Je nisipo hudhuria harusi ya rafiki huyu kuna lawama?

Ni rafiki wa kushibana kwetu kama kwao na kwao kama kwetu, urafiki wetu ni zaidi ya undugu maana tunasaidiana kuliko hata hao ndugu zetu wanavyo tusaidia

Urafiki wetu ulianza na kukua kwa kasi tukiwa school na kwa bahati nzuri kila tukivuka level moja kwenda nyingine tunajikuta tumepangiwa shule moja yani hadi raha hatujawahi kugombana hata siku moja katika urafiki wetu japo hadi sasa wote ni majobless kwa maana hatujaajiriwa pamoja na kumaliza chuo miaka kama 7 iliyopita

Sasa kasheshe ilianza nilipotaka kuoa (mimi nilioa punde tu baada ya kumaliza chuo) nilikuja gundua kuwa mtu niliotarajia kufunga nae ndoa kumbe rafiki yangu nae alikuwa anamtaka maana alikuwa classmate wetu na alivyojua nataka kufunga nae ndoa ni kama alipunguza urafiki japo hakuonesha hisia zake wazi wazi. Hii inshu niliijua kupitia kwa dada yake na aliyekuwa mchumba wangu na sasa mke wangu alinipa story nzima kwani alikuwa akiambiwa na mdogo wake mambo ya mahusiano yake

Mwanzo nilisita na nikataka kugairi kumuoa huyu mwanamke kwa kuhofia kuwa huenda anaweza kutuchanganya wote wawili au nikamuoa kwa shinikizo la ndoa ila kumbe hanipendi anampenda rafiki yangu ila baadae yeye alinifuata na kuniambia yote na kukiri kuwa moyo wake uko kwangu, sikutilia maanan nikawa busy na mdada mmoja mwingine hivi mpaka pale dada yake alipoamua nae kunifuata na kuniambia kuwa nimuelewe mdogo wake kwani alichokuwa anasema ni kweli

Basi nilifanya maamuzi ya kumuoa na mpaka sasa hivi tunaishi vizuri tu japo changamoto za ndoa hazikosekani, ila toka hivyo rafiki yangu hakuoa na hata kwenye Ile harusi yangu hakuja ila mchango alitoa na muda wote huo mawasiliano yalikuwa kawaida japo sio kama mwanzo maana hata kule kutembeleana sasa hakupo

Sasa kanitaarifu kuwa mwezi wa kwanza anafunga ndoa na amenipa muariko na hata ndugu zake wananitafuta ili niwe kampani katika hiyo harusi ( kwa sisi waislam kuna yule anaemsindikiza bwana harusi kama partner wake). Binafsi napenda niende ila kila nikiwaza ya huko nyuma napata ukakasi na ukizingatia hata ya kwangu hakuja vipi hii namimi nisipoenda kuna lawama?

Kwenu wanajamii
Nenda tena usijipe pressure kwa kujishtukia... ishi kama uelewi ili huyo anaye elewa akueleweshe wewe...
 
Wanataka kuwatesa tu watoto
Maana mlishaona kinachofuta ni watoto
Sasa watoto watakula nini ?
Hii Imani kuwa lazima chakula kitoke kwa mwanaume ili watoto wale au unaolewa ili ukalishwe, kuvishwa na kunenepeshwa na mwanaume huko wengine tushatoka

Kazi (job) sio kibarua ila vibarua vipo kibao mtaani

Mimi baba alikuwa tajiri na mama alikuwa na uhakika na vitu vyote hivyo nilivyotaja hapo juu ila mwisho wa siku mambo yalibadirika baada ya kufa mzee na tukaishi kwa shida kubwa kulala na njaa ilikuwa mazoea kwetu toka nipo 6yrs hadi nahitimu chuo ni shida tu

Je hapo nilikuwa na tofauti gani au na afadhali gani na mtoto aliezaliwa na jobless?
 
Unajuaje yeye ndio anaona kuwa nimemchukulia demu wake? Najaribu kuwaza tu
Mkuu wewe huna sababu yeyote ya msingi ya kutokwenda labda mkeo awe kakukataza ambayo nayo ni udhaifu mkubwa.

Wewe ungekuwa yeye kipindi unaoa ungeenda? Jamaa alitoa mchango lakini akampa space bibie awe comfortable.

Jaribu kuvaa viatu vyake utamuelewa
 
Rafiki yako ana akili na busara, sababu ya kutohudhuria ndoa yako inajulikana pia alipunguza ukaribu ili asiharibu ndoa yako.
Pia kama mlikuwa na ukaribu ilikuwaje msiambiane kuhusu mahusiano ya wanawake zenu Hadi unakaribia kufunga ndoa hapo Kuna kitu unaficha.
Umeongea kile nilichotaka kushauri. Cha msingi audhulie hiyo arusi ya rafiki yake.
 
Mkuu wewe huna sababu yeyote ya msingi ya kutokwenda labda mkeo awe kakukataza ambayo nayo ni udhaifu mkubwa.

