Je, nini hutokea endapo taifa lolote lile ulimwenguni litashindwa kulipa deni?

kibla matata

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2020
Posts
412
Reaction score
380
Tunafahamu kwamba mtu yeyote yule au taasisi inapokwenda kuchukua mkopo bank au kwa mtu lazima kwanza kuwe na makubaliano. Makubaliano hayo ni pamoja na dhamana ya kitu fulani.

Je, taifa lolote linapokopa fedha bank au kwa taifa lingine dhamana huwa ni nini na endapo nchi ikashindwa kulipa deni kwa muda muafaka nini hutokea?

Maana kuna mataifa tunasikia yana daiwa madeni tangu yapate uhuru hadi leo bado hawajalipa...

NAOMBA WAJUZI WA MAMBO MNIJUZE 🙏🙏🙏
 
umeuliza swali zuri,
Nafikiri[sina uhakika] kwenye mkataba wao kunakuwepo pia na kipengele cha maridhiano endapo deni halitalipwa kwa wakati.
nasubiri comment za wajuvi wa mambo nijifunze zaidi
 
Viwanja vya ndege, Mbuga za Wanyama, Majeshi, Ardhi, n.k.
 
Wadsi watachukua kile walichokubaliana na mdaiwa
Nalog off
 
Nahisi nchi itatawaliwa tena! Wananchi wanakua watumwa kama enzi zile...
 
Utafuata masharti yao mengine hasa kwenye biashara zenye faida kwao,na hilo ndio lengo kuu la kukopeshwa ili uishi chini ya maamuzi yao.
 
Bilashaka baadhi ya mali za nchi husika zitakamatwa na/au kusimamiwa na wadai ili kufidia au kulipa deni. Hakuna mkopo hutolewa bila dhamana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukigoma kulipa ina maana IMF na World bank, wanakata au kupunguza ushirikiano na wewe(haupati tena faida za kuwa kule)hili ni jambo kubwa baya ukifanyiwa, na baadae labda ikifikia kukuwekea vikwazo vya biashara, mwenyewe utaamua kukaa mezani ulipe kidogo kidogo.
NB:Hata marekani ambae ni mfadhili mkubwa ana deni World Bank kama sikosei, mikopo ni muhimu katika kukuza uchumi,tatizo ni tunaitumiaje

Kwa huku kwetu ngazi ya taifa inatumia mkopo kama ngazi ya familia yani kula vizuri mapocho pocho kuliko kujenga😊
 
Mbona Dr Magufuli anajenga sana barabara na madaraja
 
Kuna jina hutumika la "Sovereignty", laamanisha nchi huru kajitawala. Hili laamanisha hakuna yeyote yule anaweza kutoka nje aje kuwaeleza jinsi ya kutawala au alazimishe jambo lifanywe na nchi huru. Ifikapo deni, ikiwa nchi litashindwa au kukataa kulipa, hakuna kile ambacho kitaweza kufanywa ndani ya mipaka kulazimisha ulipaji wa deni. Lakini inje ya mipaka mengi yaweza kufanyika, hapa itategemea na sheria na korti za hizo inchi zingine. sote twaelewa ndege kushikwa, ikiwa inchi lina fedha katika benki ugaibuni......, mali ya ubalozi katika nchi mbali mbali zinaweza pigwa mnada, nchi moja linaweza amua kuweka vikwazo kwenye international trade wakijaribu kulazimisha ulipe deni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…