Je, nini kifanyike kwenye sheria za ndoa ili kuwapa motisha vijana wafunge ndoa (sio kuoa) kwa wingi zaidi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Mwanasheria anasema, kuoa na kufunga ndoa ni vitu viwili tofauti, binafsi yake hapendelei kufunga ndoa sababu ya ‘repercussions’ endapo mtagombana.

Anasema ni bora uwe na ‘X’ kuliko kuwa na ‘Mtalaka / Mtaliki’.
===========================

Ahsanteni wanasheria.
 
Sheria zisizo na usawa zinachochea Team Kataa Ndoa kupata uungwaji mkono na Watu wengi
Bila shaka , moja wapo unazungumzia mgawanyo wa mali sivyo? Je, upi uhalali wa mtu kudai mgawanyo wa mali zisizo katika jina lake, yaani anakuwaje na mchango katika gari ambalo jina lake halipo, kama alichangia si inapaswa kadi iwe na majina ya wote waliochangia kulinunua?

Kama mchango wake ni kufua, kupika, na kuosha vyombo, basi ahakikishe analipwa malipo yote stahiki kwa kazi hiyo papo hapo. Shida ni kwamba, anafua , kupika, na kuosha vyombo kwa ajili yake mwenyewe na watoto wake mwenyewe wa kuwazaa, sasa atalipwa na nani kwa kitu anachojifanyia mwenyewe?. Yaani ni kama fundi ajenge nyumba yake mwenyewe halafu adai tena pesa ya ufundi.

Sheria zifanyiwe maboresho, je, kwa namna gani?
 
Bila shaka , moja wapo unazungumzia mgawanyo wa mali sivyo? Je, upi uhalali wa mtu kudai mgawanyo wa mali zisizo katika jina lake, yaani anakuwaje na mchango katika gari ambalo jinalake halipo, kama alichangia si inaoaswa kadi iwe na majina ya wote waliochangia kulinunua?

Vijana wengi Kwa Sasa Wanaona Bora waishi kihuni ili kuepuka mambo kama hayo.
NI Vizuri serikali ikalitazama hili mana Huko tuendako mambo yatazidi kuwa mabaya
 
Bila shaka , moja wapo unazungumzia mgawanyo wa mali sivyo? Je, upi uhalali wa mtu kudai mgawanyo wa mali zisizo katika jina lake, yaani anakuwaje na mchango katika gari ambalo jina lake halipo, kama alichangia si inapaswa kadi iwe na majina ya wote waliochangia kulinunua?

Kama mchango wake ni kufua, kupika, na kuosha vyombo, basi ahakikishe analipwa malipo yote stahiki kwa kazi hiyo papo hapo. Shida ni kwamba, anafua , kupika, na kuosha vyombo kwa ajili yake mwenyewe na watoto wake mwenyewe wa kuwazaa, sasa atalipwa na nani kwa kitu anachojifanyia mwenyewe?. Yaani ni kama fundi ajenge nyumba yake mwenyewe halafu adai tena pesa ya ufundi.

Sheria zifanyiwe maboresha, je, kwa namna gani?
suala la msingi ni kuwa na 'prenuptial agreement' kabla ya ndoa.
 
Je, prenuptial agreement inabatilisha (forfeit) haki za kimsingi zilizoainishwa kwenye sheria ya ndoa au inakuwaje? Na Je, Prenuptial agreement inatambulika kikatiba kwenye sheria ya ndoa? Nimeisoma sheria ya ndoa, sijaona neno ‘Prenuptial agreement’ popote pale, au labda nilisoma kwa haraka sikuona; ufafanuzi tafadhali..

Na je, unajua ni kwanini wanandoa wengi hawafanyi hiyo ‘Prenuptial agreement’?
 
Kwa Tanzania sidhani kama Prenuptial Agreement inatambulika kisheria, nadhani bado haijawa effected. Lakini nadhani ni jambo MUHIMU SANA KUZINGATIWA kwa wakati wa Sasa hapa Tanzania, ni muhimu mno. Wanaume wengi sana wamekuwa wahanga wa kudhulumiwa Mali zao na Wanawake watalaka wao ambao wamekuwa wakufunga 'ndoa za kimkakati' za kutafuta Mali kupitia 'utapeli wa ndoa.'
 
