Je, Poulsen kumng'oa Zahera Yanga ?

wachezaji aliokuwa anawataka zahera yanga hawakumletea. Zahera alikuwa anawataka kina Mo Salah, Messi, Ronaldo halafu nyie mnamletea kina balinya halafu bado mnalalamikia matokeo
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Ndugu Tony92 nafikiri umenielewa vibaya. Rejea kwenye post zangu namba 14 na 29 kwenye uzi huu ndio utapata nini nilichomaanisha. Mimi sijamuunga mkono Zahera kabisa bali natamani Yanga impate Poulsen halafu wawe wavumilivu kwa angalau miaka mitatu ili aunde timu ya ushindani (maana ni muumini mzuri wa soka la vijana) ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania. Lakini mdau mmoja akasema watavumilia vipi kufungwa na boda boda FC kwa muda wote huo? Ndipo nilipomjibu kuwa tunapaswa kutoka kwenye fikra za Simba kamfunga Yanga au Yanga kamfunga Simba badala yake tujikite kwenye CAF champions ligi ili iwe kawaida kwa timu za Tanzania kufika mbali kwenye mashindano hayo na hapo hizi timu zetu zitakuwa zinaingiza pesa nyingi badala ya sifa tu nani kamfunga nani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…