Kwamba kila kitu lazima kifanyie kwa back up ya CCM? Kitu gani cha ajabu alichokifanya ambacho unaona haistahili kifanywe na yeye.
Alichonacho ni nyota tu ya kukubalika, na kaitafuta mwenyewe especially kwa wambea, wanawake wanaojipodoa, mabinti wadogo wenye kutamani mafanikio.
Ushawishi wake ametumia gharama kuupata, sometimes kukosana na serikali anaenda kichwakichwa mara akusanye rambirambi Waziri Mkuu ampinge hadharani na kumfanya apate kiki, mara amuige Rais na kupost mtandaoni kisha kupewa kesi ya uhaini.
Niffer nimesoma nae tuition niliburuzwa na cousins nikasomee center yao, alikuwa Form 1 nipo Form 2. Nachokumbuka alikuwa anaongea sana tuition nzima, sikuwa nampenda alikuwa anakuja kumfuata cousin wangu, kasoma nae na alikuwa rafiki yake kishuleshule (sahivi sio cycle yake).
Baadae sasa niko kama first year cousin yuko Diploma akaanza kunipa story za Niffer anauza chakula sijui juice mtaa gani, baadae kafungua duka la nguo, baadae Niffer anaenda wapi na wapi. Nikawa napuuzia hizo habari nasema sasa huyo si mjasiriamali kama wengine. Mimi huyo namkumbuka "demu" mwenye kuongea sana ambaye sikuwa napenda uwepo wake.
Ilinitokea baadae naperuzi Instagram ndio nikamuona kwenye feed yangu, nikashangaa mbona ana likes nyingi huyu mpiga kelele wa zamani. Kutazama followers anao wengi laki kadhaa.
Baadae girlfriend wangu akanituma nimnunulie mafuta gani nadhani yalikuwa Bio Oil yale kuna series alikuwa anayaleta, akanipa order number alikuwa ni mtu wa 600+ kasubirishwa.
Ndio nikajua kweli huyu Niffer ana kundi lake kubwa analoshawishi. Rejea sakata la Kojic, ugomvi na waagizaji wa China hasa alipogusa brenda, ugomvi na wauza vipodozi wanapeana shutuma hiki ni feki hiki ni original.
So, at least sioni kama aliibuka from nowhere.