Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 24,523
- 30,084
JF of GT wamo lakini hawana sauti na wanawindwa kama faru weupe.
JF of GT wamo lakini hawana sauti na wanawindwa kama faru weupe.
Naunga mkono hoja, hii ndio Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huu ndio Mhimili wa Mahakama za JMT ambao ndio uko responsible kutoa haki, na kilichofanyika jana, ndio utoaji haki wenyewe ndani ya JMT.Hakika Tanzania nchi yangu inapitia kipindi kigumu Sana tangu ipate Uhuru wake mwaka 1961!
Kwamba Sheria na Katiba za nji hii zinapindishwa na Mahakama kumfurahisha mtu mmoja kwa manufaa ya Chama Fulani...!
Kwamba Jeshi la Polisi limehusika na MAUAJI ya Raia mwema asie na hatia Bi Acqulina Akwilina (NIT Student)na imethibitika pasipo na Shaka ndani na nje ya Mahakama Polisi wameua. Serikali na Jeshi la Polisi wakashiriki maziko ya marehemu na Serikali kuahidi kuisaidia familia ya Marehemu KUMSOMESHA MDOGO wa marehemu Acqulina...!
Lakini Mara baada ya MAZISHI tu unasukwa mpango kabambe wa kuwakomoa Viongozi wa CHADEMA kuwa wao ndio walomwua marehemu..!
Kesi inapikwa, mashtaka yanatengezwa, ushahidi wa kughushi unabumbwa na Hukumu inaandaliwa kwa miaka 2 na inatolewa MWAKA WA UCHAGUZI 2020...!
WAUAJI MAPOLISI HAWAKULIPA HATA SENTANO WALA KULALA SEGEREA LAKINI VIONGOZI WA CHADEMA AMBAO HAWAKURUSHA HATA KARATASI NDIO WAMETIWA HATIANI KWA MAKOSA 12 KWA KIFUNGO CHA MIEZI 5 KILA KOSA AU FAINI YA TSHS. 350 MILIONI....!!
Huu ni UONEVU,UDIKTETA NA UNYANYASAJI KWA VIONGOZI WOTE WA CHADEMA NA WANACHAMA WAO..!!!
Mahakama zetu zinapotoa haki mimi humuona jaji mkuu mstaafu akiwa ikulu na kusema hakuna wakati ngumu unaozipata mahakama kama kutoa hukumu kwa maelekezo toka nje! Alitoa maneno hayo baada ya kustaafu, aliyaficha moyoni akiwa kazini! Na yule jaji mkuu mstaafu wa kesi ya Mrema kuhusu mamilioni ya BM, naye alisema alipata wakati mgumu kutoa hukumu ambayo ilimnusuru BM kuondoka madarakani, hii ni kesi pekee ambayo mshitaki na mshitakiwa wote walishinda! Bunge wakati ule lililazimisha kumkuta Mrema na hatia ya kusema uongo na kuipeleka kesi mahakamani.Naunga mkono hoja, hii ndio Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huu ndio Mhimili wa Mahakama za JMT ambao ndio uko responsible kutoa haki, na kilichofanyika jana, ndio utoaji haki wenyewe ndani ya JMT.
P
KabisaDuh...!. Huyu binti ameuliwa na watu wengine, halafu watu wengine ndio wanashitakiwa na kuhukumiwa!.
All and all, haki kamwe huwa haipotei, aliyemuua Aquiline kama bado hajafidia, ni lazima tuu atafidia, karma haina mswalie Mtume.
Na waliohukumiwa kwa dhulma na uonevu kwa kosa ambalo hawakulifanya, watafidiwa!.
Tanzania we have a long way to go hadi haki ya kiukweli kweli itendeke na kuonekana imetendeka!.
Justice must not only be done, but must also be seen to be done.
P
Watanzani tudai katiba mpya tuu ndio suluhisho la sarakasi zote hiziMahakama zetu zinapotoa haki mimi humuona jaji mkuu mstaafu akiwa ikulu na kusema hakuna wakati ngumu unaozipata mahakama kama kutoa hukumu kwa maelekezo toka nje! Alitoa maneno hayo baada ya kustaafu, aliyaficha moyoni akiwa kazini! Na yule jaji mkuu mstaafu wa kesi ya Mrema kuhusu mamilioni ya BM, naye alisema alipata wakati mgumu kutoa hukumu ambayo ilimnusuru BM kuondoka madarakani, hii ni kesi pekee ambayo mshitaki na mshitakiwa wote walishinda! Bunge wakati ule lililazimisha kumkuta Mrema na hatia ya kusema uongo na kuipeleka kesi mahakamani.
Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huyu
![]()
Wanabodi,
naomba niwafariji wafiwa na wapenda haki wote kuwa, hata kama nothing will be done, there is karma ambayo haina mswalie mtume!. When karma takes its toll, kama tutakuwepo, tutawakumbusha.
Paskali
Bundi wa karma ya Aquiline sasa limeibuka kutaka kudandia upepo wa Corona ulipaishe kuelekea kule mahali na saa hizi bundi hili linarandaranda kule juu ya ule mjengoni likisubiri giza liingie ndipo litue!.Naekekea jimbo la Kinondoni bundi mimi
sichangii chochoteBundi wa karma ya Aquiline sasa limeibuka kutaka kudandia upepo wa Corona ulipaishe kuelekea kule mahali na saa hizi bundi hili linarandaranda kule juu ya ule mjengoni likisubiri giza liingie ndipo litue!.
Itabidi tuwahi kuwaona 'wazee' kumzuia huyo bundi asije kutua juu ya paa ya lile jengo letu pale...
Maana...
P
Bundi mimi huwa nafanya kazi yangu alfajiri. Mwili unakuwa ume relax basi hapo mimi najipitia tu kuchukua changu!Bundi wa karma ya Aquiline sasa limeibuka kutaka kudandia upepo wa Corona ulipaishe kuelekea kule mahali na saa hizi bundi hili linarandaranda kule juu ya ule mjengoni likisubiri giza liingie ndipo litue!.
Itabidi tuwahi kuwaona 'wazee' kumzuia huyo bundi asije kutua juu ya paa ya lile jengo letu pale...
Maana...
P
Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huyu
![]()
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali tuu nikiuliza, Jee mnajua Jeshi la Polisi linaweza kushitakiwa mahakamani kwa kusababisha vifo vya kizembe?. Japo kifo hiki cha malaika huyu kimetokea kwa bahati mbaya bila kukusudiwa, na kwa vile hili sii tukio la kwanza kwa jeshi letu la polisi, nikichukulia mauaji ya Mwanza ya mwaka 1976, Waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo, Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu right on the spot, sioni mpaka leo, Comred Mwigulu anafanya nini ofisini!.
Japo tumesikia wahusika wote wametiwa ndani kwa uchunguzi, naomba kuwapa angalizo kuwa kwa vile hakuna ushahidi wa picha kama kifo cha Mwangosi, hivyo msishangae wahusika wote wakalindwa, na ikatolewa taarifa, Akwilina amefariki kutokana na risasi iliyofyatuliwa na wasiojulikana, hivyo hakuna uchunguzi wowote, wala mashitaka yoyote, halafu Mwigulu ataendelea tuu na kazi, with clear conscious as if nothing happened, naomba niwafariji wafiwa na wapenda haki wote kuwa, hata kama nothing will be done, there is karma ambayo haina mswalie mtume!. When karma takes its toll, kama tutakuwepo, tutawakumbusha.
Kuna mazingira ambayo polisi wanaweza kumuua raia wa kawaida katika polisi shootout na polisi wasiwe na criminal liability kama tukio hilo linahusisha matumizi halali ya risasi za moto kwa mujibu wa miongozo yao, lakini tukio lile ni kuthibiti riots, hivyo tangu lini jeshi la polisi linatumia risasi za moto kuthibiti riots za watu wasio na silaha zozote badala ya kutumia rubber bullets?!.
Tena kuna ushahidi wa kutosha na usiotia shaka, mara nyingi uvunjifu wa amani unasababishwa na polisi wanaodhibiti maandamano hayo!. Kama polisi wangesimamia na kuwapa ulinzi Chadema katika kufuata viapo vyao ili wakiona vurugu ndipo waingilie kati, what did they stand to loose?.
Kilichotokea ni uzembe tuu wa polisi wetu na hakuna excuse yoyote itakayo weza kutolewa ku justify uzembe huu wa jeshi letu la polisi kupoteza maisha ya an innocent civilian just like that na huku waziri bado yuko tuu ofisini!, anasubiri nini?. Kama mahabusu wawili tuu walitoroka Ukonga maximum prison na waziri akajiuzulu, ameuliwa Mwangosi, hakuna aliyewajibika, sasa Akwiline, its the same, hivi mpaka wafe watu wangapi ndipo dhana ya uwajibikaji itawaingia viongozi hawa wetu wa leo?. Kiukweli nimemkumbuka Mwalimu Nyerere!.
