Somo No.6
Kama umetoka kwenye familia isiyo na misingi, watu hawaheshimiani wala kupendana, watu wanashindana badala ya kusaidiana. Kama unahisi familia inakutumia kama kifaa kwa manufaa binafsi na hakuna anayejali kuhusu wewe, fanya hivi. Kwanza elewa kwamba, iwapo familia yako hawapendani, hiyo ni dalili kwamba watoto wako hawatakuwa na sehemu ya kukimbilia ikitokea haupo. Jitahidi kuhakikisha unatafuta mwenza anayetokea familia yenye hali tofauti na unayotoka wewe. Watoto wako wana haki ya kuonja ladha ya upendo angalau toka upande mmoja. Iwapo hawatawahi kuona upendo wa kindugu pande zote, hawataamini katika heshima, upendo na ushirikiano.
Usifanye makosa katika uchaguzi wa mwenza kwa sababu tayari una majeraha ya familia ulipotokea, ukiumizwa tena kwenye ndoa utakosa ladha na maana nzima ya maisha. Uchaguzi mzuri wa mwenza utakupa utulivu wa kuanzisha himaya mpya utakayoijenga kwa misingi yako na kufuta kumbukumbu za maumivu uliyopitia kwenye familia uliyotokea na utawafanya watoto wako na wajukuu kuishi katika misingi mizuri uliyoikosa.
Mwisho WA SoMo🙏🏽