SI KWELI Je, Pundamilia anaweza kuzaliana na Ng'ombe pamoja

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo na chapisho lililosambazwa kwenye ukurasa wa Facebook likimnukuu mfugaji mmoja nchini Kenya akilalamikia uwepo wa zebra katika eneo lake. Mfugaji huyo anadai kuwa zebra hao wanazaliana na ng’ombe pamoja na punda wake, hali inayosababisha kuzaliwa kwa wanyama wenye madoa yanayofanana na ya zebra.

pia kupitia chapisho ambalo limechapishwa na ukurasa wa instagram wa safari podcast lina nukuu kuwa “Ninaiomba Mamlaka ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) waje kuwachukua zebra hawa. Wamekuwa wakizaliana na ng’ombe wangu, na tayari kuna ndama aliyezaliwa akiwa na madoa kama ya zebra. Endapo hamtachukua hatua mapema, nitalazimika kuwaua zebra hao. Nawasisitiza mfike haraka kuwaondoa, kwani pia wamezaliana na punda wangu, na kusababisha kuzaliwa kwa punda mwenye madoa kama ya zebra.”
je ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
 
Tunachokijua
Madai

Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na kipande cha video pamoja na taarifa zinazosambaa zikielezwa kuwa mkazi mmoja wa Kenya amelalamikia uwepo wa Pundamilia karibu na makazi yake na hivyo kupelekea pundamilia hao kuingiliana na ng'ombe wake na hivyo kuzaliana.

Je, inawezekana Pundamilia na Ng'ombe kuingiliana na hivyo kupata watoto?

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa kabailoji Pundamilia hawezi kuzaliana na punda milia kutokana na wao kutokea katika familia tofauti yaani ngo'ombe anatokea kwenye familia ya Bovidae wakati Ngo'ombe anatokea familia ya Equidae.

Pia kuna tofauti zingine kama viungo vya uzazi, umri wa mimba, namna mimba inatungwa n.k. Kwa namna hiyo hawa ni wanyama wawili tofauti kabisaaa kijenetiki!

Ila upande wa pili: Punda, pundamilia na farasi wanaweza kuzaa mtoto kwa kuwa wao ni familia Moja ya Equidae/ Equine.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…