Je, nyumba bado ni asset ya uhakika kuliko asset zingine zote?

Asset kubwa ya binadamu ni akili yake.
Mkuu Kama haina sifa ya kukuingizia pesa sasa Na baadae hiyo haina sifa ya kuitwa Asset. Nyumba ambayo mtu anakaa yy mwenyewe Tu hai qualify kuwa asset labda Kama umepangisha au Una biashara unafanyia ndani yake
 
Reactions: BAK
Hongera kujenga maeneo hayo.....bt kuna majumba ya maana kitunda, tandika...mbagala na hata mkuranga ndani ndani vichochoroni....all in all kila mtu abaki na iman yake mkuu.

Ndio maana nikakwambia huko madongo poromoka haiwezi kua asset .. Kama una nyumba mjini ni asset kubwa tu.. Mikocheni nimeimaliza toka 2000 naipangisha toka kipindi hicho ... Now ni faida tu gharama zilishatoka kitambo..so depends hiyo nyumba yako iko wp
 
Wenzetu wazungu walishaacha zamani kujenga nyumba baada ya kugundua kwamba nyumba sio assets wameiachia serikali yao ijenge na wao wapangishe. Ukiachana na Matetemeko kuna Vita siku hizi angalia kule Libya au Syria majumba ya kifahari yalivyo haribiwa na Mabomu utagundua kwamba nyumba si kitu.
 
Mkuu bado nyumba ni mali,usiogopeshwe na tetemeko
 
Mkuu, nashukuru umetupanua mawazo kwa mchango wako huu.
 
Hilo ni kweli kabisa mwenye. Mtu mwenye nyumba ambaye hana bima mimi simuelewi kabisa lakini kuna bima nyingine kama za tetemeko la ardhi na mafuriko hazitolewi na insurance companies.

Mkuu kweli ni asset lakini pasipo bima, ni kujidanganya tu.

Leo hii hakuna mabenki yaliyokuwa yanayotegemea nyumba zilizowekwa kama dhamana ya mikopo huko Bukoba na sasa hayaamini kilichotokea?
 
Nakubaliana na mawazo ya Wiseboy , Nyani Ngabu na MR UNIINFORMED

Kila Discipline zina Defination yake ya Nyumba,
1. Accountants - Kila chenye thamani ni Asset na unakimiliki
2.Entrepreneurs - Assets ni zile zinazo zalisha mapato, ikiwa gharama inazidi kipato inageuka kuwa Liability
 
kuna current assets na fixed assets. According to book of rich dad poor dad,kuwa na nyumba ni majanga. inakuingiza kwenye gharamaz a repair na renovation.
 
BIMA hazilipi NATURAL CALAMITIES hata TERRORISM ISSUES.
 
90% ya nyumba za Tanzania ni consumables not capital. But they are assets. I think the issue should be ni capital??
 
Hilo la wazungu kuacha kujenga nyumba halina ukweli wowote. Katika nchi nyingi za magharibi zikiwemo UK, USA, Canada, Germany, Denmark, Norway, France, Sweden etc bado Wafanyakazi wa Serikali na sekta binafsi wengi hufurahia sana wanapoweza kununua/kujenga nyumba zao na bado ni assets ambazo zinathaminiwa sana na pia zina thamani kubwa sana. Pamoja na matetemeko ya ardhi, moto na mafuriko lakini bado nyumba zinathaminiwa sana katika hizo nchi zote nilizozitaja hapo. Na sasa hivi baadhi zimeanza kuweka restrictions kwa matajiri toka china ambao hupenda kununua nyumba katika nchi hizo wakati mwingine wako tayari hata kulipa mara mbili au zaidi ya bei ya nyumba husika.

 

Mawazo sahihi kabisa
 
Mkuu Kama haina sifa ya kukuingizia pesa sasa Na baadae hiyo haina sifa ya kuitwa Asset. Nyumba ambayo mtu anakaa yy mwenyewe Tu hai qualify kuwa asset labda Kama umepangisha au Una biashara unafanyia ndani yake
Miongoni mwa assets muhimu ni makazi ya uhakika wewe na familia yako. Nyumba kukulipa sio lazima iwe in terms of direct monetary earnings. Fikiria ungelipa kiasi gani kuisitiri familia yako sio tu kwa makazi lakini na kero nyingine za kupanga.
 
System Ya wazungu na waafrika kuna tofauti sana kaka, wana uhakika wa kula na kulala hata wasipofanya kazi,kutolea mfano syria na libya ni kukata tamaa Ya maisha. Nyumba ni asset and will be always asset hata mafisadi afrika nzima wanawekeza kwenye majumba kwenye miji ya maana duniani.
 
Hii dhana ya watu kuandika hapa na kuweka mahitimisho yao kwa kutumia vigezo visivyohusu kitu kwamba nyumba si asset inanishangaza sana. Duh!

Miongoni mwa assets muhimu ni makazi ya uhakika wewe na familia yako. Nyumba kukulipa sio lazima iwe in terms of direct monetary earnings. Fikiria ungelipa kiasi gani kuisitiri familia yako sio tu kwa makazi lakini na kero nyingine za kupanga.
 
Mkuu hata kwenye nchi za wazungu, nyumba bado ni asset kubwa sana kuliko asset nyingine yoyote ile, asikudanganye yoyote yule. Inaweza kutokea wakati uchumi unafanya vibaya nyumba kupoteza thamani lakini haipiti muda mrefu thamani ya nyumba itaongezeka tena na hata zaidi.

 
Hii dhana ya watu kuandika hapa na kuweka mahitimisho yao kwa kutumia vigezo visivyohusu kitu kwamba nyumba si asset vinanishangaza sana. Duh!
Inategemea una define nyumba kutoka angle gani, maana waliowengi wanaangalia kihasibu lakini sio lazima tufuate principle za accounting , kwa wengine Asset ni lazima iwe generating asset kama alivyo tafsiri Robert Kiyosaki, na ndie alie badilisha mtazamo dunian
 
bei ya nyumba inapangwa kutokana na location nyumba ilipo na sio uzuri wa nyumba.. hata ukijenga nyumba ya bilion moja chanika au kibaha huwezi kupangisha bei sawa sawa na masaki kajumba ka milion 50 tu...


Nyumba gani hiyo milion 80 unapangisha laki 2[emoji23][emoji23][emoji23] ?! Kijitonyma tu chumba laki Choo cha ku share...labda Iyo nyumba iko madongo poromoka.... Nyumba ya milion 80 ukipangisha chini laki 7 or milion
 
Nyumba bado ni asset safe, hasa ikiwa eneo zuri, tetemeko la ardhi hutokea mara ngapi kwa karne ngapi hapa Tz?
Halafu hii sio mada ya kisiasa
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…