Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
Salute Comrades
Intro
Mnamo mwaka 1969 mwanamuziki aitwae Jim Sullivan alirekodi albamu aliyoipa jina la U.F.O, ndani ya albamu hiyo kuna mistari anaimba kua ..aliacha familia yake akawa ametekwa na aliens . Baada ya miaka sita gari lake lilikutwa shambani jangwani kwenye jiji la New Mexico mpaka leo hajapatikana wapi alipo.
Anaitwa James Antony Sullivan kazaliwa August 13 1940 katika eneo la san Diego jijini California marekani. Alikua muimbaji, mtunzi na mpiga gitaa.
Jinsi alivyopotea
Tarehe 4 march 1975 Jim Sullivan aliondoka jijini Los Angeles akielekea Nashville, alikua yeye peke yake ndani ya gari lake aina ya Volkswagen. Siku iliyofuata polisi wa patrol barabarani walimuonya kutokana na uendeshaji wake wa kasi hivyo akaona apumzike kwenye Motel ya La mesa eneo la santa rosa jijini New Mexico, lakini taarifa zingine zinasema hakulala hapo kwenye hiyo hotel, aliacha funguo kwenye mlango wa chumba cha hotel (ndani).
Siku iliyofuata gari lake lilikutwa umbali wa Maili 26 kwenye shamba lililokua linamilikiwa na familia ya Gennetti, na hakuna yoyote aliyemuona akitoka ndani ya hilo gari. Ndani ya gari lake kulikutwa Pesa,gitaa,karatasi, nguo na copy kadhaa za albamu yake. Hakuonekana tena mpaka leo watu wanasema kua labda aliuawa, au alipotea, wengine wanasema kua inawezekana ni kutokana na mambo aliyoimba ndani ya wimbo wa Allien abduction.
Kuna mwili pia ulipatikana maeneo ya shambani uliofanana na jim lakini hakua yeye hivyo mpaka leo hajaonekana wala hajulikani alipo.
Ndugu wana Jf je nanyi mwaona nini kitakua chanzo cha kupotea kwake?
Na kwa masrahi yapi labda mpaka wampoteze?
Msimamo wa mwandishi kuhusu Unidentified Flying Objects (UFO)
Mimi Da'Vinci naamini kua hakuna cha UFOs wala Allien, ni mkakati wa nchi kubwa kubwa kututisha tu wanadamu na kutu Brain wash tu. Ni mambo tu wanayotengeneza ili kuona dunia si sehem salama.
Vitu kama vile..

- Ozone layer kutoboka
- Virusi vya ukimwi
- Kutuaminisha kua kuna mtu aliyewahi tokea anaitwa D.B Cooper wakati hajawahi kuwepo.
- Kwamba kuna jiwe angani linakuja kwa kasi kuigonga dunia
- Etc etc
Da'Vinci