Je, nikifungua akaunti Benki ya Standard nchini Bahamas, naweza kupata huduma kama mteja wa Benki hiyo nikiwa Tanzania?

Kote ni sahihi maana hapa wapo watu walio wai kuzipoteza hizo card wanauzoefu na hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa kifupi unaweza kutoa pesa ila hutaweza kuweka ukiwa nje ya hiyo nchi pia kwa Tanzania hawawezi ku access akaunti yako hadi nchi uliyofungulia account,tatizo hilo niliwahi kulipata nikiwa south África


Sent using IPhone X
 
Mleta mada hakuuliza masuala ya kadi, hayo mambo ya kadi tumeyaleta wachangiaji!! Yeye alizungumzia huduma za kibenki kwa ujumla wake!!

Na ukimsoma vizuri mleta mada anaonesha wazi kwamba hili suala halifahamu vizuri na ndio maana akahisi kuwa na akaunti Standard Chartered Bahama kunaweza kusaidia kupata huduma za kibenki TZ kwavile na kwenyewe kuna Standard Chartered.

Na katika hilo wala siwezi kumshangaa, mtu yeyote asiye na uzoefu anaweza kuhisi hivyo hivyo... kwamba hii ni Stanchart, na ile ni Stanchart sasa kwanini kusiwe na uwezekano wa kupata huduma as if yupo kwenye domicile branch!!

But all in all, ikiwa hata akienda huko benki kuna uwezekano, kwa kiasi kikubwa akaambiwa haya haya aliyoambiwa hapa; sasa kuna sababu gani ya kwenda benki physically?!

Ningekuelewa endapo ungesema awa-contact customer care virtually, lakini seriously mtu aende benk physically kuuliza maswali kama haya?!
 
Ukweli usio fichika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma vzr nilichandika acha ubishi usio na maana yoyote. Hiyo kadi nimetumia tu kama mfano. Iwe hudum iwe nini lakini maelezo ya benki ndiyo sahihi na ya kuaminika kuliko haya hapa kwa kiasi kikubwa kabisa. Namna ya kuwa-contact ni yeye mwenyewe aamue. Kama ana nafasi why not visit a branch physically? Na pia nimetoa option ya electronic. Jitahidi uache ubishi kwa jambo lililo wazi. Taratibu zinabadilika kila siku. Wewe unaweza kumshauri kulingana na uzoefu wako wa mwaka jana na hata mwezi wa kwanza mwaka huu, kumbe leo hii taratibu zimeshabadilika!
 
Forex or Local Tsh Acc.

What do you advice?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania kuna Standard Bank?

au unamaanisha Stanbic ama Standard Chartered?

nadhani inawezekana kwa Benki za kimataifa
Waulize hapo Bahamas
 
Mimi na wewe nani mwenye ubishi usio na maana?!

Narudia swali langu la awali kabisa... Bank iliyo Bahama watafahamu vipi how banks operate in another country?!

Na hapa napenda kusisitiza... Standard Chartered Tanzania ni subsidiary Bank inayo-operate under Tanzanian Banking Regulations, na ile ya Bahama kama na yenyewe ni subsidiary itakuwa ina-operate kwa regulations za Bahama!

Tofautisha kati ya subsidiary bank na foreign branch!

Kuna uwezekano mkubwa hata banking sofwares wanazotumia zikawa tofauti! Kuna uwezekano mkubwa sana tena sana mtu akiwa kwenye system za Standard Chartered Bank Tanzania hawezi ku-access account ya Standard Chartered Bank Bahama!

Na nina uhakika kwa 99% hata akienda branch ataambiwa tu kwamba ataweza ku-WDL kwa kutumia Card yake or else, anaweza ku-request wire transfer kutoka Bahama to TZ, ingawaje hivi sasa kuna njia nyingine very cheap inaitwa transferwise lakini siwezi kumshauri!!

Kwa maana nyingine, ni mtu au watu wenye uelewa na transactions za Tanzania ndio wanaoweza kumpa jibu sahihi! Akienda kuwauliza Standard Chartered Bank Bahama wanaweza hata wasijue Standard Chartered Bank Tanzania wana-issue accounts zipi, cards zipi, Cash WDL restrictions zipo vp n.k!

Kwa mfano, hata cash WDL limit per transaction kwa kutumia MasterCard kwenye non-hosting country inatofautiana kati ya nchi na nchi! Sasa unadhani hata kwa jambo dogo la kufahamu maximum cash limit pale Bahama watafahamu?!!

Na kwamba taratibu zinabadilika kila siku ni kweli lakini mabadiliko ya Standard Chartered Bank Bahama hayawezi kuwa ya Tanzania!! Hii maana yake nini?!

Unaweza kukuta wakati Bahama bado unaweza kutumia MasterCard lakini sheria mpya za BoT zikasema MasterCard na VISA Card zina-facilitate online transactions kwa urahisi na hivyo zinaweza kurahisisha money laundering na kwahiyo from now, Bank zinatakiwa kutumia normal ATM Cards, na yeyote anayetaka kufanya WDL au Deposit from or to a foreign country atumie traditional money transfer methods kamavile TT!

Hilo linawezekana lakini likifanyika Tanzania katu Bahama hawatafahamu, na matokeo yake wanaweza kumwmbia "YES, ukiwa Tanzania unaweza kutumia MasterCard" wakati kumbe Tz zimeshapigwa ban!
 
Maelezo meeengi lakini bado huja.address nilichokuhoji! Kwanini mhusika asitumie initiative ya kuwasiliana na bank ya Bongo ambako atapata first hand info? Kama hiyo bank ya Bahamas haiwezi kujua operation za hiyo ya Bongo, wewe ndiyo utajua? Huoni kuwa hapa anaweza kabisa kupata majibu yasiyo sahihi na akayaamini lakini baadae yakajam-cost sana kama hayako sahihi? Huo muda aliotumia kuanzisha thread kuulizia kwa nini asingewasiliana na Standard Chartered Bongo ambako ndiyo wahusika?
 
wewe jamaa leo nime-confirm rasmi kichwani kwako kuna shida mahali.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba nichangie hata kama kwa uelewa mdogo, kwanza bank ya standard ni bank bora wana huduma safi, nilifungua acc online nikiwa kwenye chumba changu kimoja na kadi nikaletewa mlangoni kabisa sikuinua ngoko zangu kuhangaika kwenda branch, pili ukifungua acc katika bank hiyo kuna option ya kuchagua ufungue acc ipi, nakushauri fungua acc ya USD hii itakusaidia kupata huduma popote pale duniani katika tawi lolote la bank ya standard.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo. Unapata huduma zote. Mimi mwenyewe ninaishi nje ya Tanzania. Nina akaunti ya Standard Bank hiyo hiyo. Huwa ninakwenda Tanzania mara nyingi tu na mara ya mwisho nilikuwa Tanzania miezi mitatu iliyopita. Kila wakati nikiwa Tanzania sijapata matatizo yo yote ya kutumia akaunti yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…