Je, nimetenda dhambi?

Je, nimetenda dhambi?

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
640
Reaction score
958
Nianze kwa ku kiri kuwa nimelelewa kwenye maadili ya kikristu lakini pia nimebahatika kuishi maeneo ambapo Waislam ni wengi. Tukiwa wadogo wazazi wetu walituruhusu tuhudhurie Madrasa. Watoto wengi hapo mtaani kwetu walitoka familia za Kiislam.

Katika harakati zangu za kijipanga kupambana na Dhambi ili niweze kuishi vizuri hapa duniani na hatimaye kuyarithi makao huko mbinguni, najiuliza dhambi ni nini? Je dhambi ina sifa zipi?

Kwa nini nauliza haya maswali? Ukweli ni kwamba kutokana na kusikia mahubiri tofauti tofauti kuhusu dhambi imebidi mimi nitake kufahamu dhambi ni kitu gani na Je tunaweza kuainisha sifa za dhambi ambazo zitakuwa Universal ili kuondoa mkanganyiko kwa wanadamu na hivyo kutusaidia kuziepuka?

Mfano ni swala la pombe. Hii ni HARAMU kwa baadhi ya dini, halali kwa baadhi.

Kuoa wake wengi
Kula aina fulani ya nyama kutoka kwa wanyama fulani,

Mimi nafikiri tukiweza kuainisha dhambi itatusaidia kuwa na usawaziko na kuenenda katika njia zinazompendeza Muumba wetu.
 
nini chimbuko la neno dhambi?

kwanini isiwe ni neno kosa tu.?
Au
Dhambi ipo kiroho na kosa ipo kidunia?
 
Binaadam ukiwa kama msimamizi wa viumbe wengine,umepewa kitu utashi,utashi ndio unakuelekeza jambo lipi ni baya lipi ni zuri.

Kila jambo unatakiwa ulifanye kwa sababu maalum tu sio kufanya sababu linakufurahisha,mfano ni hiyo kulewa.
Kama unalewa na unafurahi,basi usiwe kero,usumbufu na maudhi kwa wengine.
 
Dhambi hupatikana kwa nia mbaya, nia njema hampi mtu dhambi.
Huu ni definition yako ya dhambi? Nakubaliana na wewe huenda hii nayo ikawa sifa ya dhambi. Uenda tukatakiwa ku define vizuri zaidi.
 
Binaadam ukiwa kama msimamizi wa viumbe wengine,umepewa kitu utashi,utashi ndio unakuelekeza jambo lipi ni baya lipi ni zuri.

Kila jambo unatakiwa ulifanye kwa sababu maalum tu sio kufanya sababu linakufurahisha,mfano ni hiyo kulewa.
Kama unalewa na unafurahi,basi usiwe kero,usumbufu na maudhi kwa wengine.
Okay, mimi nipo hapa kukusanya maoni then tunatoka na definition ya dhambi. Ni dhambi hata kushika chupa la kileo kwa baadhi ya dini.
 
Back
Top Bottom