Je nimeharibu gari kwa kuliendesha huku taa ya oil ikiwaka?

Habari wana jukwaa.
Gari yangu ni Corolla Runx Engine NZFE1 vvTi. Nimetoka kubadirisha oil (BP) kama 100km zilizopita.
Tokea siku ya Alhamis sijaliendesha hadi jana siku ya Jumanne.
Nilipoendesha kama kwa saa 1 hivi, go and stop kidogo, taa nyekundu ya oil kwenye dashboard ikawa inawaka na kuzima. Baadae ikawaka moja kwa moja. Nikapanic. Nikalizima gari, nikaliacha kama dakika 15, nikacheck oil level, iko vizuri. Nikawasha ile taa haikuwaka tena. Kwakua nilikua mbali na home nikaondoka. Baada ya kama dakika 10 issue ikajirudia. Nikafanya tena kuzima, kutulia dakika 15 kuwasha, taa haikuwaka tena. Ila baada ya dakika 10 hivi ikarudia. Nikajisogeza hadi nyumbani, nikapaki.
Asubuhi leo nikawasha ili nije kazini hafu nimuelekeze na fundi (alienibadirishia Oil), nikaondoka. Taa haijawaka. Ila baada ya dakika 15 ikaanza ule mchezo. Kwenye foreni nikizima hafu nikawasha gari, ile taa inapotezea kuwaka kama dakika 20 ila itajirudi.
TATIZO LIKAONGEZEKA.
Taa ya Check Engine nayo ikawaka. Mungu Wangu. Hapo ndio nikapanic. Ila nikajisogeza hadi kazini nimepak namngojea fundi.

Je, nimeharibu engine components nini jana nilipoendesha gari wakati oil light imewaka? Kwanini taa ya Oil imewaka wakati oil level iko vizuri? Msaada wakuu.

NB. Tokea taa ya oil iwake jana, jumla nimetembea kama KM 40 hivi hadi sasa.
Hebu elezea hiyo taa ikoje?
Ni ya duara? Au ina umbile gani?
 
Msikilizie fundi, lakin siku nyingine usijaribu kaka utakaanga engine hyo.. Ulivyofanikiwa kufika home ungemtafta fundi aje hapo hapo, hiyo ni hatari kwa engine
 
Kama taa iliwaka ni kuwa oil level ilikuwa chini au inaishia au imeisha. ....fundi akiiweka oil basi anza kuwa unafungua mfuniko wa engine oil kuangalia kila wakati, ukiona kuna povu zito jeupe kwa ndani basi ujue kuwa ulichoma gasket
 
Mkuu J33 thanks kwa ushauri.
Najua nimefanya ujinga wa kulahumiwa sana. Ila mazingira yalikua mabaya ndio maana nikalazimika kuendelea.

Performance ya gari haikubadirika, ilikua kawaida Tu, I mean ata nikizima radio, sikusikia any weird car engine noise wala gari kua nzito.

Tokea last oil change and filter, nimetembea kama KM 100-150 hivi. Niliweka Oil ya BP.

Fundi bado hajaja ila nilitaka nifanye kwanza diagnosis kwa kutumia computer (bila kuondoa gari hapa) na fundi aje aangalie kwanza kama tatizo linatibika.

Ushauri zaidi? Thanks wadau.

Nina toyota rav 4, inatumika huku taa ya oil inawaka kwa zaidi ya miezi miwili, nilimpelekea fundi kaikagua akakuta ni sensor ina matatizo,
 
Hebu elezea hiyo taa ikoje?
Ni ya duara? Au ina umbile gani?
Hapana mkuu sio ya duara.
1465458623914.jpg
 
Mpaka mda huu hujapata fundi ukatuletea mrejesho??

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Nina toyota rav 4, inatumika huku taa ya oil inawaka kwa zaidi ya miezi miwili, nilimpelekea fundi kaikagua akakuta ni sensor ina matatizo,

Hiyo case yako niyakawaida kabisa ila ya mtoa mada inaleta wasiwasi maana ilianza taa ya oil ikafuatiwa na ya check engine, kwa maana rahisi ni kuwa matatizo ya oil yameiathiri engine. So vitu kama gasket au ring piston vinaweza kuwa vimepata matatizo kutokana na kukosekana oil.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
MREJESHO WAKUU.

