Habari wana JF...
Kuna mambo yanaendelea ktk nchi hii ni makubwa na ya ajabu.
Yasiposemwa huko mbele hatutaweza kupona kama Taifa.
Mnaweza mkachagua kunyamaza ila gharama ya kuja kurekebisha haya mambo ikawa kubwa sana.
Mabadiliko ya kisheria yanayoendelea Tz tena kwa "Hati za dharura" yanaondoa kabisa mifumo ya kitaasisi na kuotesha mifumo-watu.
Moja, Sheria ya Vyama vya siasa ikamfanya Mtu mmoja aitwaye "Msajili wa Vyama vya Siasa" kuwa mwamuzi wa kila kitu juu ya masuala yote ya vyama kuanzia madai hadi jinai.
Yani leo kwa sheria ile "Msajili" anaweza kuamua chochote juu ya chama na hata ikiwa ni kwa hisia tu.
Kwa wenye busara huko nyuma, makosa yote yalipelekwa ktk mahakama ambapo ushahidi pasi na shaka pande zote ulihitajika ili kuhukumu.
Leo "Msajili" tu anatosha kusema, mfano, 'Ktk kikao cheni mlimualika mgeni bila ruhusa yangu, nawafungia kufanya vikao miezi sita'.
Ule mfumo mpana wa kimahakama, umemezwa na mtu-MSAJILI.
Mbili, Ipo sheria pendekezwa (muswada) sasa ya vyama vya kijamii na asasi za kiraia. Na kwenyewe kuna Mtu msajili ambae anakuwa ktk Wizara ya Mambo ya ndani amepewa manguvu ya kuamua kwa uoni/utashi wake.
Yani huyu msajili akihisi kuna jinai anakufutilia mbali. Ni HISIA tu, au hata akiambiwa tu. ANAFUTA.
Haina kubisha. Ndio ana mamlaka hayo. Si mahakama wala nini. Ni Yeye Mtu-Msajili.
Na hawa wote ni Wateule wa Rais. Na Yeye Rais anaweza kuwatengua wkt wowote.
Nadhani mnauona mfumo mtu hapo.
Tatu, hii ndio funga kazi. Upo muswada unaopendekeza kuanzishwa kwa "Ofisi ya kushughulikia Malalamiko ya walipa kodi" chini ya Wizara ya Fedha.
Huu ni mfumo-mtu. Kama wabunge wetu wana akili wasipitishe hiki kitu. Kiufupi, mfumo wa kushughulikia malalamiko na madai ya kikodi upo mpaka sasa tena kisheria kabisa. Ambacho wabunge wangeweza fanya ni kuuboresha. Mfano kuangalia gharama na urahisi wa kila mfanyabiashara kuufikia.
Unaachaje mfumo wa kisheria wa kusuluhisha mapingamizi na malalamiko ya kodi!!!!, unaenda kuweka dawati kwenye wizara eti lishughulikie malalamiko ya wafanyabiashara Tanzania nzima?!!
Je, ni lini mfanyabiashara ataenda kulalamika wizarani??. Je, ule mfumo wa TRA kushtakiwa kwenye mabaraza na bodi za rufani za kodi, hadi Mahakama ya Rufaa unakufa??
Sasa atawekwa mtu (mfumo-mtu) pale Wizarani na atasikiliza vilio vya wafanyabiashara na kuamua.
Je, wasipokubaliana hapo, wanaenda wapi??
Kiufupi TRA inaenda kumezwa, Bodi na Mabaraza ya Rufani za kodi vinenda kumezwa pia.
Sasa kodi itakadiriwa na kulipwa pale kwenye dawati la Wizara ya Fedha. Simple!
Kwa nini mifumo-watu inapendwa sana na JPM kuliko Taasisi?
Endeleeni kutafakari...