Je, Nyerere angeogopa mikutano ya hadhara?

Je, Nyerere angeogopa mikutano ya hadhara?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Siku sikia kabisa wakati wa awamu ya Mkapa mwalimu Nyerere akipinga hata mara moja mikutano ya hadhara. Sasa inashangaza miaka hii bado kuna watu wanaogopa upinzani kiasi cha kuwatumia polisi kunyima vibali vya mikutano.

Mimi namshauri Raisi na serikali yake kuruhusu mikutano na kujibizana kwa hoja. Hata siku moja chama hakitaweza kujirekebisha chenyewe bali hoja na kuona mwelekeo wa wananchi ni muhimu kuliko kukaa vikao na kusifiana kila siku.

Narudia Nyerere alikuwa haogopi maswali, debate wala mikutano wakati ule Mrema alikuwa anafanya mikutano kila mara bila shida yeyote.
 
Unajua Nini kilitokea miaka ya mwishoni mwa 1960? Alifuta vyama vingine vyote na kubakiza TANU tu ambacho baadae kikawa CCM. Wakati wa mkapa upinzani ndio ulikua unaanza na wakati wa kikwete upinzani uliimarika lakini badala ya kutumia majukwaa yakisiasa vizuri yalianza matusi majukwaa na tuhuma zisizo na ushahidi.

Wakati wa Magufuli alizuia mikutano kwakuadai haina tija katika maisha ya mwananchi wachini na ni upotevu wa muda.
 
Nyerere alikuwa muoga zaidi ya kunguru akamsingizia sharobaro oscar kambona kuwa kaiba mabilioni wakati bajeti ya Tz ilikuwa milioni tu

Mzee Mtemvu chama chake cha ANC kikafutiliwa mbali
 
Nyerere angefuta vyama vya upinzani
 
Mrema kafanya mikutano wakati wa Mkapa sio wa Nyerere, Ingekuwa wakati wa Nyerere angepigwa shaba tu
 
Back
Top Bottom