Fundi amelichukua. Kabla hajafungua chochote, aka-flush engine kwa kuweka liquid flani (kama 0.5 liter hivi). Baada ya kutoa Oil. Oil ilikua chafu sana. Baada ya hapo akafungua Sump kule chini ambako Oil inakaa/ inalala gari likiwa halijawashwa. Kule kulikua na ka-gauze flani (mesh, chekecheo hivi) kamezibwa sana na oil chafu/ ilioganda kama tope hivi. Hivyo Oil ilikua haipiti ili kuja juu. Ndio maana sensor ikasema hakuna Oil coz juu haifiki. NB. ingawa nikipima oil level ni nzuri. kwahiyo, oil level inakua poa ila OIL PRESSURE ipo low.
oil Pump haijawa damaged. so sump imesafishwa, oil mpya ndio inawekwa na filter mpya inafungwa.

Sijafanya computer diagnosis, jamaa wa diagnosis (member wa humu JF) alinipigia cm na kusema sorry kwa kutofika jana. ila amenipa ushauri mzuri ambao nilimwambia fundi pia na nadhani umesaidia (aliongelea kufungua sump pia).

Shukrani sana wakuu, ingawa chombo bado haijakamilika ila naona afadhali.

Kikiwashwa, tutacheki tena tuone kama taa yoyote itawaka hafu nitarudisha feedback.
 
safi sana mkuu, wewe ni mmoja kati ya watu waungwana na wanaojua kujieleza umefanya vyema sana kuleta mrejesho tunaendelea kusubiri mpaka chombo ikae barabarani na itembee japo km 100
 
Huo ni ugonjwa wa kawaida kwa magari ambayo hayafanyiwi service muda mrefu, magari mengi tunayoagiza kutoka japan huwa hawafanyii service muda mrefu. Oil inakuwa imeganda kama ugali na inaziba hio mesh[Oil Strainer] hivyo inazuia oil kupanda vizuri.

Oil pump ingekufa unge-knock-isha engine mara moja, ndio maana taa inawaka baada ya dakika kumi engine ikishapata moto.
 
mnavosema service uwa mnanimix kidogo.
me najuaga service ndio kuchange oil after every 6k kms, kuchange fluids zote, etc.
sio kugusa engine. maana wauza magari wengi uwa wanasema "enginr haijawahi kufunguliwa" kama wana jisifu. sasa si ndio kufungua ile sump chini ni part ya kufungua engine au?

to make my question clear, service gani unazosema hapa apart from changing oil, add coolant, blake fluids, steering fluids etc.
 
safi sana mkuu, wewe ni mmoja kati ya watu waungwana na wanaojua kujieleza umefanya vyema sana kuleta mrejesho tunaendelea kusubiri mpaka chombo ikae barabarani na itembee japo km 100
mkuu, thanks kwa ku-appreciate.
ka toto kamepona aisee. nimekatembeza kama km 50 hadi sasa. no taa yoyote kwenye dashboard. also, performance kama imeongezeka na fuel consumption kidogo imenifurahisha. [emoji5]
 
mnavosema service uwa mnanimix kidogo.
me najuaga service ndio kuchange oil after every 6k kms, kuchange fluids zote, etc.
sio kugusa engine. maana wauza magari wengi uwa wanasema "enginr haijawahi kufunguliwa" kama wana jisifu. sasa si ndio kufungua ile sump chini ni part ya kufungua engine au?

to make my question clear, service gani unazosema hapa apart from changing oil, add coolant, blake fluids, steering fluids etc.
Service hio hio unayosema wewe...oil change. Wenzetu Ulaya wanafanya 10k-16k interval or annual, whichever comes first. Yaani unafanya service baada ya km 15,000 au baada ya miezi kumi na mbili hata kama hujafikisha km 15k. Sasa kwa utaratibu huu ukikuta mtu anapitisha service anaweza kupiga 20,000km bila service halafu unauziwa gari wewe huku dunia ya tatu....magari ya aina hii yanaingizwa sitaki kutaja wanaoingiza nisije kuonekana nina bifu za kibiashara. Ila kuna kampuni maarufu inaleta magari yana hali mbaya sana.
 
