kuomba?

Termux

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
433
Reaction score
1,067
1776318810509.png


Ndiyo, NIDA ni haki yako kama raia, kwa sababu taarifa za utambulisho wa taifa ni sehemu ya haki zako za msingi za kutambuliwa kisheria na kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi kupitia NIDA. Kupitia NIDA unaweza kupata Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN), kufungua akaunti ya benki, kupata huduma za serikali, na kutambulika rasmi kama raia.

Lakini kuhusu swali la “kwanini huruhusiwi kupata taarifa za NIDA yako?”, sababu kuu ni: Kulingana na Majarada niliopitia na kuyasoma, Ila sio kwa asilimia mia -

  1. Kulinda usalama wa taarifa binafsi
    Taarifa za NIDA zina taarifa nyeti kama majina, tarehe ya kuzaliwa, alama za vidole, na taarifa za familia. Serikali huweka masharti ili kuzuia wizi wa utambulisho au matumizi mabaya ya taarifa hizo.
  2. Uthibitisho wa umiliki wa taarifa
    Huruhusiwi kuona au kubadilisha taarifa bila uthibitisho wa kuwa wewe ndiye mhusika halali. Ndiyo maana NIDA huomba uthibitisho kabla ya kutoa taarifa au kufanya marekebisho.
  3. Baadhi ya taarifa zinapatikana kwa njia rasmi tu
    Unaweza kupata NIN au kufuatilia maombi yako kupitia huduma rasmi za mtandao za NIDA, lakini taarifa za kina zaidi zinahitaji kufika ofisini kwa sababu za kiusalama.

Kwa hiyo, si kwamba hunyimwi haki yako, bali taarifa zako zinalindwa kwa usalama wako.

#Kwa mimi Binafsi nilikuwa najua kuwa unaweza kupata details zako za NIDA kama unavoenda bank kuomba Bank Statement kama mmiliki halali wa account yako. Nmekutana na iyo changamoto.

Wadau wa Jamii Forum na wenye uwelewa wa hili jambo msaada kidogo ili tuelimishane.
 
Nchi ya kijinga, everything is flawed!
Nashindwa kuelewa, kwanini upewi taarifa zako ukiomba, wakati umeenda muhusika kuomba taarifa zako. Sijui tunakosea wapi?, Ingekuwa kaenda kuomba mtu mwengine sawa ila nmeenda mimi mwenyewe mwenye Nida yangu na sipewi.
 
Nchi ya kijinga, everything is flawed!
Na Hapo hapo NIDA ID Ikisha Expired Unapewa tena Form ya kujaza wakati Details zako zote wanazo, Hadi finger print,
Nashindwa kuelewa kwanini National ID ya Taifa inakuwa expire, Kwaiyo uraia wako unakuwa na mda, ukiisha unaenda tena kuomba mara nyingine.
 
Mimi ni raia wa tanzania, babu na bibi zangu wa pende zote ni raia wa kuzaliwa pia lakini kupata kitambulisho cha NIDA ni kasheshe na nilishakata tamaa kufuatilia. ni maombi yangu kuwa Serikali ilete huduma mtaani tena watu tujiandikishe.
 
Mimi ni raia wa tanzania, babu na bibi zangu wa pende zote ni raia wa kuzaliwa pia lakini kupata kitambulisho cha NIDA ni kasheshe na nilishakata tamaa kufuatilia. ni maombi yangu kuwa Serikali ilete huduma mtaani tena watu tujiandikishe.
 
Nilienda kujiandikisha nikaombwa f80 ya kuchukua cheti cha kuzaliwa nikasema naleta mda sio mrefu nikatoka nikaenda kunywa kongagi sijawahi rudi tena
So kwako kunywa bia ndio msingi sio kupambania haki yko!!
 
Na Hapo hapo NIDA ID Ikisha Expired Unapewa tena Form ya kujaza wakati Details zako zote wanazo, Hadi finger print,
Nashindwa kuelewa kwanini National ID ya Taifa inakuwa expire, Kwaiyo uraia wako unakuwa na mda, ukiisha unaenda tena kuomba mara nyingine.
Nchi hii isipokarabatiwa na uprising, tutaumia sana
 
Ukienda tena kuomba passport utashangaa unaambiwa ulete tena makabrasha kama hayo ya NIDA.
 
So kwako kunywa bia ndio msingi sio kupambania haki yko!!
haki yangu ndio kuchukua nida ndugu yangu. Haki unaijua kweli? Bila hiyo nida nakula nakunywa natunza familia yangu. Ukiniambia kwa umri huu wa 36yrs eti haki ni kupambania nida ntakuma hamnazo. 80k kwa maisha haya niitoe kwa makaratasi tu. 80k ili iishe vizuri wife apate 30k watoto watatu 15k@, 5k nilipe luku, 20k nijilipue na konyagi zangu,10k jikon kunawiri maisha yasonge. Lakin kunambia niende kwa mwenye kiti barua ya utambulisho 5k, usafiri hadi nipate utakula 10k, passport size photos 3k, 80k ya birth certificate, 6k ya avidav cjui, mara photocopy plus time wasted = more than 150k kisa makaratas na kakadi kanakofutika mda wowote tena urudi huko na 50k. Nefa efa waniletee wao kama ni muhimu
 
Back
Top Bottom