Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huyu
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali tuu nikiuliza, Jee mnajua Jeshi la Polisi linaweza kushitakiwa mahakamani kwa kusababisha vifo vya kizembe?. Japo kifo hiki cha malaika huyu kimetokea kwa bahati mbaya bila kukusudiwa, na kwa vile hili sii tukio la kwanza kwa jeshi letu la polisi, nikichukulia mauaji ya Mwanza ya mwaka 1976, Waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo, Ali Hassan Mwinyi alijiuzulu right on the spot, sioni mpaka leo, Comred Mwigulu anafanya nini ofisini!.
Japo tumesikia wahusika wote wametiwa ndani kwa uchunguzi, naomba kuwapa angalizo kuwa kwa vile hakuna ushahidi wa picha kama kifo cha Mwangosi, hivyo msishangae wahusika wote wakalindwa, na ikatolewa taarifa, Akwilina amefariki kutokana na risasi iliyofyatuliwa na wasiojulikana, hivyo hakuna uchunguzi wowote, wala mashitaka yoyote, halafu Mwigulu ataendelea tuu na kazi, with clear conscious as if nothing happened, naomba niwafariji wafiwa na wapenda haki wote kuwa, hata kama nothing will be done, there is karma ambayo haina mswalie mtume!. When karma takes its toll, kama tutakuwepo, tutawakumbusha.
Kuna mazingira ambayo polisi wanaweza kumuua raia wa kawaida katika polisi shootout na polisi wasiwe na criminal liability kama tukio hilo linahusisha matumizi halali ya risasi za moto kwa mujibu wa miongozo yao, lakini tukio lile ni kuthibiti riots, hivyo tangu lini jeshi la polisi linatumia risasi za moto kuthibiti riots za watu wasio na silaha zozote badala ya kutumia rubber bullets?!.
Tena kuna ushahidi wa kutosha na usiotia shaka, mara nyingi uvunjifu wa amani unasababishwa na polisi wanaodhibiti maandamano hayo!. Kama polisi wangesimamia na kuwapa ulinzi Chadema katika kufuata viapo vyao ili wakiona vurugu ndipo waingilie kati, what did they stand to loose?.
Kilichotokea ni uzembe tuu wa polisi wetu na hakuna excuse yoyote itakayo weza kutolewa ku justify uzembe huu wa jeshi letu la polisi kupoteza maisha ya an innocent civilian just like that na huku waziri bado yuko tuu ofisini!, anasubiri nini?. Kama mahabusu wawili tuu walitoroka Ukonga maximum prison na waziri akajiuzulu, ameuliwa Mwangosi, hakuna aliyewajibika, sasa Akwiline, its the same, hivi mpaka wafe watu wangapi ndipo dhana ya uwajibikaji itawaingia viongozi hawa wetu wa leo?. Kiukweli nimemkumbuka Mwalimu Nyerere!.
Poleni sana, wazazi, wanafunzi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, wana Kinondoni wote na wote walioguswa na kifo hiki, japo mimi ni mwandishi wa habari tuu ila nimesomea sheria, kazi ya uandishi naifanya kwa mapenzi tuu, lakini sasa naanza kujitafakari upya, kwa kupima nitakuwa na msaada gani kwa jamii nikilinganisha kuendelea na uandishi au kuingia kwenye sheria kuielimisha jamii haki zao?.
Serikali yetu lazima itoe taarifa rasmi kulaani mauaji haya, na ikibidi kugharimia mazishi, na kutoa pole nene ya ubani, kuwafariji wafiwa na kuwapooza, ili wasiende mahakamani!. Kifo cha Imran Kombe, mjane aliishitaki Serikali mahakamani na kulipwa kifuta machozi cha shilling milioni 300!.
Kama hizi ndizo gharama za demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuzilipia kwa kuzingarimia kwa machozi, jasho na damu, ili tuu kulazimisha chama fulani lazima kishinde uchaguzi!, bora tufute kabisa hivi vyama vingi, turudi kwenye mfumo wa chama kimoja, CCM iachwe itawale peke yake!. Lakini yote haya Mungu yupo na haya anayaona, hivyo utakapofika wakati wa karma taking it's toll kwa wahusika waliopaswa kuchukua hatua, but they didn't, tusijifanye kushangaa na kujiuliza why?.
Rip, mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa kozi ya Procurement $ Logistics Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Aqulina Akwilini Baftaha, baada ya kufariki kwa dunia kwa kupigwa risasi iliyompata akiwa ndani ya basi la dala dala lililopita eneo la tukio.
Paskali
PIA SOMA
- Maandamano ya CHADEMA: Aqulina Akwilini Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika