Bado ume-twist tena. Hapo juu ulisema suala siyo card. Hapa unasema suala ni kadi. Unasimamia wapi ndugu yangu? Mimi nimesema maelezo yoyote atakayoyapata hapa juu ya huduma hayatakuwa sahihi kama angewasiliana na benki yenyewe. Upo hapo?
Ni mgumu wa kuelewa, au tatizo lako ni nini hasa?! Ni kwamba huelewi au unataka ligi isiyo na maana au unapenda ubishi ambao kabla ulisema napenda ubishi usio na maana huku ukionesha wazi wewe ndo unapenda ubishi usio na faida!!
Kisha unadai nime-twist wakati tangia mwanzo nimesema wazi kabisa kwamba anaweza kufanya transaction bila kujali benk ipi kwa kutumia kadi!!
Kwa mfano hapa chini, nimetaja akitumia mashine za CRDB kuonesha anaweza kufanya WDL kwa kutumia mashine ya benki yoyote ile provided iwe inapokea VISA/MasterCard!!
Hata "deposit" na yenyewe ndo hivyo hivyo... anaweza kutumia benki yoyote ile kwa sababu kinachofanyika sio direct deposit bali ni wire transfer!!
Post yangu ya kwanza kabisa ni hii:
Huduma zipi kwa mfano unazotaka uwe unapata tu kutoka Standard Chartered Tanzania?!
Kama ni deposit, utafanya "deposit" lakini sio moja kwa moja bali through wire transfer au njia nyingine yoyote... kitu ambacho unaweza pia kufanya kupitia benki yoyote ile!!
Kama ni ku-WDL, itakuwa ni sawa na hapo juu, in additional to MasterCard and/or Visa Card!
Kama kuna privilege yoyote labda privilege ya correspondence bank in case Standard Chartered Bahamas ndio correspondence bank ya Standard Chartered Bank Tanzania.
By correspondence bank I mean, benki inayotumika ku-facilitate transaction kati ya benki mbili ambazo kwa kawaida zinakuwa kwenye mataifa tofauti.
But wait... The Bahamas?! I hope sio offshore bank account.
Baada ya post ya kwanza, post yangu ya pili nikamweleza uwezekano wa yeye kutumiwa kadi hata akiwa Bongo huku nikitangulia kumweleza ni mambo yapi anaweza kufanya kabla hajasafiri:-
Bila kujali upo Bahama au wapi, kabla hujatoka unatoka ughaibuni unatakiwa kufanya yafuatayo:-
1. Kama card yako inakaribia ku-expire, nenda branch waambie wa-extend muda au kukupa kadi nyingine, and they will do it.
2. Kabla hujatoka ughaibuni hakikisha una-update contact info zako za Bongo! In case card uliyopewa ime-expire au kupotea, utawa-contact nao watakutumia kadi nyingine! Hawatakutumia kupitia tawi la Standard Chartered la Bongo bali watakutumia kwa njia ya kawaida, kv through DHL!
3. Kaa ukifahamu Universal Transactions kwa kutumia Card ni very expensive kwa amount kuanzia $1000, na ni very cheap ukitumia wire transfer!
Ukitumia ATM Machines za CRDB kwa mfano, kwa kila transaction isiyozidi TZS 400K wanachukua pesa ya nyama, mchele, sukari, vitunguu na vikorokoro vingine kibao ya kukuwezesha kuandaa pilau nyama just for a single transaction!
Now assume unataka kuchukua TZS 5M!
Hapo #3 maana yangu ni kwamba, kama akaunti ina mpunga wa kutosha na hutarajii kurudi ughaibuni, piga wire transfer pesa yako yote to a local bank account na huko account ya ughaibuni acha dola mia chache tu!
Kwa bahati mbaya akawa hajaelewa issue ya wire transfer, ndipo nikaandika post ya tatu na kumfafanulia:-
Namaanisha unahamisha pesa kutoka Bahama kwenda akaunti ya Kibongo, na njia itakayotumika uwezekano mkubwa ni Wire Transfer ambayo kwa kawaida ina-range from USD 25 (+10 +X ) to USD 30(+10 +X).
Hiyo USD 25 au USD 30 ndo transfer charge, USD 10 inaenda kwa Correspondence Bank, na hiyo USD X ambayo inakuwa kati ya USD 5-10 inachukuliwa na Local Bank unakoingiza hiyo pesa!
Kwa maana nyingine, kama Bahama una USD 10K, Bongo itaingia takribani USD 9950. Kama Bongo unayo forex account, itaingia kama ilivyo lakini kama una local currency account, hizo USD 9950 zitakuwa converted into TZS na kuingizwa kwenye akaunti.
Sasa hadi hapo ni kipi nilicho-twist?!
Lakini cha ajabu kabisa, wewe ile unaanza kuchangia tu, ukaanza na ligi zisizo na maana yoyote ile:-
Mbona unaongea kinyume? Ushauri na maelezo ya benki ndiyo bora zaidi kuliko hapa. Benki hawawezi kukudanganya hasa benki kubwa kama hiyo lakini hapa unaweza kupewa majibu yasiyo sawa. Napata shaka kama kweli umewahi kusafiri halafu info kama hizi hujui pa kuzipata. Anyway wasalimie huko Lukuledi ambako wewe unasema ni nje ya nchi.
Ukaona jamaa anajisingizia yupo nje kumbe sio! All in all, awe nje au asiwe nje, was it necessary?
Kutokana na maelezo yako, ndipo nikakuuliza:-
Hivi unatarajia Standard Chartered Bank Bahama wanaweza kufahamu banking procedures za Bongo?! Kumbuka hizi sio foreign branches bali ni subsidiary ban ambayo kila moja ina-operate kulingana na regulation za nchi husika!!!
The same issue bado nimekuwa nikisisitiza hata posts za karibuni!
Again, nime-twist nini hapo?!
Baada ya kujibu nilichokuuliza, ukadai:-
Mbona unapenda sana ku-complicate mambo ndugu yangu. Kama kweli yuko huko aende hiyo benki watampa maelezo ya kutosha kulingana na kadi aliyonayo. Unafikiria kwa mfano hawawezi kujua kuwa mteja wao akipoteza kadi akiwa nje ya nchi yao anatakiwa afanye nini ili kupata mpya? Ok... tufanye hawawezi kujua procedures za Bongo kama ulivyosema, je mawasiliano hayawezekani? Hata kama benki haitaki kuwaulizia, je yeye hawezi kuulizia kwenye karne hii yenye kila aina ya mawasiliano? Kwa mfano akiandikia banki husika email kuulizia na kuulizia hapa ni wapi atapata jibu sahihi zaidi?
Yaani mie niliyetoa jibu la nini anaweza kufanya unadai na-complicate lakini sio wewe unayetaka aende bank physically!!
Again, kipi nime-twist?! Wapi nimebadilisha maelezo yangu?!