Je, nini kimepelekea wajasiriamali (wafanyabiashara) kuwa wengi nyakati hizi? Je, nyakati zijazo kutatokea nini kwenye hili kundi la watu?

Je, nini kimepelekea wajasiriamali (wafanyabiashara) kuwa wengi nyakati hizi? Je, nyakati zijazo kutatokea nini kwenye hili kundi la watu?

Haswaa, tunapenda dezo.! Kilimo na ufugaji tumeachia wazee huko vijijini.

Leo nimetafuta maziwa ya ng'ombe mtaa mzima nimekosa, nimekaa chini nikatikisa kichwa in magufuli style nikajisemea ihiiiii, aah.!
Sema huko nako kunahitaji mtaji mkubwa sana vinginevyo inabidi utumie nguvu ni kazi ambazo zinachosha sana ndio maana wengi wanazikimbia
 
Kwanini anataka afanye biashara ?
  • Ipo kwenye damu kwamba ndio hulka yake ?
  • Anachopata hakitoshi hence anatafuta zaidi kwa kubahatisha na huku ?
  • Anaokoteleza kwa kumpiga ganji muajiri; yaani kule kwenye kazi hafanyi kazi yake vizuri (100%) bali anatumia muda wa kule kufanya ya huku ?

In short watu wanafanya biashara ili iweje ? Ni hobby, waongeze kipato kiwe maradufu au ni kutafuta mkate wa kila siku ? Jibu la hapo utaona wengi ni kutafuta mkata ndio maana wengi stress haziwaashi na tabasamu usoni limekuwa thing of the past.. (mwendo wa kuhamisha madeni na kuongeza riba) Na kwa uhakika wa kwamba biashara ni ngumu na sio ya kila mtu angalia ni biashara ngapi zina-fail; Na shukuru Bongo hakuna ushindani zikija corporations hapa ni mwendo wa watu kufunga vibanda vyao na kuanza kulalamikia masuala ya Uzawa...
Nimeona biashara nyingi sana zimefeli, nimeona watu wengi sana wakiisha na madeni makubwa kisa biashara mengine yamepelekea mpaka nyumba zao kupigwa mnada na bank. Kiufupi watu wanafanya biashara kwa kuiga hakiona fulani kafungua biashara flani na ameona mwenzie anauza nae anataka kufungua biashara hiyo hiyo bila kuangalia ubunifu biashara lazima ifeli
 
Mbona wageni wanafaulu sana au mashine ni bei ghali sana wahindi waarabu wanauzia juisi viungo vya chakula na madudu ya ajabu wanafaulu sisi ndiyo tumekuwa wateja wap wakubwa tunafeli wapi?!!!!!!!!

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Hapo jibu ni moja kukua kwa uchumi, viwanda vingi vinaongezeka na kila siku vinazalisha unategemea mnunuzi awe mmoja?, hapana kwahyo na maduka lazima yaongezeke kwakuwa upatikanaji wa bidhaa ni rahisi na pia sababu nyingine kuwepo na njia rahis ya usafirishaji au uagizaji wa bidhaa kutoka nje, mfano china to Tanzania watu wanaagiza na kupata mizigo yao kwa wakati tofauti na zamani au miaka ya nyuma, pia kuboreshwa kwa miundo mbinu kama vile barabara, mawasiliano, umeme nk. Kwa kila sehemu ambayo inawezesha kuongezeka kwa wafanyabiashara (inawarahisishia shughuli zao). Sababu zipo nyingiii kwa leo ngoja niishie hapaa.............
 
Ukiangalia nchi "zilizoendelea" sipendi label hii! Ila utaona kuwa vitu vinakuwa formalized zaidi utakuta kuna kampuni chini ya 5-10 zinacontrol kila sector na wanatumia hiyo nguvu yao kuweka vikwazo kwa mtu yoyote mpya kuingia kwenye sector yao, wanasukuma na kuhonga serikali kuweka sheria za kuzuia watu wapya, wanamiliki malighafi, wanaweka mikataba na suppliers ambayo hairuhusu mwingine kupata chance, wanatengeneza patents zisizokuwa na maana na wanakushitaki ukitengeneza chochote kinachofanana, kama kuna kampuni 2-3 zinazoshindana wana "collude" na kupanga bei kunakuwa hakuna ushindani wa kweli.

Mwishoni tutaenda huko.
 
Hamna kitu,mkumbo tu wapo wanafanya kwasababu Fulani alifanikiwa kwenye kitu Fulani Hawa huwa wanafungua na kuendelea kufanya biashara hata km wanapata asala,wengine wanawafungulia wake au wapenzi wao ili wapate sehem ya kushinda ili asi cheat ni vurugu tu
 
Back
Top Bottom