Ndoa zikiwa nyingi faida gani taifa linapata ? Na zikiwa chache hasara gani taifa linapata ?
Sasa kwanini vijana wanao zalisha wanawake bila ndoa wanasumbuliwa kila kukicha kwamba wafunge ndoa? Maana yake ni kwamba ndoa ni kitu muhimu katika ustawi wa familia na jamii kwa ujumla. Shida ni sheria ya KITAPELI iliyotunhwa enzi za ujima na kwa sasa imekuwa mwiba mkubwa kwa wanaume wanaotaka kufunga ndoa. Sheria iboreshwe, je; iboreshwe kwa namna ipi?
 
kuishi na mke/mume wa ndoa kuna faida zake lakini kwa baadhi ya familia zinachukulia mahusiano ya ndoa kama ajira/uwekezaji hasa pale mwanaume anapokuwa na kipato kikubwa na tatizo linaweza kuwa kubwa akifariki au wakitalikiana rejea kesi ya mmiliki wa ngurdoto hotel au case ya davis mosha.

matatizo huwa kidogo mke akiwa ndiye mwenye kipato kikubwa rejea uchebe na shilole na yule mbunge aliyepewa zuio la mahakama kutumia jina la mtalaka wake.
 
Bila shaka , moja wapo unazungumzia mgawanyo wa mali sivyo? Je, upi uhalali wa mtu kudai mgawanyo wa mali zisizo katika jina lake, yaani anakuwaje na mchango katika gari ambalo jina lake halipo, kama alichangia si inapaswa kadi iwe na majina ya wote waliochangia kulinunua?

Kama mchango wake ni kufua, kupika, na kuosha vyombo, basi ahakikishe analipwa malipo yote stahiki kwa kazi hiyo papo hapo. Shida ni kwamba, anafua , kupika, na kuosha vyombo kwa ajili yake mwenyewe na watoto wake mwenyewe wa kuwazaa, sasa atalipwa na nani kwa kitu anachojifanyia mwenyewe?. Yaani ni kama fundi ajenge nyumba yake mwenyewe halafu adai tena pesa ya ufundi.

Sheria zifanyiwe maboresho, je, kwa namna gani?

shida sio mgawanyo wa mali pekee

mke ana haki ya matunzo hata kama mmedivorce kwa kosa lake yeye... hata kama umemfuma anazini ukamwacha kama amezaa na wewe bado ana haki ya kula hela zako. na hata kama hamjazaa ana haki na mali zako zilizopatikana kipindi cha ndoa... zinaa yake haimtoi kwenye mali
 
Na hiki ndio kinanifanya niamini kwamba wanaume wanaofunga ndoa lazima watakuwa na ubongo nusu kichwani.
Hayo matumzo kisheria yanaitwa ‘ALIMONY’, yaani azae nje ya ndoa, ukimpa talaka bado umtunze yeye na toto lake la nje ya ndoa.., na hii hupelekea wanaume wengi kukodi majambazi kuuwa wake zao ili kukwepa kutoa talaka na kupoteza nusu ya jasho lao huku akiendelea kumtumza yeye na bwana wake mpya. ‘ALIMONY’ ni sheria ya kiwendawazimu, na ni kikwazo kikubwa kwa wanaume wenye akili timamu kufunga ndoa (ukiacha wale wenye ubongo nusu), pia ni chanzo kikubwa cha ‘Staged murders’.
 
inategemea si ndoa zote zina matatizo pamoja na changamoto ndogo ndogo zilizopo. mfano ni miaka 18 sasa niko kwenye ndoa na sijawahi kujuta kuoa japo si siku zote ni furaha na nyakati hizi hata yule asiye na mke/mume anaweza pitia kwa namna nyingine.
 
Kuvuka barabara huku umefunga macho na ukafika salama si jambo la ajabu. Ila itakuwa ni ajabu kama utakuja jukwaani kujisifu au kujitolea mfano juu ya hilo.
 
bandeko andeko nimeeleza awali kabisa, mwanasheria anasema ‘Kuoa / kuolewa’ na ‘Kufunga ndoa’ ni vitu viwili tofauti. Pia nimeeleza jinsi ndoa ilivyo muhimu katika jamii, na ndio maana nikauliza, nini kifanyike kwenye sheria za ndoa ili vijana wengi zaidi wapate motisha ya kufunga ndoa?
 
Cheti cha ndoa kwa wanawake imegeuka kuwa asset na rasilimali kuu kwao, ukimnyima tu pesa ya kusaidia ndugu zake, anakwambia bora aende mahakamani mgawane mali.., hii changamoto inadidimiza utayari wa vijana kufunga ndoa.
 
Back
Top Bottom