Je, nyumba bado ni asset ya uhakika kuliko asset zingine zote?

Je, nyumba bado ni asset ya uhakika kuliko asset zingine zote?

Kwanza kabisa nyumba sio asset per se...nyumba inaweza kua asset endapo tu itakua inakuingizia hela mfano kwa kuipangisha au shughuli yoyote ile ya kiuchumi...kama nyumba unaitumia kwa makazi yako binafsi hapo hakuna asset...

Hiyo ni sawasawa na kusema mama wa nyumbani hazalishi economically au hana mchango kwy pato la familia!kitu ambacho sio. Imagine ungekua unalipa kodi mf 300K iyo hela unayoikwepa hapo ndio economic benefit ya kuwa na nyumba.Kwa hiyo nyumba ni asset na inameet definition ya asset hata km hujapangisha au huitumii kwa biashara.
 
Baada ya tetemeko kuikumba mikoa kadhaa ya kanda ziwa,nimeanza kujiuliza kama kumilki nyumba bado ni asset ya kuaminika kama tulivyozoea.

Ni kawaida kusikia mtu anasema ukitaka kuwekeza na hela yako isipotee kirahisi,wekeza katika majengo na wala si vyombo vya moto au kitu kingine chochote.

Sometimes ni bora hata chombo cha moto unaweza kukikarabati kwa gharama ndogo na kikatengamaa kuliko hekalu lililoporomoka kutokana na tetemeko.

Baada ya tukio hili la tetemeko, nimeamini asset ni ile tu iliyowekewa bima na hata kama una jumba lako lakini halina bima, basi ujue unajidanganya tu maana moto nao hauwezi kukuacha salama.

Nasema hivi kwasababu naamini inawezekana zaidi ya asilimia 97 ya nyumba zilizobomoka hazikuwa na bima yoyote ikiwemo bima ya moto na wengi wao waliamini wameshajikomboa kimaisha kwa kumiliki nyumba bila kujali ni ya ukubwa gani ili mradi tu ana nyumba.

Tukio hili liwe funzo kwa watu kuwekea bima mali zao zikiwemo nyumba zao.
Insurance companies huwa wanavoid natural disasters. Kwa Tanzania kwa vile matukio kama haya siyo kawaida inawezekana insurance companies wakacapitalize!!
 
Bado itabaki kuwa asset muhimu sana. Kwanza unafanya savings masuala ya pango.
Kikubwa ambacho watanzania tu waoga kukitumia ni kukopea bank. Ni collateral ya kuaminika sana.
Tatizo tukisha kopa tunaishia kuongeza wake au nyumba ndogo na kujenga heshima Bar!
Ngumu sana kulifanya gari kuwa collateral hasa hii mitumba tunayo nunua
Dah. ..Mwenye Enzi Mungu akubariki. .maana nilikuwa nataka kujiuliza hichi kizazi kina kwenda wapi....hongera kwa kuiona hiyo. ..trust me ni wachache wanaoona hivyo. .KEEP IT UP!
 
Ili uiite nyumba yako ni asset lazima ujiulize inakuzalishia kitu gani kwa mwaka na thamani yake ya kuiuza kwa haraka ni kiasi gani kulingana na gharama za kuipata hiyo nyumba.

Kwa hiyo swali la msingi tu, ni kwamba watu wengi wamepigwa upofu na kuamini kwamba nyumba ni asset akati sio hivo.

Kuna vitu ni quality asset kuliko nyumba
Tusaidie kuvitaja hivyo vitu...
 
Asset kama nyumba KAMWE haiwezi kufananishwa na biashara ya mahindi. Ondoa hiyo dhana yako potofu kwamba ili nyumba iweze kuwa asset ni lazima ikuingizie mapato. Hakuna kitu kama hicho kwenye accounting hivyo usijaribu kuchomeka definition za kutoka hewani.

Unajua maana ya "INFLATION" ? okay toa hilo neno "mahindi 200 bags" badala yake iwe ni "MISHAHARA YAKE 100"
kwa maana ya 250k ilikuwa sawa na mishahara yake 100, na kwa sasa mishahara hiyo 100 ni 1500k ,
 
Achana na hawa watu wanaoandika vitabu kuwazuga watu ili wao watajirike. Mjadala huu unahusu nyumba jikite kwenye nyumba tu badala ya kutanga tanga huku na kule Mkuu.
Bila shaka ndyo maana mifuko yote mikubwa inawekeza kwenye majumba. Hapa nadhan watu wanachanganya mambo...hiv mtu anayemiliki nyumba ya kuishi ya kawaida pale kariakoo utaweza kusema anamiliki liability hata kama hamuingiza mia kwa mwezi?! Wadau wanasahu kwamba unaweza kuiconvert hyo property kuwa billions in just moments...yaan mie ntajenga hadi nafwaaaa......
 
