Naomba nione picha ya Yesu....achana na yule jamaa aliyeigiza movie ya yesuYesu alikuwepo vitabu vinaelezea,sayansi hadi picha zake..hivyo ukishamjua Yesu basi Huna haja ya ku-doubt uwepo wa Mungu
DuuuhNaam kiongozi ndio maana mimi hua naamini kua hakuna kitu kinachoitwa D.B. Cooper bali ni character tu kwenye story waliyotunga na kutuaminisha kua lilitokea.
Db cooper ni kama madenge he's never existed
What?
nimemcheck,inawezekana jamaa hakufanikiwa kutua...Jamaa asuefahamika aliyeteka ndege mwaka 1975 akaomba pesa kisha akaruka nazo mpaka leo haifahamiki alienda wap na alitokea wap
swali tata,inaonesha ransom aliyopewa hakuitumia cos namba zake zilikuwa zimerekodiwa...Kama hakufanikiwa alienda wapi!?
Ukisoma ufunuo Yohana aliona nyota ikiiangukia dunia na wengi walikufa na kuangamia, nashangaa wao husema eti sayari Mara jiwe sisi tushaambiwa nyota itaanguka sio kugongwaSalute Comrades
Intro
Mnamo mwaka 1969 mwanamuziki aitwae Jim Sullivan alirekodi albamu aliyoipa jina la U.F.O, ndani ya albamu hiyo kuna mistari anaimba kua ..aliacha familia yake akawa ametekwa na aliens . Baada ya miaka sita gari lake lilikutwa shambani jangwani kwenye jiji la New Mexico mpaka leo hajapatikana wapi alipo.
Anaitwa James Antony Sullivan kazaliwa August 13 1940 katika eneo la san Diego jijini California marekani. Alikua muimbaji, mtunzi na mpiga gitaa.
Jinsi alivyopotea
Tarehe 4 march 1975 Jim Sullivan aliondoka jijini Los Angeles akielekea Nashville, alikua yeye peke yake ndani ya gari lake aina ya Volkswagen. Siku iliyofuata polisi wa patrol barabarani walimuonya kutokana na uendeshaji wake wa kasi hivyo akaona apumzike kwenye Motel ya La mesa eneo la santa rosa jijini New Mexico, lakini taarifa zingine zinasema hakulala hapo kwenye hiyo hotel, aliacha funguo kwenye mlango wa chumba cha hotel (ndani).
Siku iliyofuata gari lake lilikutwa umbali wa Maili 26 kwenye shamba lililokua linamilikiwa na familia ya Gennetti, na hakuna yoyote aliyemuona akitoka ndani ya hilo gari. Ndani ya gari lake kulikutwa Pesa,gitaa,karatasi, nguo na copy kadhaa za albamu yake. Hakuonekana tena mpaka leo watu wanasema kua labda aliuawa, au alipotea, wengine wanasema kua inawezekana ni kutokana na mambo aliyoimba ndani ya wimbo wa Allien abduction.
Kuna mwili pia ulipatikana maeneo ya shambani uliofanana na jim lakini hakua yeye hivyo mpaka leo hajaonekana wala hajulikani alipo.
Ndugu wana Jf je nanyi mwaona nini kitakua chanzo cha kupotea kwake?
Na kwa masrahi yapi labda mpaka wampoteze?
Msimamo wa mwandishi kuhusu Unidentified Flying Objects (UFO)
Mimi Da'Vinci naamini kua hakuna cha UFOs wala Allien, ni mkakati wa nchi kubwa kubwa kututisha tu wanadamu na kutu Brain wash tu. Ni mambo tu wanayotengeneza ili kuona dunia si sehem salama.
Vitu kama vile..
Ahsante
- Ozone layer kutoboka
- Virusi vya ukimwi
- Kutuaminisha kua kuna mtu aliyewahi tokea anaitwa D.B Cooper wakati hajawahi kuwepo.
- Kwamba kuna jiwe angani linakuja kwa kasi kuigonga dunia
- Etc etc
Da'Vinci
Shida IPO hapo. Kitabu cha ufunuo mnakitafsiri kama kilivyoandikwaUkisoma ufunuo Yohana aliona nyota ikiiangukia dunia na wengi walikufa na kuangamia, nashangaa wao husema eti sayari Mara jiwe sisi tushaambiwa nyota itaanguka sio kugongwa
Sasa tukitafsiri kwa michoro au Kwa sanamu kilizo nazo?Shida IPO hapo. Kitabu cha ufunuo mnakitafsiri kama kilivyoandikwa
Nafanya kama lengo la mwandishiHua unafanyaje ili kutafsiri mistari ya biblia?