Wewe ungekuwa yeye kipindi unaoa ungeenda? Jamaa alitoa mchango lakini akampa space bibie awe comfortable.

Jaribu kuvaa viatu vyake utamuelewa
Jaribu kuvaa viatu vyangu pia maana hata kumuoa huyu mwanamke nimebet tu sijajua how far they gone
 
Siyo lazima uende. Ila pia ukienda Haina madhara. Hayo mambo ya zamani unapotezea tu. Angalia moyo wako unakuambia nini. Pia jaribu kupata maoni ya mkeo huyo aliyewagombanishaga. Binafsi ningeangalia tu nafsi yangu inaniambia nini. Wala nisingeumiza kichwa.
 
Mkuu sikushauri uende bcs inaweza leta ukaribu mkubwa zaidi kati yenu na siku za usoni ikaleta dosari. ni ushauri tu. Lakn sababu ya kukualika anataka mshuhudie ni kama kisasi ua Kam sivyo kwann asisitize.
 
Umewaza kama niwazavyo yani yeye kwangu hakuja niende mimi ilhali kuna kamsonono ka chini chini
 
Ahsante kwa ushauri, japo mambo za mapenz ni ngumu kushaurika at least huu nimeuelewa ila kichwani mwangu bado nina maswali chungu nzima
Wewe ni type ya watu wanaopenda ku complicate mambo. Yaani wivu usikie wewe, halafu bado uje kutuuliza why uende? Tabia za ajabu ajabu kwa mwanaume
 
Kwenye complication ushauri muhimu
 
Nenda,kama jamaa alitoa mchango ina maana alionesha yupo pamoja na wew ila hakutaka kuhudhuria ndoa maana asingekuwa comfortable na hata mkeo asingekuwa comfortable,pia angesema awe anakuja kwako labda kuna vitu vingetokea

Huenda jamaa na mkeo walikuwa wameshapiga hatua kazaa huenda hata alishawahi mshika kalio,kwahyo kuwa mbali na nyinyi alitumia akili sana
 
Aloooh
 
Ni rafiki wa kushibana kwetu kama kwao na kwao kama kwetu, urafiki wetu ni zaidi ya undugu maana tunasaidiana kuliko hata hao ndugu zetu wanavyo tusaidia

Urafiki wetu ulianza na kukua kwa kasi tukiwa school na kwa bahati nzuri kila tukivuka level moja kwenda nyingine tunajikuta tumepangiwa shule moja yani hadi raha hatujawahi kugombana hata siku moja katika urafiki wetu japo hadi sasa wote ni majobless kwa maana hatujaajiriwa pamoja na kumaliza chuo miaka kama 7 iliyopita

Sasa kasheshe ilianza nilipotaka kuoa (mimi nilioa punde tu baada ya kumaliza chuo) nilikuja gundua kuwa mtu niliotarajia kufunga nae ndoa kumbe rafiki yangu nae alikuwa anamtaka maana alikuwa classmate wetu na alivyojua nataka kufunga nae ndoa ni kama alipunguza urafiki japo hakuonesha hisia zake wazi wazi. Hii inshu niliijua kupitia kwa dada yake na aliyekuwa mchumba wangu na sasa mke wangu alinipa story nzima kwani alikuwa akiambiwa na mdogo wake mambo ya mahusiano yake

Mwanzo nilisita na nikataka kugairi kumuoa huyu mwanamke kwa kuhofia kuwa huenda anaweza kutuchanganya wote wawili au nikamuoa kwa shinikizo la ndoa ila kumbe hanipendi anampenda rafiki yangu ila baadae yeye alinifuata na kuniambia yote na kukiri kuwa moyo wake uko kwangu, sikutilia maanan nikawa busy na mdada mmoja mwingine hivi mpaka pale dada yake alipoamua nae kunifuata na kuniambia kuwa nimuelewe mdogo wake kwani alichokuwa anasema ni kweli

Basi nilifanya maamuzi ya kumuoa na mpaka sasa hivi tunaishi vizuri tu japo changamoto za ndoa hazikosekani, ila toka hivyo rafiki yangu hakuoa na hata kwenye Ile harusi yangu hakuja ila mchango alitoa na muda wote huo mawasiliano yalikuwa kawaida japo sio kama mwanzo maana hata kule kutembeleana sasa hakupo

Sasa kanitaarifu kuwa mwezi wa kwanza anafunga ndoa na amenipa muariko na hata ndugu zake wananitafuta ili niwe kampani katika hiyo harusi ( kwa sisi waislam kuna yule anaemsindikiza bwana harusi kama partner wake). Binafsi napenda niende ila kila nikiwaza ya huko nyuma napata ukakasi na ukizingatia hata ya kwangu hakuja vipi hii namimi nisipoenda kuna lawama?

Kwenu wanajamii
Nenda bhana.
 
Back
Top Bottom