Mtoa mada Unahitaji kutambua nini maana ya asset. Kwa kukusaidia asset ni kitu kinacho generate pesa. Nyumba ya kuishi haijawai kuwa asset hata siku moja in accounting unless ni kama ya bihshara. Na kama ni ya bihashara unabidi ukumbuke kuwa any business has two sides. Loss and Profit.
 
Ili uiite nyumba yako ni asset lazima ujiulize inakuzalishia kitu gani kwa mwaka na thamani yake ya kuiuza kwa haraka ni kiasi gani kulingana na gharama za kuipata hiyo nyumba.

Kwa hiyo swali la msingi tu, ni kwamba watu wengi wamepigwa upofu na kuamini kwamba nyumba ni asset akati sio hivo.

Kuna vitu ni quality asset kuliko nyumba
Tupe mfano mkuu tunaweza pata Mawazo mazuri hapa
 
Mkuu kweli ni asset lakini pasipo bima, ni kujidanganya tu.

Leo hii hakuna mabenki yaliyokuwa yanayotegemea nyumba zilizowekwa kama dhamana ya mikopo huko Bukoba na sasa hayaamini kilichotokea?
hakuna bima kwa majanga ya asili kama hayo.........
 
kwa kipindi cha sasa nyumba zimeshuka kqa mara ya kwanza kwa mfano mdogo angalia watu wengi waliokua wanagombea flems kwa sasa wanafunga wenyewe rudi kwenye nyumba me binafsi nina wateja wangu hapa wanauziwa nyumba zao na benk moja hapa dar ni nyumba kumi na tano wanalia wanasaka walau mteja ajitokeze kabla ya mnada kwa robo tatu ya valuation report
 
Nyumba gani hiyo milion 80 unapangisha laki 2[emoji23][emoji23][emoji23] ?! Kijitonyma tu chumba laki Choo cha ku share...labda Iyo nyumba iko madongo poromoka.... Nyumba ya milion 80 ukipangisha chini laki 7 or milion
Usibishe vitu usivyokuwa na uhakika navyo
 
Yaan hata kama ingekuwa bima ni lak 5 kwa mwaka...bado ningelipa...na ningelipa miaka yote ambayo namiliki hyo property...why

Bse hyo bima inanipa kinga ya majanga eg moto...wizi...third party compasation...wakat ni kweli kwamba unaweza kumaliza miaka 10 bila kupata janga....lakin ni ukweli usiopingika kwamba janga likikufika utakumbuka bima.

Sbb ya pili ni kwamba kila mwaka nyumba inapanda thaman...so kiulinganifu na bei nayolipa bima itabaki kuwa ndogo.

Hapa bima itakuwa na maana tu kama hauna nia ovu...yaan kutengezea janga feki ili bima ikulipe...maana kama utatengeneza janga...una uwezekano mkubwa usipate fidia.

Mkuu ni vema kutambua kuwa sio nyumba zoote hupanda thamani kila mwaka, zipo nyumba nyingi sana kupoteza thamani kila mwaka, fatilia vitu vifuatavyo kwenye nyumba , Rate ya capital gain ya nyumba maeneo ilipo, Inflation Rate ya uchumi eneo husika au nchi otherwise nyumba inweza kupungua thamani badala ya kupanda kinachodanganya ni MONETARY TERMS(tarakim za pesa dhidi ya thamani halisi)
 
Sure...nyumba unajenga milion 80....kisha unapangisha laki mbili kwa mwez...kwa mwaka milion 2.4, kuirudisha hiyo 80milion yataka miaka kedekede kama miaka 33 hivi...na hapo hiyo ni mtaji uliowekeza sio faida.....na hapo bado unahitaji ukarabati...inakuwa imezeeka....pili hiyo hela haiwez kukaa tu hapo had kufika 80m....so mm binafsi huwa siamin kuchukua hela yako yote na kujenga nyumba eti asset....80milion unaweza fanya biashara kubwa na ukapata faida two times ndani ya miaka 2.
Otherwise kuwa na nyumba ya kuishi ni muhimu bt not kama ideology ilivyo kwa wabongo wengi kwamba ukiwa na nyumba ww ni tajiri..
Mjomba hizo hesabu za uongo. Ukisema kodi ya laki mbili inahitaji miaka 33 kulipa milion80 unamaanisha kodi itakuwa ileile kwa miaka 33! Huo ni upotoshaji mkubwa ukichukulia kuwa kodi za nyumba zinapanda karibu kila baada ya miaka 3!
 
