Tetesi: Je, Rais Magufuli anaondoa mifumo ya kitaasisi na kuweka mifumo-watu?

Tetesi: Je, Rais Magufuli anaondoa mifumo ya kitaasisi na kuweka mifumo-watu?

Ukishaona kiongozi anahubiri uzalendo na anahakikisha watu wote wanaamini uzalendo ni matendo yake, na hapo hapo hataki katiba yenye maoni ya watu, tena anaongea hivyo hadharani, hapo ujue kuna balaa kubwa. Matokeo yake hataki katiba mpya, lakini anahakikisha utashi wake ndio unageuzwa kuwa sheria na watu wako kimya, katika mazingira hayo ujue siku wananchi watataka kutoka kwenye hizo sheria basi damu lazima imwagike.
Akishajenga maisha nje ya taasisi na sheria ajue sote (hata yeye) hatakuwa salama tena.
 
KaZijua akili za waTz kuwa hawawezi lolote ndio maana anafanya yale ayaonayo na bunge letu si la kuhoji hasa kwa wengi hivyo tutarajie mengi zaidi
Shida ni kwamba uwezo wake ni mdogo, hata ile global politics haielewi kabisa. Ogopa mungu-mtu asiye na maarifa, ni uharibifu tu
 
Wabunge ndio wawakilishi wetu wakishaamua kunengua na kuitikia kila wimbo "ndiyooo...." huku wanaopinga upuuzi wakiitwa wasaliti na kufukuzwa bungeni...
Kazi tunayo...
Huko mbele hii kazi ni ngumu na ya kuchosha. Labda tugeuze kibao 2020.
 
Serikali ya Ccm ni Ovu, dhaifu na ya hovyo kuwahi kutokea toka tupate uhuru?

"Mith 28:1 "Waovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayewakimbiza, lakini waadilifu wana ujasiri kama simba"

Serikali ya Ccm chini ya Magufuli

1.Imeshindwa kuwawezesha wakulima kupata pembejeo kwa bei nafuu na kuwapatia masoko ya uhakika wa mazao yao.

2.Wafanyabiashara wamebanwa na kodi za kubambikiziwa

3.Hakuna ajira mpya

4.Wafanyakazi wamebanwa hakuna nyongeza ya mshahara

5. Vyama vya siasa vimebanwa kufanya siasa

6. Watu wanatekwa na kuuawa hakuna mtu aliyekamatwa walakushutumiwa

7. Manunuzi yote yanafanywa na raisi mwenyewe

8 Serikali imejitoa OPEC

9. Miswaada zaidi ya kumi imepelekwa Bungeni ndani ya kipindi cha miaka mitatu tu miswaada hiyo imelenga:

1 Kubana uhuru wa kutoa maoni
2 Kutisha watu
3 Kuzuia Vyama vya upinzani kufanya siasa
4 Kuzuia uwazi katika uendeshaji wa serikali

Narudia tena kuuliza swali je serikali ya Ccm chini ya Magufuli ni Ovu, dhaifu na ya hovyo kuwahi kutokea?
"Ogopa sana mtu mroho ambae ni mchoyo pia". CCM ni waroho, wachoyo na wakatili.
 
Je tuwalaumu kina Ade Kilangi na Masaju, wanaoitumia taaluma yao ovyo kuliangamiza taifa? Wanasheria wa hovyo wanaotunga sheria kandamizi...
 
Wenye 'macho' tulishaliona hili tangu kipindi Cha uchaguzi maana watu waliambiwa wamchague huyu jamaa na sio chama kama ilivyo desturi yao miaka nenda rudi...
 
Watawala wetu wanapambana kufa kufa na kupona kuhodhi madaraka ya kisiasa. Pamoja na vyama vya siasa hofu yao nyingine ni asasi za kiraia. Marekebisho ya sheria mbalimbali kwa hati ya dharura yanakusudiwa kupunguza mchango wa asasi za kiraia katika mchakato wa chaguzi zijazo. Siyo siri kwambà asasi za kitaifa zipo karibu na jamii na zina ushawishi mkubwa. Watawala wetu wanahofu jamii iliyo na elimu ya uraia.
 
Wenye 'macho' tulishaliona hili tangu kipindi Cha uchaguzi maana watu waliambiwa wamchague huyu jamaa na sio chama kama ilivyo desturi yao miaka nenda rudi...
Aisee kwa hiyo ndio maana anajitapa kwamba fomu alichukua mwenyewe....!!!
 
Watawala wetu wanapambana kufa kufa na kupona kuhodhi madaraka ya kisiasa. Pamoja na vyama vya siasa hofu yao nyingine ni asasi za kiraia. Marekebisho ya sheria mbalimbali kwa hati ya dharura yanakusudiwa kupunguza mchango wa asasi za kiraia katika mchakato wa chaguzi zijazo. Siyo siri kwambà asasi za kitaifa zipo karibu na jamii na zina ushawishi mkubwa. Watawala wetu wanahofu jamii iliyo na elimu ya uraia.
Hofu ya viti walivyovikalia...
 
Magufuli anatamba kwa sababu bunge ni hovyo dhaifu na hawajitambui
wananchi uwezo wao mdogo mfinyu na hatujali kesho yetu
vijana matahira waoga wala chips mabazazi wapumbavu hawana uzalendo kulinda nchi yao bali kudandia vijisenti duniani pote nchi inalindwa na vijana dhidi ya udhalimu wvijana watanzania utasikia tangulia wewe na wanao
maraisi na viongozi wengine waliotangulia ni wanafiki i mabazazi na madumila kuwili yamenyamaza yakidhani yenyewe yapo salama
 
Je tuwalaumu kina Ade Kilangi na Masaju, wanaoitumia taaluma yao ovyo kuliangamiza taifa? Wanasheria wa hovyo wanaotunga sheria kandamizi...
Kilangi na mashamba watachomwa moto siku moja huwezi ukafikia nafasi ya kuitwa dokta wa sheria harafu ukaja kupitisha miswada usiku wa maanane kwa ajili ya kumlinda mtu mmoja stupido kabisa
 
Umenikumbusha a man of the people and an enemy of the people.. Moja ya novel zinazosadifu hali halisi nchini mwangu..
Wabunge ndio wawakilishi wetu wakishaamua kunengua na kuitikia kila wimbo "ndiyooo...." huku wanaopinga upuuzi wakiitwa wasaliti na kufukuzwa bungeni...
Kazi tunayo...
Aa
 
Huu mfumo uliasisiwa na Nyerere hawa wengine wanafuata nyayo tu, na ndio maana mihimili ya bunge na mahakama ni vibogoyo au umesahau kauli ya mkuu kuhusu muhimili uliojichimbia chini sana kuliko mwingine.
 
Hii hali inatisha sana ,Kila mwenye ufahamu naomba awe makini na kinachoendelea katika taifa letu.
 
Je tuwalaumu kina Ade Kilangi na Masaju, wanaoitumia taaluma yao ovyo kuliangamiza taifa? Wanasheria wa hovyo wanaotunga sheria kandamizi...

Msomi yeyeto masikini afai atarubunika Na mwenye Mali Kwa kutenda matakwa ya mwenye Mali. Umasikini una impact kwenye dhana ya uongozi pia.
 
Copy and paste from Nyerere ndie muasisi wa one man show ambalo jibu lake huwa ni total failure kila angle,yote haya ni marudio tu.Samaki ujikaanga Na mafuta yake mwenyewe
 
Back
Top Bottom