Soma vzr nilichandika acha ubishi usio na maana yoyote. Hiyo kadi nimetumia tu kama mfano. Iwe hudum iwe nini lakini maelezo ya benki ndiyo sahihi na ya kuaminika kuliko haya hapa kwa kiasi kikubwa kabisa. Namna ya kuwa-contact ni yeye mwenyewe aamue. Kama ana nafasi why not visit a branch physically? Na pia nimetoa option ya electronic. Jitahidi uache ubishi kwa jambo lililo wazi. Taratibu zinabadilika kila siku. Wewe unaweza kumshauri kulingana na uzoefu wako wa mwaka jana na hata mwezi wa kwanza mwaka huu, kumbe leo hii taratibu zimeshabadilika!
Mimi na wewe nani mwenye ubishi usio na maana?!
Narudia swali langu la awali kabisa... Bank iliyo Bahama watafahamu vipi how banks operate in another country?!
Na hapa napenda kusisitiza... Standard Chartered Tanzania ni subsidiary Bank inayo-operate under Tanzanian Banking Regulations, na ile ya Bahama kama na yenyewe ni subsidiary itakuwa ina-operate kwa regulations za Bahama!
Tofautisha kati ya subsidiary bank na foreign branch!
Kuna uwezekano mkubwa hata banking sofwares wanazotumia zikawa tofauti! Kuna uwezekano mkubwa sana tena sana mtu akiwa kwenye system za Standard Chartered Bank Tanzania hawezi ku-access account ya Standard Chartered Bank Bahama!
Na nina uhakika kwa 99% hata akienda branch ataambiwa tu kwamba ataweza ku-WDL kwa kutumia Card yake or else, anaweza ku-request wire transfer kutoka Bahama to TZ, ingawaje hivi sasa kuna njia nyingine very cheap inaitwa transferwise lakini siwezi kumshauri!!
Kwa maana nyingine, ni mtu au watu wenye uelewa na transactions za Tanzania ndio wanaoweza kumpa jibu sahihi! Akienda kuwauliza Standard Chartered Bank Bahama wanaweza hata wasijue Standard Chartered Bank Tanzania wana-issue accounts zipi, cards zipi, Cash WDL restrictions zipo vp n.k!
Kwa mfano, hata cash WDL limit per transaction kwa kutumia MasterCard kwenye non-hosting country inatofautiana kati ya nchi na nchi! Sasa unadhani hata kwa jambo dogo la kufahamu maximum cash limit pale Bahama watafahamu?!!
Na kwamba taratibu zinabadilika kila siku ni kweli lakini mabadiliko ya Standard Chartered Bank Bahama hayawezi kuwa ya Tanzania!! Hii maana yake nini?!
Unaweza kukuta wakati Bahama bado unaweza kutumia MasterCard lakini sheria mpya za BoT zikasema MasterCard na VISA Card zina-facilitate online transactions kwa urahisi na hivyo zinaweza kurahisisha money laundering na kwahiyo from now, Bank zinatakiwa kutumia normal ATM Cards, na yeyote anayetaka kufanya WDL au Deposit from or to a foreign country atumie traditional money transfer methods kamavile TT!
Hilo linawezekana lakini likifanyika Tanzania katu Bahama hawatafahamu, na matokeo yake wanaweza kumwmbia "YES, ukiwa Tanzania unaweza kutumia MasterCard" wakati kumbe Tz zimeshapigwa ban!