Mkuu ni vema kutambua kuwa sio nyumba zoote hupanda thamani kila mwaka, zipo nyumba nyingi sana kupoteza thamani kila mwaka, fatilia vitu vifuatavyo kwenye nyumba , Rate ya capital gain ya nyumba maeneo ilipo, Inflation Rate ya uchumi eneo husika au nchi otherwise nyumba inweza kupungua thamani badala ya kupanda kinachodanganya ni MONEY TERMS(tarakim za pesa dhidi ya thamani halisi)
Nakubaliana na wewe kabsa kwa maana pana....lakin katika inchi ambazo uchumi unakuwa kama zetu hiz bado value itaongezeka...si kwa 100% but itaongezeka.

Pia ileweke hapa nyumba inategemea na mtaji wa mtu katika kuwekeza...hapa wengi wanazungumzia bajet za mil 80 na zaid....kwangu hyo ni bajet kubwa sana...mie binafs nalenga soko la watu wa chini...zile nyumba zimejengwa kama shule....yaan unajaza humo wapangaji wanakuwa wanapigia taarabu humoooo mwisho wa mwez wananipa changu....yaan mfano ipo moja ina vyumba 10 kwa elf 50 kila mwez...! Hii nyumba hata ikiporomoka thaman bado nipata mtu wa kupanga room 50elf.

So my take...ni jinsi mtu anavoendea hili jambo la soko unalolifikiria
 
kwa kipindi cha sasa nyumba zimeshuka kqa mara ya kwanza kwa mfano mdogo angalia watu wengi waliokua wanagombea flems kwa sasa wanafunga wenyewe rudi kwenye nyumba me binafsi nina wateja wangu hapa wanauziwa nyumba zao na benk moja hapa dar ni nyumba kumi na tano wanalia wanasaka walau mteja ajitokeze kabla ya mnada kwa robo tatu ya valuation report

Wasaidie wale wanao oota kuwa ni lazima kila mwaka nyumba inapanda thamani, kibaya zaidi wakidanganywa na wahasibu kuwa kufuata matarakimu tu ya pesa(money terms) wala sio thamani halisi ya nyumba(asset value) na bado inategemea na hali ya uchumi, watu wengi tu siku hizi wanafilisika kwa kujenga nyumba kibao kwa mitazamo ya wahafibu eti nyumba ni asset inayo appreciate in value
 
Nakubaliana na wewe kabsa kwa maana pana....lakin katika inchi ambazo uchumi unakuwa kama zetu hiz bado value itaongezeka...si kwa 100% but itaongezeka.

Pia ileweke hapa nyumba inategemea na mtaji wa mtu katika kuwekeza...hapa wengi wanazungumzia bajet za mil 80 na zaid....kwangu hyo ni bajet kubwa sana...mie binafs nalenga soko la watu wa chini...zile nyumba zimejengwa kama shule....yaan unajaza humo wapangaji wanakuwa wanapigia taarabu humoooo mwisho wa mwez wananipa changu....yaan mfano ipo moja ina vyumba 10 kwa elf 50 kila mwez...! Hii nyumba hata ikiporomoka thaman bado nipata mtu wa kupanga room 50elf.

So my take...ni jinsi mtu anavoendea hili jambo la soko unalolifikiria
shukrani sana kukupata na mm nina wazo hilo naomba nikutafute ili kupata uzoefu wako please
 
Mjomba hizo hesabu za uongo. Ukisema kodi ya laki mbili inahitaji miaka 33 kulipa milion80 unamaanisha kodi itakuwa ileile kwa miaka 33! Huo ni upotoshaji mkubwa ukichukulia kuwa kodi za nyumba zinapanda karibu kila baada ya miaka 3!
kwani hiyo 80 mln ni ile ile miaka yoote ? ? ? kama kodi inapanda na uwekezaji wa hiyo nyumba nao lazima upande km kodi imepanda mara 2 yaani mfn toka 50,000 hadi 100,000 basi yawezekana kabisa thamani ya ile 80 mln kwa sasa ikawa 160 mln sasa linganisha hy kodi 100,000 kwa mtaji 160,000,000 unarudi kule kule 33yrs,,,, jamaa yuko sahihi cha kujifunza hapa ni nini maana ya mfumuko wa bei ktk uwekezaji INFLATION EFFECTS IN INVESTMENTS
 
Back
Top Bottom