Je, Ole Sabaya alipewa kibali na Magufuli kuhujumu uchumi?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Anaandika Wakili msomi Jonh Mallya,
Ni usiku wa manane. Lengai Ole Sabaya amelaza kichogo chake kwenye kiganja. Mwili wake ameulaza juu ya sakafu baridi akitazama dari la chumba cha mahabusu ambacho taa zake hazizimwi usiku-kucha.

Kelele za wenyeji zinamghasi, lakini hazimtoi kwenye lindi la mawazo, majuto na masikitiko. Anakumbuka alivyokua analala mahoteli makubwa bila kulipa. Anajua leo na siku nyingi zijazo hatolipia mahali pa kulala. Atalala bure.

Lakini wasiwasi wa kulawitiwa, kupigwa na wababe wa jela, kupewa adhabu na askari magereza na hofu ya kukutwa na hatia au kuongezewa mashtaka vinamnyima raha.

Anajuta na haoni tumaini mbele yake. Anamkumbuka mwendazake. Anatamani ajiunge nae, lakini hana fursa ya kufanya hivyo. Anajuta kwanini alizaliwa, lakini hawezi kulaumu wazazi wake. Anajuta kuteuliwa, lakini anajua kuna wenzake waliteuliwa na hawakufanya mabaya aliyofanya yeye.

Anajisikia dhalili. Amevaa sweta, lakini anahisi baridi. Yuko na watu wengi lakini anajihisi mpweke!

Anakumbuka mazungumzo yake na Godbless Lema, alivyomwambia aliyekuteua sio Mungu. Anatamani siku ijirudie aukubali ule ushauri wa Lema, lakini haiwezekani tena. Anajipa moyo huenda atashinda vita hii, lakini akitafakari haoni mwanga. Dunia nzima inajua ubaya wake.

Amechoka kulala kwa mgongo, anajaribu kugeuka alale kwa ubavu, lakini mtu wa pembeni yake ni mnene na anakoroma kwa nguvu. Anatamani apate angalau konyagi ndogo imsaidie kulala, lakini Kisongo ni gereza lenye ulinzi mkali. Hawezi kupata huduma hiyo kwa sasa.

Anawakumbuka viongozi waliokua marafiki zake. Anajipa moyo huenda wakamsaidia. Lakini anakumbuka nao wanatafuta uteuzi, hivyo hawawezi kusimama upande wake kwa sasa.

Anafumba macho kuzuia machozi. Anatamani apate usingizi alale ili mawazo yakatishwe, lakini wapi!

Anasikitika tena. Anailaani siku Mwendazake alipokufa. Anailaani siku aliyoenda Takukuru kwa wito wa barua. Analaani ndugu zake ambao hawakumshauri aache ubaya. Analaani marafiki zake waliokua wanamsifia na kumuita jembe.

Anainua mkono kutazama muda, lakini hakuna saa mkononi. Anakumbuka yuko jela na huko saa, mkanda na viatu haviruhusiwi.

Anajisonya kimoyomoyo,
Anajitukana, anajilaani.!

My Take
Sabaya ana kesi ya uhujumu uchumi,ubakaji na matumizi mabaya ya madaraka aliyofanya kipindi cha utawala wa Magufuli. Alifanya yote haya huku Wilaya na Mkoa ukiwa na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo TISS. Walikuwa wapi?

Haya, Chadema walipiga kelele, Mbowe alipiga kelele, Lema akaonya. Mitandao ya kijamii ikaweka mambo hadharani. Lakini Rais aliyemteua hakufanya chochote. Akasema wewe chapa kazi.

Swali: Je Sabaya alipewa kibali cha kuhujumu uchumi?
 
Tabia binafsi za mtu zisihusishwe na Mtu/watu wengine.

Kama mzazi anashindwa kutambua kuwa Binti yake huwa ananyanduliwa, anakuja kushangaa tu Binti ana Mimba,

Sembuse Hayati aliekuwa na majukumu ya Taifa zima aisee..

NOTE: kuhusisha upuuzi wa sabaya na Ethics za hayati Magufuli ni upuuzi wa SGR.
 
Ujumbe huu,majuto hayo na mafunzo yaliyo ndani yake natamani vingewafikia wote wenye mamlaka,au dhamana yoyote katika jamii ili kwa pamoja tuijenge jamii iliyobora,taifa na ulimwengu uliokuwa bora wenye kuheshimu utu na haki kwa wote.
 
... sahihi kabisa; uchumi wa Kaskazini.
 
Mbona mifano yako hata haiendani kabisa, yaani mabaya ya kiongozi uyafananishe na mambo ya mahusiano ya mzazi na mtoto!!ni mala ngapi mabaya ya sabaya yalibainishwa tena kwa ushahidi wa sauti/video lakini mwendazake ndio kwanza alikuwa akizidi kumpenda, ili kuwananga watu?!!nani alikwambia kazi ya rais ni kufuatilia kila jambo la nchi linaloendelea kila siku?ndio maana kuna ma DSO, RSO, ndio kazi zao, je hao wa wilaya ya hai na mkoa wa kilimanjaro si walikuwepo?lakini kwa kuwa alikuwa na baraka zake hakuna wa kumfanya kitu, kwani makonda yale yote aliyokuwa anayafanya yanatofauti gani na hayo ya sabaya?lakini si alikuwa akiambiwa chapa kazi?
 
mfano wa kitoto huo. Rais anavyombo isitoshe watu walisema. Samia yeye kaonaje?
 
Sabaya ni picha halisi ya mamlaka iliyo mteua!
 
Majuto mjukuu
 
Magufuli as a president alikuwa anajua sana tu na akakaa kimya so alikuwa anahusika na huu udhalimu maana yeye mwenyewe alikuwa dhalimu sana kachukua pesa za watu mpaka wakakimbia nchi.
 
Alipewa kibari cha mdomo ambacho akiwezi Kumsaidia..

Jk Alisema Zakuambiwa Changanya na Zako..
 
Mwendazake kufuatilia Kila kitu ndo Ilikua Kazi Yake..
 
Hii kesi Ole Sabaya ATASHINDA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…