Je, nyumba za mawaziri Mikocheni nani anaishi kwa sasa?

Je, nyumba za mawaziri Mikocheni nani anaishi kwa sasa?

Davan

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2020
Posts
1,125
Reaction score
1,413
Baada ya serikali kuhamia Dodoma ni wazi kuwa mawaziri wote sasa wanatakiwa kuishi Dodoma jirani na ofisi zao.

Je, hizi nyumba zao za mikocheni kwa sasa hivi nani anaishi humo?

Nashauri tupewe watumishi wa DSM au serikali izipangishe kwa wanachi kwa kodi ndogo ili kila mwananchi afaidi matunda ya nchi yake.

"HESLB 6% kila mwaka ni wizi"
 
Kwani kabla ya kuhamia Dodoma, hizo nyumba za Dodoma alikuwa akiishi nani si zilikuwepo? Na walipotoka Dar wamefika na kuingia tu.
 
Kuna chama wakishinda urais watarudi Magogoni hivyo nyumba zitatumika kuanzia 2025 Lissu akiwa atakapochukua nchi.
 
Wakiwa dawa wanaishi humo, wakiwa Dom wanaishi lodge za pale majengo.
 
Waweke kodi rafiki watu tupo tutakaa 200000-300000
Yaani dar saivi ma TOLET mengi yapo tupu,,,, hayo mamijengo ya mawaziri ni tupu hata Wateja hamna labda km Unataka wakakae machinga
 
Yaani dar saivi ma TOLET mengi yapo tupu,,,, hayo mamijengo ya mawaziri ni tupu hata Wateja hamna labda km Unataka wakakae machinga
kuna mkenya mshkaji wangu akionaga bei za nyumba kule instagrama za dsm huwa anashangaa sana jumba kali unasikia 400,000 kwa mwezi huwa namuambia real estate Tanania ni kama imekufa tangu 2016 hata frames za biashara siyo deal tena zamani kabla hata haijaisha frame watu washalipia kabisa siku hizi wadada wa kuuza urembo nguo wengi wanauzia home au kwenye magari yao wanatembeza
 
Kuna chama wakishinda urais watarudi magogoni hivyo nyumba zitatumika kuanzia 2025 Lissu akiwa atakapochukua nchi.

Yaani huyu Lodi Lofa bado anaota kuongoza Tanzania. Hili nalo ajabu la dunia.
 
Attachments

  • Screenshot_20210116-125246_Gallery.jpg
    Screenshot_20210116-125246_Gallery.jpg
    80 KB · Views: 2
Baada ya serikali kuhamia Dodoma ni wazi kuwa mawaziri wote sasa wanatakiwa kuishi Dodoma jirani na ofisi zao.
Je hizi nyumba zao za mikocheni kwa sasa hivi nani anaishi humo?
Nashauri tupewe watumishi wa DSM au serikali izipangishe kwa wanachi kwa kodi ndogo ili kila mwananchi afaidi matunda ya nchi yake.

"HESLB 6% kila mwaka ni wizi"

Mkipewa hamchelewi kuanza kufugia ng'ombe na kuku
 
Nakubaliana na wewe ila bado yako maeneo nyumba ni ghali kidogo.
Pia uwepo wa baby walkers umeshusha bei ya nyumba mjini, mtu anaweza kupanga nyumba nzima bunju kwa laki 2.5 akaendesha vitz hadi posta bila shida kuliko kupanga nyumba ya laki 6 sinza.

Back
Top Bottom