Je, niolewe naye? Baba yake alizaa na Mama yangu

Je, niolewe naye? Baba yake alizaa na Mama yangu

Mkuu inapendeza ukiwa ndani ya mada bila kutoka kwenye mstari. Huna haja ya kufanya assumption ambazo hazipo just kwa kuwa umependa kufanya hivyo.

Hoja ni kuwa Mtoto wa baba mkubwa nina muunganiko wa damu na yeye kupitia baba yangu.

Huyu Mwanaume A sina Muunganiko naye wa damu kupitia Baba wala Mama. Ila tumeunganishwa kupitia dada yangu tu. basi. Sasa mwongozo wako au ushauri uangalie kupitia hoja hii.

Mama, kumbuka hapo nyuma umejitetea/jieleza kuwa hamchangii baba wala mama. Nami nimekujibu from the same angle. Sasa umekuja na hoja ya mahusiano ya damu. Ok!

Ikiwa A anamwita B, baba ni lazima atamwita mama yako mama. A na dada yako wanauhusiano wa damu wa moja kwa moja zaidi ya yale ya mtoto wa baba mkubwa. Then, jiweke wewe kwenye nafasi ya A. Je! Ni halali kwake kumwoa mtoto wa mama mkubwa (mke wa baba mkubwa) ambaye hakuzaa na baba mkubwa? Ndani ya mada, je ni halali A kumwoa mtoto wa mama wa kambo ambaye mama wa kambo hakuzaa na baba yako?
 
mmh hili suala linahitaji busara sana maana ukiangalia huyo ni kama kaka yako coz ni kaka wa dada yako.hata kama baba yake hakuoana na mama yako lakini mtoto waliezaa ndo alieleta undugu wenu.kwahiyo huyo ni kaka yako.ila jaribu kufuatilia kimila zaid na ww mwenyewe msimamo wako uko vp
 
huyo ni ndugu yako usioe wala kuolewa naye

kuna madhara ya kiafya, kijamii na kiakili

kiafya kama kuna magonjwa ya kurithi yataendelea badala ya kukomeshwa

kijamii je unaendaje kutoa mahali kwa na nani atakukubali

kiakili, hamtafurahia maisha yenu ya ndoa kutokana na taarifa mchanganyiko mlizo naz

kidini, ka kuwa ni ndugu haikubaliki ninyi kuoana

tulia tafuta mwingine
 
Kimsingi huyo kijana si ndugu yako kwa damu ila ni ndugu ya huyo dada yeko mwingine kwa kuwa wanachangia baba. Nawe ndugu yako hi huyu dada ambaye mnachangia mama. Juu ya kuolewa ni ruksa kisheria, vinginevo mila na desturi (heshima na utu wema) unatumika kama kanuni nyingine ya kuwakataza kuoana. Ongea na mama yako mzazi usikie atakushauri vipi.
 
Mimi sioni shida hapo, na nina imani hata wewe huoni shida! Komazeni undugu ambao wazazi wenu waliuanzisha!
 
hebu fikiria kuwa ingekuwa ni siri huijui?ungefanyaje?ungeeolewa tu
so wapo wengi wanaolewa na ndugu zao bila kujua......
ndo maana dini inatambua 'mahusiano ya ndoa tu'
kama mama yako angeolewa ndoa rasmi na baba yake huyo kijana ingekuwa hadithi tofauti...
for now,wewe olewa tu..........
Ninakubaliana nawe The Boss kwa hili kwani kidini ni pale tu ambapo watoto wa damu moja ni wale tu waliozaliwa katika ndoa. Hii ni kusema kuwa licha ya wewe, hata huyo baba yako angeweza kumwoa ndugu yako C.

Tukiwacha ya dini, tuje ya kidunia na kimantiki. Ukweli ni kuwa katika haya ya kidunia na kimantiki haikubaliki baba kumwoa mwanawe. Lakini linapokuja suala lako, huyo mwanamume hana uhusiano wowote wa damu na BL. Hata kama huyo Baba angekuwa amemwoa mama yake, bado kidamu huyo mwanawe aliyezaa kwengine si kaka yake. Kwa maelezo hayo na kwa mawazo yangu, Big Lady anaweza kuolewa na huyo kijana.
 
Ninakubaliana nawe The Boss kwa hili kwani kidini ni pale tu ambapo watoto wa damu moja ni wale tu waliozaliwa katika ndoa. Hii ni kusema kuwa licha ya wewe, hata huyo baba yako angeweza kumwoa ndugu yako C.

Tukiwacha ya dini, tuje ya kidunia na kimantiki. Ukweli ni kuwa katika haya ya kidunia na kimantiki haikubaliki baba kumwoa mwanawe. Lakini linapokuja suala lako, huyo mwanamume hana uhusiano wowote wa damu na BL. Hata kama huyo Baba angekuwa amemwoa mama yake, bado kidamu huyo mwanawe aliyezaa kwengine si kaka yake. Kwa maelezo hayo na kwa mawazo yangu, Big Lady anaweza kuolewa na huyo kijana.

Mamamia,watoto wa damu moja si wale tu waliozaliwa ndani ya ndoa. Hata wale waliozaliwanje ya ndoa kama wanachangia damu kwa njia ya wazazi au mzazi mmoja bado diniinatambua kwamba wako ndugu wa damu hata kama uhusiano wao hautokani na ndoahalali. Hivyo kama wako ndugu wa damu hata dini haikubali kufungisha ndoa hiyokwa sababu za kiroho na za kibaolojia. Tunapoongea mambo ya vizuizi vya ndoahasa cha undugu (consanguinity) hatuangalii uhalali wa mahusiano ya wazazi wawahusika bali uchangiaji wao wa damu.
Kwa kesi hii ya huyu dada, kimsingi hakuna uhusiano wa damu kati yao kwa vilewazazi wao wamewazaa na partners wengine. Pili, hao wazazi hawaishi pamoja kamamme na mke (walizaa kama marafiki tu na urafiki ukaisha). Kwa hivo huyu dadakwa mawazo yangu aweza olewa na yule kijana, vinginevo heshima za mila na ukoovinawashauri vinginevo.

 
hakuna kitu ka laana hapa,undugu gani huo mnataka kuutengeneza kwa kuunganisha big g iliyotafunwa juzi na jana? Olewa mama kama mmependana,ongea na viongozi wako wa dini wakupigeni maombi ya kutosha muondoe iyo so called laana

Asante my dear. Ila naona maoni ya hapa yanazidi kuniweka njia panda.
 
Duuh! Huku unakotaka kwenda sasa siko kabisa, unapotea njia. Kama ningekuwa mimi nisingeolewa kabisa maana huyo ni kaka yangu hata kama hakuna muunganiko wa damu. Naomba nitangulize samahani kwa swali hili ....hivi mama yako angekuwa hai, unadhani angekushauri vipi?

Sijui Mkuu wangu. Alifariki ningali mdogo sana.
 
Swali zuri. Kwa kifupi hii ni INCEST. Inaweza kuwaletea madhara ya kibaiolojia kwa watoto watakaozaliwa. Kumbuka waswahili wanaosema binamu nyama ya hamu ndio wale wale wanaoamini mtoto amerogwa pale atakapozaliwa na mtindio wa ubongo au/na matatizo mengine. Mimi sikushauri uolewe nae!

Hivi madhara ya kibaolojia yanaweza kupatikana hata kama hamna connection yoyote ya damu?
 
Back
Top Bottom