Mambo ya Mapenzi ni mambo ya Moyo,It has to be your heart speaking to his heart.Sikiliza moyo wako,heshimu hisia zako lakini hakikisha una uhakika na hisia zako.Kwa sababu kama utakuwa umemtamani ni dhahiri kuwa jinamizi la rafiki yako litakutesa sana kwenye maisha yako.
Mapenzi yako kwake unayajua wewe,sisi huku hata kama tutashauri hatuwezi kuondoa ukweli kama unampenda au laa'Nadhani unaufahamu usemi wa LOVE IS BLIND.Kama kweli unampenda haya mambo mengine yatakuwa ni changamoto ndogo sana.
Jamii always huwa ina comment katika kila jambo,liwe zuri au baya.Sio watui wote katika jamii watakaofurahishwa na kitu chochote unachofanya.Usitafute sana kumfurahisha kila mtu.Angalia moyo wako,hisia zako,hisia za mwenzako na maisha yako ya baadaye.Je,do you see him besides you milele yote? Isijekua umemtamani tu kwa vile alikua anakuita mke mdogo.Kwa sababu kama ulikua unampenda lazima ungekuwa na wivu nae tangu rafiki yako yuko hai.Cha msingi wewe ndo mwamuzi mkuu katika hili