Duuh,hapa panaweza kuwa na ukweli kati ya uliyoyasemamkuu heshima kwako kaka mkubwa..[emoji4] [emoji4]
Lakini mkuu kumbuka kuwa kifo cha huyu jamaa kimeleta utata mwingi sana kwa sababu aliwahi kuhukumiwa kifungo cha maisha kutokana na kesi ya kumuua mke wake wa pili na kupelekea Hatimaye kushtakiwa na mauaji ya mke wake mwaka 1998, alikimbilia Costa Rica, kisha Panama, Venezuela na hatimaye kwenda Thailand, ambapo alikamatwa mwaka 2002.
Alirejeshwa Atlanta kwa kesi, alihukumiwa mwaka 2006 na kuhukumiwa maisha ya gerezani.
Alikuwa na mwendesha mashtaka David Boone ambaye alikuwa anamtetea kwani inasemekana alifarakana na huyo mke wake wa pili.
Mke wake aliamua kumshitaki klkwani aliamini kuwa endapo kesi itafika mahakamani basi sehemu ya mali za Sullivan atapewa huyo mwanamke kwani alidai taraka.
Ndipo bwana James akamua kumtafuta jangili mmoja anaitwa Phillip Harwood na kumpa kiasi cha , $25,000 kumuua mke wake Lita Sullivan alipofungua mlango wa nyumba yake ya mji wa Atlanta ..
Lakini kutoka na kesi hiyo kuunguruma mahakamani kwani ilikuwa ni lazima James Sullivan ahukumiwe kifungo cha maisha lakini wakili wake alimtetea ambapo ilipelekea kukamatwa kwa yule jangili aliyelipwa pesa ndefu na kufungwa miaka 20 .
Lakini James alifungwa kifungo cha nje kwani wakili wake alimtetea kuwa alikuwa bado ana mawazo juu ya kifo cha mke wake hivyo hangeweza kuvumilia maisha ya gerezani ,.
kutokana na kuwa na mawazo ya kufiwa na mke wake au sijui alikuwa anafanya unafiki ndo akawa na mawazo ya hapa na pale na kupelekwa kujiua yeye mwenyewe shambani huko bila kumhusisha mtu..
shida ilikuwa ...... ni wapi mwili wake ulipotelea,..
Baadhi ya documentary zinasema kifo chake kinahusishwa na FBI waliokuwa wanamsaka kwa kuwa alikuwa na makosa mengi sana ikiwemo la kuimba nyimbo ambazo zilikuwa zinawapa hofu kubwa watu( Alliens and UFO) na kukimbiza gari hasa nyakati za usiku kwa kasi sana ..japo alipewa onyo lakini hakuiacha tabia ile..
Lkini pia inasemekana kuwa familia ya marehemu Lita ndo ilipanga njama za kulipiza kisasi kwa kumuua binti yao..hivyo na wao wakaamua kumpoteza bila ushahidi
Lakini documentary zingine zinasema jamaa aliuliwa na FBI kwani alianza kuzungumzia mambo ya mental abduction yaliyokuwa yanafanywa na Aliens kwa viongozi wastaafu katika serikali ya marekani kuhofia kutoa siri za uhusiano wa seeikali ya marekani na Viumbe toka sayari za mbali( Aliens)..
Lakini ushahidi mwingine unasema kuwa ilikuwa ni hofu yake ya kuogopa kifungo cha maisha hivo aliamua kujiua kwa kuwa alikuwa mkiwa aliyejaa hofu na roho ilikuwa inamsuta kwa kumuua mkewe...
Mpaka leo bado FBI wanaendelea na uchunguzi sijui watapata jawabu juu ya kupotea kwake..
Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa anaamini uwepo wa Yesu wakati Alliens picha zao zimechorwa zama za Kale kabla ya Yesu nadhani ni huko AztecPicha za Yesu kivipi ndugu? Haya mambo yanayohusisha imani ni fumbo manake hata kuhusu Aliens kuna various proof abt them, cha msingi ni kuamini unachoona sahihi.