Poleni sana, wazazi, wanafunzi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, wana Kinondoni wote na wote walioguswa na kifo hiki, japo mimi ni mwandishi wa habari tuu ila nimesomea sheria, kazi ya uandishi naifanya kwa mapenzi tuu, lakini sasa naanza kujitafakari upya, kwa kupima nitakuwa na msaada gani kwa jamii nikilinganisha kuendelea na uandishi au kuingia kwenye sheria kuielimisha jamii haki zao?.
Serikali yetu lazima itoe taarifa rasmi kulaani mauaji haya, na ikibidi kugharimia mazishi, na kutoa pole nene ya ubani, kuwafariji wafiwa na kuwapooza, ili wasiende mahakamani!. Kifo cha Imran Kombe, mjane aliishitaki Serikali mahakamani na kulipwa kifuta machozi cha shilling milioni 300!.
Kama hizi ndizo gharama za demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuzilipia kwa kuzingarimia kwa machozi, jasho na damu, ili tuu kulazimisha chama fulani lazima kishinde uchaguzi!, bora tufute kabisa hivi vyama vingi, turudi kwenye mfumo wa chama kimoja, CCM iachwe itawale peke yake!. Lakini yote haya Mungu yupo na haya anayaona, hivyo utakapofika wakati wa karma taking it's toll kwa wahusika waliopaswa kuchukua hatua, but they didn't, tusijifanye kushangaa na kujiuliza why?.
Rip, mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa kozi ya Procurement $ Logistics Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Aqulina Akwilini Baftaha, baada ya kufariki kwa dunia kwa kupigwa risasi iliyompata akiwa ndani ya basi la dala dala lililopita eneo la tukio.
Paskali
Wanabodi,
Wewe kama mwana JF, unapata an added advantage to be the first to know, ambapo leo katika tukio la maboresho ya jeshi la polisi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ametoa kauli kwa kutumia fasihi, ambapo ameliamuru jeshi la polisi, kukabiliana na majambazi wenye silaha kwa "kuwanyang'anya silaha kwa haraka haraka" ambapo polisi wameruhusiwa kutumia mbinu za medani, (kivita) (MM) ambazo hutumiwa na majeshi wakati wa vita, ambapo kazi huwa ni moja tuu, kumteketeza adui!.
Amri hiyo kwa Jeshi la Polisi, inamaanisha, Polisi hawahitaji tena kuwakamata majambazi wanaotumia silaha, bali kukabiliana nao kwa kuwaua papo kwa papo, na polisi wataofanya mauaji hayo ya kuwauwa majambazi hayo papo kwa papo bila kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, hawatafikishwa tena mahakamani, kama zamani, bali sasa watapandishwa vyeo!.
Tanzania ni nchi ya kidemokasia inayofuata katiba yenye kuzingatia misingi ya haki na utawala wa sheria!, amri kuu ya kwanza ya haki, ni "no one is condemned unheard", yaani hakuna mtu atakayehukumiwa bila kusikilizwa!. Amri hii ya rais, imewapa mamlaka polisi, sio tena kuchunguza, kukamata na kuwapeleka majambazi wanaotumia silaha, mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, bali sasa polisi hawana tena haja ya kukamata na kufanya uchunguzi, bali kukitokea tuu tukio la uhalifu wa kutumia silaha, polisi wamepewa mamlaka kuwa ni wachunguzi, prosecutors, mahakimu tena kwa kutoa "capital punishment", na hakuna tena haja ya kumsubiri rais kuzisaini hizo hati za capital punishment, bali, wao wenyewe kutumia MM, kuitekeleza adhabu ya kifo, na baada ya hapo kusubiria kupandishwa vyeo!.
Jumamosi Njema.
Paskali
Rejea.
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa .
Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa ..
Ni katika kukumbushana tuu, kuwa jeshi la polisi, likifanya madudu, linashitakika!, wasio shitakika ni wale jamaa zetu na JWTZ!.Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali tuu nikiuliza, Jee mnajua Jeshi la Polisi linaweza kushitakiwa mahakamani kwa kusababisha vifo vya kizembe?. nikichukulia mauaji ya Mwanza ya mwaka 1976, Waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo, Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu right on the spot, sioni mpaka leo, waziri anafanya nini ofisini!.