1. majini hayapo kwenye ukristo, yapo kwenye uislamu tu. bibilia ambayo haijatafsiriwa haitaji majini, bibilia ya kiingereza tu haitaji majini.
Mkuu… Neno JINI lisikuchanganye maana limetoka ktk lugha ya KIARABU.
Ukisema MAJINI yapo kwenye UISLAMU tu ina maana mwanzo wa kuwepo kwao duniani umeanza baada ya MUHAMMAD kuanzisha UISLAMU,
SI KWELI.
MAJINI… yalikuwepo tangu kale pia hawa majini ni malaika walioasi kwa mujibu wa BIBILIA.
Haya yote ni majina ya kutambulisha MAJINI… kwa mujibu wa BIBILIA.
PEPO
PEPO WABAYA
PEPO WAOVU
ROHO WAOVU
SHETANI
MASHETANI
IBILISI
MJARIBU
Njia ya kujua kuwa hao nlio wataja ndio hao hao ambao waliitwa MAJINI baada ya UISLAMU kuja.
Sifa yao kubwa ni kuharibu yaan… Kumpagaa mtu
Kumpa ugonjwa mtu(kukudhuru)
Kuharibu mimba (tasa)
Kuangamiza (kukuua)
Na mengineyo…
__________________________
Kwa mujibu wa Bibilia hakuna PEPO MWEMA (JINI) maana woote walisha laaniwa na Mungu hivyo hawana TOBA hata wapige MAOMBI vp, hivyo nashangaa MUISLAMU akiniambia kuwa JINI mwema anafanya MAOMBI kama watu wanavyofanya MAOMBI!
Huwa najiuliza hayo maombi ya maJINI anayajibu Mungu gani!!?
Kumbe yanajibiwa na mungu ALLAH.
Pia ukisoma injili kuna sehemu YESU KRISTO alisimangwa juu ya NGUVU anazo tumia kuponya watu wenye PEPO.
aliambiwa hivi….… Mathayo 12:23-24
23 Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi?
24 Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.
__________________________
Ukisoma huo mstari wa 24 unakuja kuona kuwa MAFARISAYO waliamini na walijua kuwa mkuu wa pepo ni beel-zebuli ambaye ndiye IBILISI au SHETANI tumwitavyo sisi waswahili.