Je, Poulsen kumng'oa Zahera Yanga ?

Je, Poulsen kumng'oa Zahera Yanga ?

We mechi za Yanga sijui hata kama unaangaliaga naona unaandika maneno mengiii.

Zahera ukiangalia msimu huu toka umeanza yaani kila mechi hakuna mabadiliko yoyote ya kiuchezaji timu ndo inazidi kucheza ovyo kila mechi sasa nani wa kuwajibika?

Timu inacheza mpira haueleweki yani ni kubutua butua tu sasa kocha anafanya kazi gani?

Wachezaji alowataka wote wameletwa na hawaonekani kuonyesha hata kiwango nani wa kuwajibika hapo?
Ndugu Tony92 nafikiri umenielewa vibaya. Rejea kwenye post zangu namba 14 na 29 kwenye uzi huu ndio utapata nini nilichomaanisha. Mimi sijamuunga mkono Zahera kabisa bali natamani Yanga impate Poulsen halafu wawe wavumilivu kwa angalau miaka mitatu ili aunde timu ya ushindani (maana ni muumini mzuri wa soka la vijana) ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania. Lakini mdau mmoja akasema watavumilia vipi kufungwa na boda boda FC kwa muda wote huo? Ndipo nilipomjibu kuwa tunapaswa kutoka kwenye fikra za Simba kamfunga Yanga au Yanga kamfunga Simba badala yake tujikite kwenye CAF champions ligi ili iwe kawaida kwa timu za Tanzania kufika mbali kwenye mashindano hayo na hapo hizi timu zetu zitakuwa zinaingiza pesa nyingi badala ya sifa tu nani kamfunga nani.
 
Back
Top Bottom