Nianze kwa ku kiri kuwa nimelelewa kwenye maadili ya kikristu lakini pia nimebahatika kuishi maeneo ambapo Waislam ni wengi. Tukiwa wadogo wazazi wetu walituruhusu tuhudhurie Madrasa. Watoto wengi hapo mtaani kwetu walitoka familia za Kiislam.
Katika harakati zangu za kijipanga kupambana na Dhambi ili niweze kuishi vizuri hapa duniani na hatimaye kuyarithi makao huko mbinguni, najiuliza dhambi ni nini? Je dhambi ina sifa zipi?
Kwa nini nauliza haya maswali? Ukweli ni kwamba kutokana na kusikia mahubiri tofauti tofauti kuhusu dhambi imebidi mimi nitake kufahamu dhambi ni kitu gani na Je tunaweza kuainisha sifa za dhambi ambazo zitakuwa Universal ili kuondoa mkanganyiko kwa wanadamu na hivyo kutusaidia kuziepuka?
Mfano ni swala la pombe. Hii ni HARAMU kwa baadhi ya dini, halali kwa baadhi.
Kuoa wake wengi
Kula aina fulani ya nyama kutoka kwa wanyama fulani,
Mimi nafikiri tukiweza kuainisha dhambi itatusaidia kuwa na usawaziko na kuenenda katika njia zinazompendeza Muumba wetu.