Hivi yule mhaya na huyo Singa singa walikuwa wanawaza nini kuwatesa wananchi wenzao kiasi kile? Kwani hapakuwa na ujanja mwingine wa kuishawishi serikali kukodi hayo majenereta kwa capacity charge kubwa? Si wangewapa rishwa tu, kulikuwa na haja gani ya kufungulia mabwawa maji yaishe halafu wakamdanganya Rais Kikwete kwamba hata baada ya miaka 10 mabwawa hayatajaa, halafu mwezi uliofuata tu, mvua zikanyesha na yakajaa hadi maji yanamwagikia juu, na hapo mkataba washasaini...Halafu unakuta kasheshe lote kuiweka nchi gizani master mind walikuwa wahuni wawili tu, muhaya mmoja na rafiki yake muhindi. Sometimes kiongozi lazima uwe mkatili kwa masirahi ya wengi
Vyanzo vya uzalishaji was umeme vimeongezekaBado nakumbuka machungu makali tuliyopitia Watanzania mnamo mwaka 2006 enzi za mkwere wakati taifa lilipopitia kipindi kigumu cha mgao wa umeme kuwahi kushuhudiwa katika historia.
Je, nini hasa kimefanyika kukomesha mgao? Au wale waliokuwa wakihongwa kufungulia mabwawa wamestaafu au ni nini? Whats going on?!
Unasemaje?🤔Umeme bado haujawa that much stable lakini ni 1000 times better. Kama huoni pengine umri unakubana maana mpaka watoto wa primary wana iPads.
Kukupa picha tu, ulikuwa unapiga pasi ngui za wiki nzima ili angalau umeme ukipotea uendelee na kazi. Kifupi Hali ilikuwa mbaya
Una matatizo ya kusoma au kuelewa?Unasemaje?🤔
Mzee wa bongo fleva bila shaka halijamfikia mezani au jamaa wameongeza ubani kwenye chetezo, kwenye vigoda vyao, bila kufanya hivyo mambo hayawaendei poa.Bado nakumbuka machungu makali tuliyopitia Watanzania mnamo mwaka 2006 enzi za mkwere wakati taifa lilipopitia kipindi kigumu cha mgao wa umeme kuwahi kushuhudiwa katika historia.
Je, nini hasa kimefanyika kukomesha mgao? Au wale waliokuwa wakihongwa kufungulia mabwawa wamestaafu au ni nini? Whats going on?!
Pesa za umeme wa Nyerere zinaenda wapi?Umeme miaka ya nyuma ulikuwa unategemea mabwawa ya Mtera, Kidatu, Kihansi na Nyumba ya Mungu peke yake. Ugunduzi wa gesi wakati wa Mkapa na ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi wakati wa Kikwete umefanya Tz isitegemee tena mvua kuzalisha umeme wake.
Sasa tunazalisha umeme mwingi kuliko tunavyohitaji angalau kwa 300MW zaidi. Pia mtandao wa usambazaji umeme mikoani na pia katika miji umeboreshwa sana kipindi cha Kikwete na Magufuli. Siku zijazo baada ya kukamilika kwa mradi wa Stiegler tutakuwa na ziada kubwa ya umeme hasa kuanzia mwaka 2023 kwa kipindi fulani tutatafuta tumwuuzie nani umeme, lakini kuanzia 2027 tunaweza tukaanza tena kutafuta namna ya kuongeza uzalishaji wa umeme.