Kama nimeshaihisi hivi, ila ngoja niipotezee tu maana mi mwenyewe naagizia hapo hapo.
 
Service hio hio unayosema wewe...oil change. Wenzetu Ulaya wanafanya 10k-16k interval or annual, whichever comes first. Yaani unafanya service baada ya km 15,000 au baada ya miezi kumi na mbili hata kama hujafikisha km 15k. Sasa kwa utaratibu huu ukikuta mtu anapitisha service anaweza kupiga 20,000km bila service halafu unauziwa gari wewe huku dunia ya tatu....magari ya aina hii yanaingizwa sitaki kutaja wanaoingiza nisije kuonekana nina bifu za kibiashara. Ila kuna kampuni maarufu inaleta magari yana hali mbaya sana.
Mkuu, isije ikawa ni wale wazee wa ''be behind''? Usisababishe presha yangu ipande [emoji3]
 
Habari wana jukwaa.
Gari yangu ni Corolla Runx Engine NZFE1 vvTi. Nimetoka kubadirisha oil (BP) kama 100km zilizopita.
Tokea siku ya Alhamis sijaliendesha hadi jana siku ya Jumanne.
Nilipoendesha kama kwa saa 1 hivi, go and stop kidogo, taa nyekundu ya oil kwenye dashboard ikawa inawaka na kuzima. Baadae ikawaka moja kwa moja. Nikapanic. Nikalizima gari, nikaliacha kama dakika 15, nikacheck oil level, iko vizuri. Nikawasha ile taa haikuwaka tena. Kwakua nilikua mbali na home nikaondoka. Baada ya kama dakika 10 issue ikajirudia. Nikafanya tena kuzima, kutulia dakika 15 kuwasha, taa haikuwaka tena. Ila baada ya dakika 10 hivi ikarudia. Nikajisogeza hadi nyumbani, nikapaki.
Asubuhi leo nikawasha ili nije kazini hafu nimuelekeze na fundi (alienibadirishia Oil), nikaondoka. Taa haijawaka. Ila baada ya dakika 15 ikaanza ule mchezo. Kwenye foreni nikizima hafu nikawasha gari, ile taa inapotezea kuwaka kama dakika 20 ila itajirudi.
TATIZO LIKAONGEZEKA.
Taa ya Check Engine nayo ikawaka. Mungu Wangu. Hapo ndio nikapanic. Ila nikajisogeza hadi kazini nimepak namngojea fundi.

Je, nimeharibu engine components nini jana nilipoendesha gari wakati oil light imewaka? Kwanini taa ya Oil imewaka wakati oil level iko vizuri? Msaada wakuu.

NB. Tokea taa ya oil iwake jana, jumla nimetembea kama KM 40 hivi hadi sasa.
Piga picha hyo taaa inayowaka then weka hapa nikuambie ni kitu gani kimetokea
Taa ya check engine huwa inawaka kutokana na mambo mengi so plz usipanik
Fanya kama nilivyokuambia nione ni nn
 
Mkuu, iliwaka taa kama ya chano hivi. Ila fundi alivyobadirisha Oil na Ku-flush engine mambo yakawa mukide.

779a3ecab96eed821453d0c65aa637e9.jpg
 
mkuu, thanks kwa ku-appreciate.
ka toto kamepona aisee. nimekatembeza kama km 50 hadi sasa. no taa yoyote kwenye dashboard. also, performance kama imeongezeka na fuel consumption kidogo imenifurahisha. [emoji5]

Mara nyengine badilisha na petrol filter ambayo watu wengi hawaibadilishi na wala hawaijui. Hii inasadia kupunguza matumizi ya mafuta
 
Back
Top Bottom