SI KWELI Je, nukuu/maneno haya yametolewa na mzee Warioba?

SI KWELI Je, nukuu/maneno haya yametolewa na mzee Warioba?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu

Katika pitipita zangu nimekutana na hizi kauli ambazo zimetolewa na Mzee Warioba ni kweli?







Warioba 3.jpg
Warioba 2.jpg
Warioba 1.jpg
Warioba 4.jpg
 
Tunachokijua
Jaji Joseph Warioba Amewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1985-1990, amewahi pia kuwa Mkuu wa chuo cha kilimo cha Sokoine (SUA) baada ya uteuzi wa mwaka 2016.

Madai

Kupitia mtandao wa Facebook kumekuwa na grafiki zilizobeba nukuu zinazodaiwa kuwa ni za Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba kuhusu masuala ya uchaguzi na kuwataka Watanzania waunge mkono serikali iliyopo madarakani, huku akipongeza namna jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa.

Grafiki zilizobeba nukuu hizo zina utambulisho wa chombo cha habari cha Jambo TV.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa nukuu ama maneno hayo hayajatolewa na Jaji Joseph Warioba kama inavyoonekana kwenye grafiki hizo.

Disemba 17, 2025 Jaji Warioba alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kupiga picha ya pamoja kisha kusambazwa katika vyombo mbalimbali vya habari. Licha ya picha hizo kusambazwa katika vyombo vya habari lakini haikuelezwa ni nini haswa kilichojadiliwa katika mkutano huo.

Aidha hakuna kumbukumbu yoyote inayoonesha kuwa Jaji Warioba alizungumza chochote mara baada ya uchaguzi na hata baada ya kukutana na Samia hadi wakati uhakiki huu unafanyika, hivyo maneno na nukuu hizo ni za kughushi.

JamiiCheck imefanya ufuatiliaji zaidi na kubaini kuwa grafiki zilizobeba nukuu hizo hazijachapishwa na Jambo TV na hivyo utambulisho wao umetumika kwa lengo la kupotosha, pia aina ya mwandiko (fonts) zilizotumika si za chanzo hicho.
Kwa kutumia ufuatiliaji wa maneno unabainisha kuwa Sio kweli hizi kauli zimetolewa na mzee Warioba bali zimetengenezwa kwa lengo la kupotosha umma.

Hivyo taarifa ambazo zimechapishwa katika kurasa za mitandao ya facebook na nyingine zinapotosha uhalisia wa kile ambacho alikizungumza waziri mkuu msitaafu pindi akifanya mahojiano wa waandishi wa habari mwaka 2024

Sambamba na hivyo ukurasa wa rasmi wa jambo Tv Instagram na twiter zamni X haijachapisha taarifa yoyote ambayo inamuhusu mzee Warioba akizungumzia masuala ya kuwaunga mkono viongozi na kupongeza uchaguzi ambao umefanyika kwa mfano wa moja ya kauli ambayo inaonekana kwenye graphic ni ’’Nawaomba wananchi wawaunge mkono viongozi wote waliochaguliwa maana shughuli za maendeleo huanzia ngazi za chini’’

Taarifa ambayo imechapishwa na Jambo tv Instagram kumuhusu Mzee sinde Warioba ni siku ya ambayo amekutana na Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan na ilikuwa Habari picha ambayo inasomeka ’’RAISI SAMIA ATETA NA WARIOBA IKULU DSM”

Waziri mkuu Mstaafu amekutana na raisi samia siku ya Disemba 17 2025

Sambamba na taarifa hiyo picha ambayo imetumika sio ya sasa bali ametumia picha ya Disemba 04 2024 wakati ambao jaji Mstaafu sinde warioba alikuwa anafanya mahojiano na vyombo vya habari juu ya uchaguzi wa mitaa ambao ulifanyika na hali ya kisiasa nchini Tanzania
 
Nguvu inayotumika kufanya kila namna kuhalilisha kilichofanyika Oktoba 29, 2025 ingetumika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi tungesonga mbele. Waziri Mkuu mliyepewa ndiye huyo kutwa anachambana kwenye majukwaa utadhani bado yuko kwenye kampeni, ni kama anaongoza kikundi cha propaganda na sio baraza la mawaziri
 
Back
Top Bottom