Je, Pole Pole atarejea sasa Tanzania? Usalama wake ukoje ikiwa ataamua kurejea? Namshauri asirejee sasa.

Je, Pole Pole atarejea sasa Tanzania? Usalama wake ukoje ikiwa ataamua kurejea? Namshauri asirejee sasa.

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
12,151
Reaction score
44,120
Nimekaa nimewaza hilo, kwa namna Balozi aliyejiuzuru Humphrey Pole Pole alivyoinanga hadharani serikali ya sasa ya Tanzania, CCM na vyombo vya dola, huku akiharibu kabisa taswira ya Mama Samia kitaifa na kimataifa kwa uamuzi wake wa kujiuzuru huku akitoa sababu mujarabu.
Je, atarejea sasa Tanzania?
Na je akirejea usalama wake ukoje?

USHAURI WANGU.
Humphrey Pole Pole asijaribu kabisa kurejea tena hapa Tanzania kwa kipindi hichi, ni vyema akatafuta ukimbizi wa kisiasa huko USA au Ulaya, maana akirejea tu, haya yatamkuta:

1. Atanyang'anywa pasi yake ya kusafiria na hataruhusiwa kusafiri popote.

2. Atakamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi, uhujumu uchumi au uhaini.

3. Wasiojulikana wanaweza kufanya kazi yao.
 
Japo siwezi kushangaa hayo yakitokea lkn ametenda kosa gani au ndio mwendelezo wa ubaya ubwela
Binafsi mimi niko upande wake
 
CCM imepoteza dira - Horace Kolimba

Baada kutoa kauli hiyo aliwekewa sumu kwenye mic akafa.

Ni vizuri kurejelea historia, nafikiri Polepole hili somo analo.
 
Ama hakika Polepole ameonesha ujasiri wa hali ya juu sana. Kamchoma Samia na kitu cha ncha kali jichoni.
 
Kwa hatua hii, kuna picha flani inakuja kama kimenuka hivi. Kuanzia kwa PM, na sasa hili hapa. Mengi yabakuja bila shaka
 
Back
Top Bottom